Wednesday, March 24, 2010

Best Blogger Tips
WIZI KWENYE MABENKI: Watu kumi wanaswa kwa wizi wa kimafia

Via Mwananchi

WAKATI habari za wizi wa kimafia wa Sh300 bilioni zikiwa zimeistua serikali, watu kumi wamekamatwa kwa tuhuma za wizi mwingine wa aina hiyo uliohusisha Sh360 milioni za benki moja nchini.

Kukamatwa kwa watu hao kumetokea siku moja baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti wizi huo mkubwa unaotumia teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta ambao ulifanyika kwenye benki nne kubwa nchini, taarifa iliyofanya Mamlaka ya Mapato (TRA) kuanza uchunguzi.

Mbali na taarifa za kukamatwa kwa watu hao, vyombo vya habari pia vimeripoti kukamatwa kwa  mfanyabiashara mmoja aliyekuwa akifanya jaribio la kuiba kimafia Sh221 milioni kutoka benki ya NBC.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ambazo zilithibitishwa na msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Abdallah Msika zinasema watu hao walikamatwa kati ya Februari na Machi, katika msako wa jeshi hilo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga na Zanzibar.

Kukamatwa kwa watu hao kumetokea wakati benki zimekuwa zikihaha kubadili na kuboresha mifumo yake ya kuchukua na kutoa fedha kwa njia ya elektroniki kwa lengo la kukabiliana na uhalifu uliokithiri unaofanywa na watu walio ndani na nje ya nchi.
Endelea kusoma habari hii.......

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits