Mr II ajitosa ubunge Mbeya Mjini
SIKU moja baada ya msanii nguli, mwasisi wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo fleva’ hapa nchini, Joseph Mbilinyi ‘Mr II Sugu’ kushikiliwa na polisi kwa mahojiano, jana alitangaza nia ya kuwania ubunge katika Jimbo la Mbeya Mjini sambamba na kufafanua tuhuma zilizomfanya ashikiliwe na chombo hicho cha dola.
Kwa mujibu wa taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jijini Dar es Salaam jana, Mbilinyi ambaye anajulikana zaidi katika anga la muziki kama Mr II ama Sugu, anatangaza rasmi kugombea ubunge katika Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ().
“Kwa muda mrefu katika maisha yangu ya kimuziki, pamoja na kuimba nyimbo za kuburudisha nimekuwa zaidi mstari wa mbele kuimba nyimbo za kutetea haki za makundi mbalimbali katika jamii na taifa kwa ujumla. Wakati umefika sasa wa kuhamisha jukwaa la mapambano ya kudai haki, kutoka jukwaa la muziki mpaka jukwaa la siasa, kwa dhamira ile ile ya kutumia kipaji changu alichonijalia Mwenyezi Mungu, kuimba na kuhutubia kwa ajili kuleta mabadiliko ya kweli katika taifa letu,” alisema Mr II na kuongeza:
“Nyimbo zangu zimekuwa zikibeba sauti ya watu wasio na sauti, ili zisikike kwa watawala, lakini hata hivyo kwa kipindi chote ambacho nimekuwa nikifanya harakati hizi watunga sheria na wafanya maamuzi ya kisera chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameshindwa kuongoza vizuri taifa kuweza kufanya mabadiliko ya kweli, yenye kuhakikisha Watanzania wananufaika na vipaji vyao ambavyo Mwenyezi Mungu amewajalia na taifa linanufaika na rasilimali na maliasili ambazo tumejaliwa kuwa nazo.”
Alisema anatangaza nia ya kugombea ubunge ili kuchangia katika kuongeza nguvu ya chama mbadala katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, awe ni sehemu ya sauti mbadala katika kutunga sheria, kuwawakilisha wananchi, kuandaa sera na kuiwajibisha serikali kuweza kutekeleza yale ambayo yeye na wanaharakati wenzake katika sanaa wamekuwa wakiyapigia kelele muda mrefu kupitia muziki na maisha yao.
Endelea kusoma habari hii.................