Waziri amfungia umeme mchungaji Mwasapila
Via Mwananchi
WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, amebadili sura ya makazi ya Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania(KKKT), Ambikile Mwasapila kwa kumfungia umeme unaotumia mionzi ya jua.
Umeme huo, ulifungwa jana na kampuni ya Ensol(t) Limited na hivyo kufanya makazi ya mchungaji huyo kuwa na umeme wa uhakika na hivyo kuboresha tiba yake kwa kuchemsha.
Kwa mujibu wa mafundi wa Kampuni ya Ensol, gharama za kufungwa kwa umeme huo ni zaidi ya Sh4 milioni na fedha hizo zimetolewa na Lukuvi.
Waziri Lukuvi ambaye ni mmoja wa mawaziri wa kwanza kufika Samunge na kupata kikombe cha tiba, pia ndiye
alisaidia kupunguza msongamano wa magari baada ya kuanzisha utaratibu wa kuingia Samunge kwa vibali.
Akizungumza na Mwananchi jana kwa niaba ya mchungaji Mwasapila, msaidizi wake, Fredrick Nsajile alisema, mchungaji ameshukuru sana kwa msaada huo wa Lukuvi.
"Mchungaji Mwasapila anashukuru kwa msaada huu mkubwa ambao utasaidia kuwapo kwa umeme wa ukakika na kwa wakati wote na hivyo kurahisisha kazi ya kuchesha dawa,"alisema Nsajile.
Nsajile pia alitoa shukrani kwa msaada wa waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Dk Terezya Huvisa na serikali Mkoa wa Arusha, wa kumalizika kuezeka mabati nyumba mpya ya mchungaji Mwasapila.
"Tunatoa shukrani kwa wote wanaoendelea kutusaidia ili kuboreshwa huduma hapa Samunge, wapo wengi na mchungaji anawaombea maisha mema,"alisema Nsajile.
Monday, May 9, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment