Dokta Remmy afariki dunia
Mwanamuziki maarufu nchini Tanzania Ramadhani Mtoro Ongala, amefariki dunia.
Dr Remmy kama alivyojulikana amefariki baada ya kuugua kwa takriban wiki mbili ambapo alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo, moyo, kisukari na shinikizo la damu.
Dr Remmy kama alivyojulikana au sura mbaya kama alivyopenda kujulikana wakati mwingine atakumbukwa sana kutokana na umahiri wake katika kutunga na kuimba nyimbo zilizozungumzia juu ya maisha ya kila siku,na pia mapenzi.
Wimbo siku ya kufa ni moja ya nyimbo zilizompatia umaarufu mkubwa Dr Remmy enzi za uhai wake, wakati huo akiimbia Bendi ya Orchestra Makassy iliyoasisiwa ma mjomba wake Kitenzogu Makassy almaaruf Mzee Makassy.
Umaarufu wa Dr Remmy ulifikia hadi makazi yake kuitwa Sinza kwa Remmy. Mbali na wimbo siku ya Kufa Wimbo mwingine kati ya nyingi alizoimba Dr Remmy kuonyesha alivyokuwa na hisia kali ya kifo ni Wimbo ujulikanao kama Kifo.
Mwanazmuziki Dr Remmy alizaliwa mnamo mwaka 1947,katika mji Kisangani lakini na kukulia mjini Bukavu huko Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo enzi hizo ikijulikana kama Zaire kabla ya kuhamia nchini Tanzania mwaka 1977, ambapo alijiunga na Bendi ya Mjomba wake Mzee Makassy na baadaye alijiunga na Super Matimila na kisha kurejea tena kwa mjomba wake Mzee Makassy kabla ya kuachana na Muziki wa kidunia na kuanza kuimba muziki wa kiroho hadi mauti yalipomkuta usiku wa kuamkia Jumatatu.
Marehemu ameacha mjane na watoto watano.
Monday, December 13, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment