Mapigano Libya |
Kumekuwepo na mapambano ya siku kadhaa kati ya
makundi yanayokinzana katika mji wa mwambao wa Zawiya nchini Libya
ambapo takriban watu 7 waliuawa.
Hatahivyo serikali ya mpito imesema kwamba mapigano hayo yalisuluhishwa.
Wachambuzi wanasema mapigano hayo yanazusha masuala kadhaa kuhusu hali ya utulivu baada ya kuondoka kwa Gaddaffi nchini Libya.
Libya bado inakabiliwa na changamoto za kuenea silaha na vikundi vya watu wenye silaha baada ya uasi uliosababisha kuporomoka kwa utawala wa Kanali l Muammar Gaddafi.
Kiongozi wa utawala wa mpito Mustafa Abdul-Jalil alisema baraza la taifa la mpito limewakutanisha wazee kutoka maeneo yanayogombaniwa ya Zawiya na maeneo ya karibu ya makabila ya Warshefana - na kwamba mzozo huo umesuluhishwa mwishoni mwa wiki.
Hatahivyo baadhi ya watu wamearifu kuwa mapigano bado yalikuwa yanaendelea wakati akiongea.
Taarifa zaeleza kuwa mapigano yalianza pale wapiganaji kutoka Warshefana walipoweka kizuizi cha barabarani katika njia panda karibu na Zawiya, na kuwatambia wapiganaji kutoka mjini humo.
Wapiganaji kutoka Zawiya waliwashutumu wale kutoka Warshefana kuwa na ufungamano na utawala wa zamani.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment