Ndesamburo-Hata mchange bilioni moja nitawashinda
via Mwananchi
MBUNGE wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema) amejibu mapigo akisema hata kama CCM itaendesha harambee na kupata Sh1 bilioni bado haitaweza kumng’oa kwenye jimbo hilo .
Kauli ya Ndesamburo inatokana na taarifa zilizowakariri viongozi wa CCM mkoani hapa wakisema kuwa Mei mwaka huu wataendesha harambee kubwa ili zipatikane Sh500 milioni kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu.
Sehemu kubwa ya fedha za harambee hiyo ambayo mwenyekiti wa CCM,Jakaya Kikwete anatarajiwa kuiendesha, zimepangwa kuelekezwa kwenye Jimbo la Moshi Mjini ambalo Ndesamburo amekuwa akilishikilia tangu mwaka 2000.
Lakini Ndesamburo aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa jitihada hizo hazitaweza kumng'oa hata kama watachangisha fedha zaidi ya hizo walizopanga.
“Nawaambia hao CCM hata wakikusanya Sh1 bilioni na viongozi wao wote wakahamia Moshi, bado hawataning’oa; nawaomba wananchi wajiandae kula fedha hizo kwa sababu ni jasho lao,†alisema Ndesamburo.
Ndesamburo alimuomba Rais Kikwete kutoingia katika mtego huo hasa ikizingatiwa ndio kwanza amesaini Sheria ya Udhibiti wa Fedha katika Uchaguzi ambayo pia inalenga kudhibiti ushawishi wa kutumia fedha kwa wananchi wakati wa uchaguzi.
Naye mbunge wa viti maalumu (Chadema), Lucy Owenya alionyesha kushangazwa na hatua ya CCM kutafuta Sh500 milioni za kampeni wakati hali ya huduma katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi ni mbaya.
Endelea kusoma habari hii..........
Sunday, March 28, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment