CCM yamwangukia Bashe
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimegeuka kuwa kigeugeu baada ya kumwangukia aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Hussein Bashe, kikimtaka akasaidie kukipigia kampeni katika jimbo la Nzega mkoani Tabora.
Habari za kuaminika zilizopatikana kutoka Nzega na Dar es Salaam jana, zinasema CCM imeteua zaidi ya makada 20 katika jimbo hilo, kwa ajili ya kukinadi chama hicho ambacho kinaonekana kupata wakati mgumu.
Bashe ambaye alitangazwa na CCM hivi karibuni na kuvuliwa nyadhifa zote na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), kisha kutangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa chama hicho, Kapteni John Chiligati, kuwa si raia, kunaibua maswali mengi kama uamuzi huo, ulikuwa sahihi.
Bashe ambaye alishinda kura za maoni kwenye jimbo la Nzega, lililokuwa likishikiliwa na Lucas Selelii, (CCM) na ushindi wake kupewa Dk. Hamisi Kigwangala ambaye amepitishwa rasmi kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Akitangaza uamuzi huo, baada ya kumalizika kwa kikao cha NEC cha mchujo wa wagombea ubunge na Baraza la Wawakilishi, Chiligati, alisema CCM imeamua kumtimua Bashe uanachama na kumuengua kuwania ubunge katika jimbo la Nzega, baada ya kubaini kuwa ni raia wa Somalia.
Endelea kusoma habari hii.............