Saturday, March 5, 2011

Best Blogger Tips
Wapinzani wakabiliana na majeshi ya Libya

Wapinzani nchini Libya wamezuia jaribio la majeshi ya serikali ya kuuchukua tena mji wa Zawiya, kilomita 50 magharibi mwa mji wa Tripoli.

Kufuatia mapigano makali siku ya Jumamosi asubuhi, majeshi ya serikali yalilazimishwa kusogea nje ya mji, ingawa baadhi ya taarifa zinasema wamejipanga upya na huenda wakawa wanapanga mashambulizi mapya.
Idadi ya vifo haiko wazi.

Wakti huohuo, wapinzani wanaompinga Kanali Muammar Gaddafi wamechukua udhibiti wa mji wa bandari wa Lanuf, mashariki mwa Tripoli.

Waangalizi wanasema kwa ujumla ni vigumu kujua nani anadhibiti wapi, wakati mvutano wa kuitawala Libya ukiendelea.

Mjini Tripoli, kuna hali ya kujiamini miongoni mwa wanaoutii utawala, huku udhibiti ukionekana kuongezeka mjini Tripoli na maeneo mengine ya kati, kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyepo huko.

Lakini katika maeneo mengine, waandishi wa habari wanasema waandamanaji wana ari kubwa ya kuuondoa utawala wa Kanali Gaddafi.

Taarifa kutoka Zawiya zinasema mji huo umeshambuliwa kutoka upande wa mashariki na magharibi kutoka kwa wanajeshi wa serikali wenye silaha nzito.
Source: BBC

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits