Wednesday, April 14, 2010

Best Blogger Tips

Siasa na biashara kuzuiwa bungeni

WAKATI upepo wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi ukiwa haujatulia hasa baada ya Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa, kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete alisaini sheria iliyochomekwa vifungu ambavyo havikujadiliwa au kupitishwa na Bunge, Muswada wa Sheria nyingine mpya ya Kutenganisha siasa na Biashara unaweza kubisha hodi katika mkutano huu wa Bunge, Raia Mwema, imeelezwa.

Sheria hiyo ya kutenganisha siasa na biashara inatarajiwa kuathiri maudhui ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 iliyotungwa baada ya kuanguka kwa Azimio la Arusha, na hasa kipengele chake cha kutangaza mali kuendelea kufanywa siri na kuwa kosa la jinai kwa anayefichua siri hizo.

Tayari Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Sofia Simba katika mkutano uliopita wa Bunge aliweka bayana kuwa mkutano huu ulioanza wiki hii mjini Dodoma, utajadili na hata kupitisha Muswada wa Sheria ya Kutenganisha Siasa na Biashara ambao ni pacha na Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Muswada huo wa sheria hiyo ya siasa na biashara unakuja katika wakati ambao swali kubwa linalosubiriwa na wabunge wengi ni je, biashara gani ambayo kiongozi anazuiwa kuendelea kuifanya wakati wa utumishi wake kwa umma, ikizingatiwa kuwa viongozi wengi ambao ni pamoja na mawaziri ni wanahisa katika kampuni kubwa nchini. Hata hivyo, swali ambalo linajitokeza huku kukiwa na taarifa kuwa serikali tayari imekwishabainisha aina ya biashara husika.
Endelea kusoma habari hii............

 

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits