Bomani atoa waraka mzito CCM, Serikali
MWANASHERIA Mkuu mstaafu wa Serikali Jaji Mark Bomani, ameandika waraka mzito kwenda CCM na serikali yake, ambao pamoja na mengine unaelezea mfumo wa sasa wa uchaguzi kuwa ni kichochea cha ufisadi katika kupata viongozi wa dola.
Waraka huo mzito wa Jaji Bomani ambao unazungumzia nchi ilikotoka, iliko na inakoelekea, umekuja kipindi ambacho joto la uchaguzi mkuu wa Oktoba likiwa juu.
Ndani ya waraka huo wenye kichwa cha habari: "Mapendekezo ya Mark Bomani, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu," ambao gazeti hili limefanikiwa kupata nakala yake jijini Dar es Salaam jana, Jaji Bomani amechambua mifumo miwili mikubwa ya uchaguzi ambayo ni nguzo ya demokrasi.
Katika uchambuzi huo, Jaji Bomani, alisema Tanzania kama makoloni mengine yaliyotawaliwa na Uingereza, imerithi mfumo wa uchaguzi wa majimbo wa mkoloni huyo, lakini una athari kubwa ikiwemo matumizi ya rushwa katika uchaguzi na gharama za kuendesha uchaguzi katika majimbo.
Jaji Bomani alifafanua katika waraka huo kwamba, pamoja na Tanzania kurithi mfumo huo unaotumiwa na nchi ya Jumuiya za Madola (Commonwealth Countries), hivi karibuni ilijiongezea aina nyingine ya uwakilishi kama vile viti maalumu.
Endelea kusoma habari hii.......
No comments:
Post a Comment