Saturday, February 26, 2011

Best Blogger Tips
Hasheem Thabeet


Hasheem Thabeet, alipotakiwa na gazeti moja la Memphis  kuelezea  jinsi ilivyokuwa kwake katika mwaka wake wa kwanza kama mchezaji wa NBA, alitoa jibu la kuvutia , “ Nilikuwa kama nyati aliyeona mwanga wa tochi.”

 Thabeet  akiwa ameshacheza misimu miwili ya NBA, hajaonyesha mchezo wa kuvutia  kama alivyosema kwenye jibu lake.

Inawezeka  ikawa hivyo kwa mtu ambaye bado anajifunza kucheza mchezo huo. Thabeet amekuwa akicheza soka  tangu akiwa mdogo kwenye nchi yake ya Tanzania yenye jumla ya watu takribani milioni 41 iliyopo mashariki ya bara la Afrika.

Thabeet ambaye ametimiza miaka 24 wiki iliyopita, hakuwa akicheza mpira wa kikapu mpaka alipokuwa na miaka 15, muda mfupi baada ya baba yake kufariki. Akiwa mtoto wa kiume kutoka katika moja ya nchi masikini duniani, kuja kwake Marekani ilikuwa ni kwa ajili ya kuisaidia familia yake iwe na maisha bora.

Alituma maombi kwenye vyuo mbalimbali, kwa matumaini kwamba angepata ufadhili wa masomo. Mmoja kati ya walimu wa michezo alimuona katika mashindano, na akaishia katika shule za sekondari za Majimbo ya Califonia na Mississipi kabla ya kwenda katika mji wa Houston kwenye jimbo la Texas, ambapo aliingia katika shule ya sekondari ya Cypress ( Cypress Christian High School).

Thabeet alipofika  shuleni  kwake Cypress Christian mwaka 2005, ilimuwiya vigumu sana katika kujifunza kucheza mpira wa kikapu, licha ya urefu wake wa futi 7-3, alipata shida katika mchezo huo.

Kwa ujumla ilieleweka kwamba Thabeet asingeweza kucheza mchezo huo katika daraja la kwanza.

Hivyo ndivyo kocha msaidizi wa chuo cha Connecticut Andre LaFleur  alivyowaza baada ya kumuona Hasheem kwa mara ya kwanza. Aliyomuona mara ya pili, Thabeet alikuwa amebadilika sana, akionyesha maendeleo mazuri katika mchezo huo, na alipomuona kwa mara ya tatu alikuwa akicheza vizuri zaidi.

Lafleur alikuwa Houston wakati thabeet alipokuwa akipambana na timu ya Blake Griffin katika mashindano ya Kingwood. Lafleur akamjulisha kocha mkuu wa UConn Jim Calhoun kwamba Thabeet anaweza kuwa  namba moja kati ya wachezaji watakaochaguliwa kujiunga na NBA hapo baadaye.

Baadaye mwaka 2009 katika kuwachagua wachezji bora wa kujiunga  na NBA, Hasheem Thabeet alikuwa ni chaguo namba 2 nyuma ya Blake Griffin aliyekuwa namba 1.

Thabeet anaendelea

“Alikuwa anacheza mpira wa kikapu kama vile anacheza soka” Lafleur anasema, “Lakini kitu cha muhimu ni kwamba kila wakati ukimuona alikuwa anakuwa mzuri mzaidi”. “Unafikilia kwamba: kila kitu anachoona hapa ni mara yake ya kwanza, maisha yake aliyokulia ni tofauti na ya wachezaji wa hapo ambao ndoto yao  ni kucheza NBA. Kufanikiwa kwake kufika chuoni kumemfanya ajulikane nyumbani. Ikabidi ajifunze malengo yake mapya, alikuwa hajui kitu.

Sasa hivi ni karibu miaka miwili tangu Hasheem aanze kazi yake katika NBA, watu wengi wanamuona kama vile ambavyo Lafleaur alivyomuona kwa mara ya kwanza, mtu mrefu aliye legelege na asiyeweza kuchangia chochote katika mchezo huo.

Timu ya Rockets, ambayo imewapeleka wachezaji wake Shane Battier na Ish Smith huko Memphis kwa ajili ya kumchukua Thabeet, wana imani kuwa  mchezaji huyo mrefu na mwenye umbo kubwa katika NBA atabadilika na kuwa mzuri zaidi kama ilivyokuwa wakati akianza kujifunza mchezo huo.

“NI wazi kuwa tunahitaji mchezaji wa kati katika timu yetu”, anasema Daryl Morey ambaye ni Meneja Mkuu wa Rockets. “ Hasheem Thabeet ana uwezo wa kuendeleza kipaji chake katika sehemu ya ulinzi na pia kuwa mchezaji mzuri wa kati. Sasa hivi bado hajafikia hapo, kama angekuwa katika hali hiyo sisi tusingekuwa na uwezo wa kumpata.”

Ujasiri na kujiamini

Kujiamini na ujasiri ndivyo vitu vinavyomsaidia, lakini Lafleaur anasema Thabeet ni mtu ambaye anajivunia mafanikio yake. Hali ya kuwa anasakamwa mara kwa mara inamuumiza, lakini hali ya kumchukulia kwamba ameshindwa katika mchezo huo inamuumiza zaidi.

“ Naelewa kwamba kwenye idara ya ulinzi ni mzuri ingawa naweza kufanya vizuri zaidi,” Thabeet alimuandikia barua pepe mwandishi wa Rockets Jonathan Feigen siku ya ijumaa. “ Jambo moja ambalo nimejifunza  ni kwamba wakati wowote unaweza kuwa bora, niko hapa kufanya kazi kwa bidii, kujifunza mfumo wa timu hii ya Rockets na nina furaha kubwa kwa kupata nafasi hii.”

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits