JK ampa U-DC 'hasimu' wa Sophia Simba
Via Mwananchi
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa wilaya nchini kwa kumfukuza aliyeshindwa kusimamia sera ya Kilimo Kwanza, huku akimteua tena Husna Mwilima, ambaye alijikuta kwenye uhasama na Sophia Simba katika kipindi kifupi alichofanya naye kazi kwenye Umoja wa Wanawake wa CCM.
Mwilima, ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, na Martin Shigela, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Lindi, waliteuliwa kuwa makatibu wa jumuiya za CCM za vijana na wanawake mapema mwaka jana, lakini Husna akajikuta kwenye mgogoro mkubwa ambao vyombo vya habari viliripoti kuwa ulitokana na tofauti kati yake na Simba, ambaye ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Utawala Bora).
Mgogoro huo uliishia kwa UWT kutangaza kusimamishwa kwa Mwilima mwishoni mwa mwezi Februari ikieleza kuwa uamuzi huo ulifanywa na baraza kuu la umoja huo baada ya kuridhika kuwa kulikuwa na udhaifu katika utendaji wake, huku ikikanusha kuwepo kwa tofauti kati yake na Simba.
Lakini jana, taaaarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imeeleza mabadiliko yaliyofanywa na rais, yakiwemo ya kumrejesha Mwilima kwenye ukuu wa wilaya, yanalenga kuongeza ufanisi.
Akitangazwa kusimamishwa kwa Mwilima, makamu mwenyekiti wa UWT, Asha Bakari Makame alisema uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha Baraza la UWT kilichofanyika Dodoma Novemba 17 hadi 20 mwaka jana.
Alisema Baraza lilimsimamisha kwa kuwa msingi wa UWT ni maadili ya kiutendaji na ukweli, kwa kuwa jumuiya hiyo ndio mama na baba wa CCM.
Kwa habari zaidi ingia hapa.........
Tuesday, April 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment