- Waliokunywa wapimwa baada ya siku 90
- Matokeo yaonyesha bado wana virusi
- Wailaumu Serikali ‘kubariki’ kikombe cha Babu
Kaaya na wenzake walikuwa na imani kubwa kuwa huenda tiba hiyo ikawa ndiyo mwisho wa mateso na mahangaiko ya muda mrefu yanayotokana na kusumbuliwa na virusi vya ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa dunia haijapata tiba yake.
Watu hao walikuwa wamesafirishwa kwa msaada wa shirika la (EACNASO) ambalo pia ni muungano wa mtandao wa mashirika yanayojishughulisha na ugonjwa huo kwa nchi za Afrika ya Mashariki lenye makao yake mjini Arusha.
Imani ya waathirika hao ilijengwa juu ya msingi kuwa dawa ya kikombe cha Babu kwa wakati huo ilikuwa gumzo kubwa nchini na viongozi mbalimbali wa serikali kutoka kada mbalimbali, kama mawaziri wa serikali, majaji wa Mahakama Kuu, wenyeviti wa vyama vya siasa, wakuu wa mjeshi na wananchi, walipigana vikumbo katika kijiji hicho kupata uponyaji wa maradhi yanayowasumbua kupitia tiba hiyo.
Baada ya safari ngumu ya siku moja na nusu kutokana na ubovu wa barabara, Kaaya na wenzake walifika Samunge na kupata tiba ya kikombe cha Babu; huku wakipewa siku 90 kama muda ambao virusi vitakuwa vimetoweka katika miili yao.
Aidha, majibu ya vipimo vya watu hao pia vilikuwa vinasubiriwa kwa hamu na makundi mbalimbali katika jamii kutokana na watu hao kujitangaza kuishi na virusi hivyo na kuwa tayari kuweka hadharani majibu ya vipimo vya hali zao.
Lakini miezi minne sasa tangu muda uliotolewa “kisayansi” na Mchungaji Masapila kuwa virusi vitakuwa vimeisha miilini mwao, Kaaya na wenzake wote waliotumia tiba hiyo wamevunjika moyo baada ya kupimwa upya na kuonekana kuwa bado wana virusi vya ugonjwa huo hatari.
Endelea kusoma habari hii......................
No comments:
Post a Comment