Saturday, October 23, 2010

Best Blogger Tips
CCM, Chadema walumbana mauaji Maswa

Via Mwananchi

WAKATI Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akikitupia makombora Chadema kwamba kinahusika na mauaji yaliyotokea katika mkutano wa kampeni, Jimbo la Maswa Magharibi, Chadema kimesema chama hicho tawala ndicho kitabeba lawama kwa kuvamia mkutano wao.

Mgombea urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akiwa katika mkutano wa kampeni mkoani Tanga jana alisema maafa hayo yamesababishwa na CCM kwa kuwafundisha na kuhamasisha vijana wake kuvamia mikutano ya vyama vingine vya siasa.

Alisema muda sasa umefika kwa serikali kuonyesha kwa vitendo kwa kuwashughulikia wote wanaohusika kuvunja amani ya nchi bila kujali itikadi zao za kisiasa kwa kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria kwani kuvunja amani ni kosa la jinai.

Dk Slaa alitaja baadhi ya maeneo nchini ambako umwagaji damu umetokea mpaka sasa kutokana na sababu za kisiasa kuwa ni pamoja na Hai, Kagera, Tarime, Mwanza, Mpanda na Maswa na kuhoji sereikali inasubiri watu wangapi wajeruhiwe au kupoteza maisha ndipo ichukue hatua.

"Tangu nimeanza mikutano yangu inayokaribia zaidi ya mikutano 460 hadi sasa nimesisitiza amani na kueleza wazi kuwa siko tayari kwenda Ikulu kwa wananchi wangu kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa na wengine kupata ulemavu au kupoteza maisha. Nimekuwa nikimuomba Kikwete ajitokeze hadharani kukemea vitendo vya vijana wa CCM kuanzisha vurugu na avunje na kupiga marufuku makambi ya vijana hao lakini hata siku moja hajafanya hivyo ikiwa ni dalili ya kuunga mkono vitendo hivyo," alisema Dk Slaa.

Wakati Slaa akisema hayo, kwa upande wa CCM Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusufu Makamba amesema kuna ushahidi wa kimazingira unaoonyesha kuwa mgombea wa Chadema jimbo la Maswa Magharibi, John Shibuda amehusika katika mauaji yaliyotokea juzi wilayani humo na kusababisha kifo cha mtu mmoja

Makamba ambaye alikuwa wilayani Maswa jana ambapo mbali na kufanya shughuli za chama pia alikwenda kutoa salamu za rambirambi kwa ndugu wa merehemu Steven Kwilasa, ambaye alikuwa dereva wa mgombea ubunge wa jimbo la Maswa Magharibi kupitia CCM, Robert Kisena.
Endelea kusoma habari hii..............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits