Thursday, May 19, 2011

Best Blogger Tips
Mkuu wa IFM Ajiuzuru kutoka wadhifa wake

Via BBC

Mkuu wa shirika la fedha duniani, Dominique Strauss Kahn amejiuzulu.

Taarifa hiyo ya kujiuzulu kwa Strauss Kahn imechapishwa katika wavuti wa shirika hilo.
Anasema amejiuzulu ili atumie muda uliobakia kujitea katika kesi inayomkabili ya kujaribu kumbaka mwanamke mmoja mjini New York.

Strauss Kahn ametuma taarifa yake kwa bodi ya shirika hilo. Amesema kuwa anakanusha mashtaka yote dhidi yake na amesikitishwa na kisa hicho kilichomkabili.

Shirika hilo limesema kuwa litatangaza hivi karibuni utaratibu wa kumteua mkurugenzi mpya. Kwa sasa John Lipsky ataendelea kuwa kaimu Mkurugenzi mkuu wa IMF.

Awali waziri wa fedha wa Marekani amesema kuwa mkuu wa shirika la fedha duniani (IMF), Dominique Strauss-Kahn, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli, hawezi tena kuendesha shughuli za shirika hilo.

Timothy Geithner ametoa wito kwa IMF kumteua rasmi kaimu mkuu wa shirika hilo.
Bwana Strauss-Kahn anazuiliwa katika jela moja mjini New York baada ya kukamatwa hapo jumamosi kwa kosa la kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli moja.

Strauss-kahn ambaye amezuiliwa katika gereza la wafungwa sugu la Rikers Islands mjini New York yupo chini ya ulinzi mkali kuchunga asijiue. Hii ni baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Wakili wa mwanamke huyo kutoka Guinea, Afrika Magharibi, anayemtuhumu Strauss-Kahn, amesema mteja wake amepata mshutuko ambao sio wakawaida.

Wakili huyo ameongeza kuwa kwa sasa yupo mafichoni na kwamba anajihisi ''Yuko pekee duniani''.

Strauss-Kahn, mwenye umri wa miaka 62, anakabiliwa na mashtaka saba dhidi yake na iwapo atapatikana na hatia, atahukumiwa kifungo cha hadi miaka 25 jela.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits