Kibaki na Odinga kukutana Jumapili
Kwa mujibu wa taarifa ya Salim Lome msaidizi wa waziri wakuu viongozi hao wawili wanategemewa kujadili matatizo yanayoikabili serikali ya mseto ikiwa ni pamoja na suala la rushwa ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kazi kwa mawaziri wa elimu na kilimo.
Lakini wakati huo huo wafuasi wa Rais Mwai Kibaki wamepinga vikali kuhusika kwa Koffi Annan kwenye usuluhishi huo na walieleza kuwa ni bora aende huko Kenya kama mtalii tu lakini si kuingilia kati siasa za Kenya.
Msemaji huyo wa Odinga ameongeza kwamba tayari viongozi hao wameshafanya mazungumzo ya awali kwenye simu wakati Bw. Odinga akiwa ziarani huko Japan na kukubaliana kuwa watakutana siku ya Jumapili.
Kofi Annan aliyefanikiwa kuwashawishi kumaliza mzozo wao aliwasihi watilie maanani mazungumzo hayo na hasa masuala ya rushwa na mabadiliko muhimu kwenye taasisi za taifa.
No comments:
Post a Comment