Waifunga Celtics 83-79
Derek Fisher, akiwa na mkewe Candace, wakisheherekea ubingwa baada ya kuifunga Boston, Celtics 83-79, huko Staples Center, Los Angeles.
Mchezo ulikuwa mkali sana, huku timu zote zikiwa imara katika ulinzi, hali iliyopelekea uhaba wa magoli, kwani ushindi huo wa 83-79 unadhihirisha ni jinsi gani timu zote mbili zilivyokuwa imara katika ulinzi. Ron Artest aliamsha uhai wa Lakers baada ya kurusha mpira na kupata point tatu muhimu katika dakika za mwisho za mchezo huo.
Kobe Bryant ndiye MVP wa mwaka huu, akiwa na wastani wa point 28.6, rebounds 8 na 3.9 assists katika mlolongo wa michuano hiyo. Hii inakuwa ni mara yake ya pili kuchukua taji hilo, mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka jana. Pia hii inakuwa ni mara ya 5 kwa Kobe Bryant kuchukua ubingwa huu, mara zote akiwa na Lakers. Bado hajafikia record ya mkongwe Michael Jordan, ambaye alichukua ubingwa huo mara 6, na alikuwa MVP mara 6.
Phil Jackson, anakuwa kocha wa kwanza katika historia ya mchezo huo, kwa kuchukua ubingwa huo mara 11.
Rais wa Marekani, Barack Obama, ambae ni mpenzi mkubwa wa mchezo huo, alitabiri Lakers kuwa mabingwa mwaka huu katika mahojiano yake na TNT.
Celtics, bado wana sifa nzuri katika historia ya mashindano hayo, kwani wameshachukua ubingwa huo mara 17, ukilinganisha na Lakers ambao baada ya kuchukua ubingwa mwaka huu, inakuwa ni mara ya 16, ikiwa nyuma ya Celtics mara 1.
No comments:
Post a Comment