Saad Gaddafi |
Serikali ya Mexico imesema imezuia njama iliyokuwa
ifanywe na kundi la wahalifu la kumpenyeza kwa magendo mmoja wa watoto
wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi nchini Mexico.
Msemaji wa serikali ya Mexico alisema Saadi Gaddafi na baadhi ya wanafamilia wake walizuiwa kutokana na matokeo ya ripoti za kijasusi.
Watu wengi wamekamatwa kutokana na tukio hilo.
Maafisa wa Mexico wamsema jaribio hilo- lililoibuliwa Septemba 6- lilihusisha majina na nyaraka za uongo.
Nyumba salama
Waziri wa mambo ya ndani Alejandro Poire alisema mpango huo unahusisha mtandao wa uhalifu " mkubwa wa kimataifa", lakini ikagundulika mwezi Septemba kabla ya mpango huo kukamilika.Mtandao huo ulihusisha watu kutoka nchi mbalimbali, ikiwemo Mexico, Denmark na Canada, Bw Poire aliuambia mkutano wa waandishi wa habari huko Mexico.
Alisema, walikuwa wakinunua nyumba zenye salama na kufungua akaunti za benki.
Tarehe 14 Septemba- siku nane baada ya njama hiyo kugundulika- Niger ilisema Saadi Gaddafi, mwenye umri wa miaka 38, aliwasili mjini Niamey.
Iliripotiwa kuwa alisafirishwa kwa ndege ya kijeshi kutoka mji wa Agadez kaskazini mwa nchi hiyo.
Septemba 29, Shirika la polisi la kimataifa, Interpol lilitoa " hati ya kukamatwa" kwa Saadi Gaddafi, wakitaka nchi wanachama imkatae iwapo atatokea kwenye nchi zao.
Wakala wa polisi wa kimataifa wamesema anatakiwa kwa madai ya kutoa vitisho kwa kutumia silaha alipokuwa mkuu wa shirikisho la mpira la Libya.
Saadi Gaddafi, ambaye alikuwa akicheza soka katika ligi kuu ya Italia Serie A, pia amewekewa vikwazo vya kusafiri na mali zake kutiwa tanji chini ya azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa lililopitishwa mapema mwaka huu.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment