Marekani yazuia mali za mfanyabiashara Msumbiji
Wizara ya fedha ya Marekani imezuia mali za mtu anayeshukiwa kuwa mfanya biashara za madawa ya kulevya kutoka Msumbiji baada ya kutajwa kuwa msafirishaji mkuu wa madawa ya kulevya na rais wa Marekani Barack Obama.
Wizara ya fedha ya Marekani imezuia mali za mtu anyeshukiwa kuwa mfanya biashara za madawa ya kulevya kutoka Msumbiji baada ya kutajwa kuwa msafirishaji mkuu wa madawa ya kulevya na rais wa Marekani Barack Obama.
Katika taarifa Jumanne Afisa wa juu wa wizara ya fedha Marekani amesema Mohamed Bashir Suleiman ni muuzaji mkuu wa madawa ya kulevya na kwamba mtandao wake ulichangia kwenye biashara inayokua ya madawa ya kulevya na wizi wa fedha katika eneo kubwa la Afrika.
Biashara tatu za Suleiman zilitajwa kuwa sehemu ya mtandao wake wa usafirishaji Hii ina maana kwamba mali zake zote zilzopo kwenye ardhi ya Marekani hivi sasa zimezuiwa na raia wa Marekani hawaruhusiwi kufanya biashara na makampuni yake matatu.
Source: VOA
Saturday, June 5, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment