WIZARA ya Nishati na Madini imesema zaidi ya Sh1 milioni zinahitajika kwa ajili ya kubadilisha mfumo wa gari moja linalotumia mafuta ya petroli kutumia gesi asilia, Bunge lilielezwa jana.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima aliliambia Bunge hayo jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Muheza (CCM) Herbert Mtangi aliyetaka kujua Serikali inasema nini kuhusu utekelezaji wa mradi wa gesi kwa magari hapa nchini.
Waziri Malima alisema mpaka sasa mifumo ya magari 36 yamebadilishwa ili kuweza kutumia gesi asilia ambapo alisema kasi ya ubadilishwaji wa mifumo ya magari ni ndogo kutokana na gharama za ubadilishaji kuwa kubwa.
Aidha Malima alisema kasi ndogo ya za elimu juu ya suala hilo imesababisha ufahamu mdogo wa manufaa ya matumizi ya gesi kwenye magari ikilinganishwa na matumizi ya petroli.Alifafanua kuwa mkakati wa Serikali wa awali mwaka 2008, ulikuwa ni kuanzisha vituo vya mfano na masoko ambapo walianzisha kituo cha kujaza gesi kwenye magari ubungo.
Alisema kituo hicho kina uwezo wa kujaza magari 200 kwa siku.
Alisema Serikali kupitia TPDC kwa kushirikiana na Pan African Energy walianza mchakato wa mradi wa kutumia gesi asilia kwenye magari, viwandani pamoja na majumbani kwa lengo la kupanua manufaa ya kiuchumi na kijamii.
Source: Mwananchi
Monday, August 15, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment