Ghorofa Dar hatarini kuanguka, lipo Kariakoo
WAKAZI na watu wanaofanya shughuli zao maeneo ya Kariakoo jana walipata kitu kingine cha kushangaa lakini kinachotishia usalama wao; jengo la ghorofa nane lililo na ufa na ambalo wakati wowote linaweza kuanguka eneo hilo la kibiashara lenye watu wengi.
Watu wengi walikuwa wamesimama chini ya jengo hilo lililo kwenye makutano ya Mtaa wa Swahili na Mafia baada ya kupata habari kuwa liko hatarini kuanguka kiasi cha serikali ya mkoa kusimamisha ujenzi wake ikiwa ni miaka michache tangu iundwe kamati iliyopewa jukumu la kuchunguza majengo yaliyojengwa chini ya viwango, lakini ripoti yake ikatiwa kapuni.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa serikari imesimamisha ujenzi wa jengo hilo kwa sababu linaweza kusababisha maafa makubwa baada ya kupata ufa mkubwa katika ghorofa ya kwanza.
No comments:
Post a Comment