MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amewatolea uvivu
wagombea wa nafasi mbalimbali ambao majina yao yamekatwa, akisema
wanaotaka kukihama chama hicho kwa sababu wametoswa, waondoke haraka.
Licha
ya kuwatakia safari njema, Rais Kikwete aliwatupia lawama baadhi ya
wanaCCM ambao wameripotiwa kuendesha malumbano na kugeuza uchaguzi huo
kama uwanja wa vita.
Akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (Nec)
jana, Rais Kikwete alisema kumekuwapo na taarifa mbalimbali ambazo
zimemfikia pia kwamba baadhi ya wanachama wanatishia kukihama chama
hicho kama majina yao yatakatwa.
“Wako wenye ndimi mbili ambao
wanasema kuwa wasipoteuliwa wanaweza kuondoka. Ah! Mimi nasema
watangulie huko maana inaonyesha kuwa walishaandaa maeneo ya kwenda,”
alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wajumbe wa Nec.
Alisema
CCM kinayo taarifa kuhusu watu kugombana na hata kutoleana silaha,
jambo alilosema linashangaza, huku akihoji kuna nini katika uongozi tena
Nec?
“Uchaguzi usigeuzwe uwanja wa fujo. Wengine wanatoleana
silaha kama majembe, ngumi na silaha nyingine, hivi wanagombana nini
huko? Uchaguzi usigeuzwe kuwa ni uwanja wa vita.” alisema.
Hivi
karibuni, baadhi ya makada wa chama hicho wamekuwa wakitoa kauli
mbalimbali za kukitishia chama hicho akiwemo Mbunge wa Musoma Vijijini,
Nimrod Mkono ambaye alikaririwa akisema kama jina lake halitapitishwa,
patachimbika.
Mbunge huyo alisema hayo siku chache baada ya jina
lake kutupwa na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi iliyokuwa
ikipitia na kuteua wagombea watatu kwa ajili ya kuwania nafasi ya
mwenyekiti wa jumuiya hiyo.
"Hapatatosha CCM," alisema Mkono alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kutoswa kwake katika mchujo wa awamu hiyo ya awali.
Ingawa
Rais Kikwete hakutaja majina, Mbunge wa Nzega Dk Khamis Kigwangallah na
Hussein Bashe nao waliripotiwa kutoleana maneno makali hata kuonyeshana
bastola, huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na
Mbunge wa Kahama, James Lembeli wakiendesha malumbano kwa muda mrefu.
Inadaiwa
kuwa majina hayo yote na ya vigogo wengine yamekatwa na jana baadhi yao
walikuwa wanadai kuwa CCM kinataka kuzalisha upinzani ambao
utakisababishia kushindwa katika safari yake kisiasa hasa katika mfumo
huu wa vyama vingi.
Licha ya makaripio hayo, Rais Kikwete
alibainisha kuwa CCM kinasemwa na watu kuwa kinakithiri rushwa katika
chaguzi zake hivyo akawataka wagombea kubadilika kabla ya kukamatwa na
Takukuru.
“Zipo taarifa ingawa hatujazithibitisha kwamba wapo baadhi ya wagombea wanamwaga fedha sijawahi kuona…
Takukuru
wapo wanaendelea na kazi. Chama chetu kinasemwa tujipe fursa ya
kubadilika, tusisubiri kukamatwa na kuanza kuilaumu PCCB.”
Kuhusu
uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali, Rais Kikwete alisema katika
uchaguzi huo, wamejitokeza watu wengi tena vijana wasomi na kwamba
Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati Kuu, zimewapandisha na kuwakata
waliotumikia chama muda mrefu.
“Kama hukuteuliwa kuna mawili, ama
nafasi zimejaa au hufai una upungufu kidogo na huo ni utaratibu wa
chama siyo kuoneana,” alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa.
Alisema
katika uteuzi huo vijana watapewa nafasi zaidi kutokana na ukweli kuwa,
chama bila ya vijana hakiwezi kuwa imara kwa sababu ndiyo nguvu ya
ushindi.
“Hao watakaoachwa watambue kuwa tunafanya hivyo kwa
ajili ya kutengeneza timu ya ushindi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa Bara na Visiwani, hivyo kuachwa jina
lako isiwe nongwa,” alisema na kuongeza:
“Lazima tukipe chama chetu watu wa kushinda… Lazima tutambue sasa tunaunda timu ya ushindi wa chama siyo ushindi wa mtu.”
Hata
hivyo, Rais Kikwete alitoa angalizo kuwa anajua kikao cha Halmashauri
Kuu kingekuwa na mjadala mzito, lakini lazima wakipe chama watu wa
kushinda.
Majina manne
Kamati Kuu ya CCM, inadaiwa
kupendekeza majina ya wagombea wanne kwenye jumuiya zake, tofauti na
kanuni ya chama hicho ya nafasi moja kuwaniwa na watu watatu.
Kikao
chake kilichomalizika juzi usiku, kinadaiwa kubadili kanuni ya
kupendekeza wagombea watatu kwa nafasi moja na kwamba, hivi sasa
mapendekezo hasa kwenye jumuiya ni wagombea wanne.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa, hatua hiyo inalenga kutoa ushindani kwa wagombea.
Hata
hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipotakiwa
kuzungumzia suala hilo hakukanusha wala kukubali zaidi ya kusema kwamba
hata kama utaratibu huo umetumika siyo mara ya kwanza kwa chama hicho.
Alisema
kama Jumuiya ya Vijana wanaojitokeza lengo lao linakuwa kupata uzoefu
na kwamba, idadi ya majina inategemeana na busara za kikao kinavyoona
ili kutoa nafasi kwa wagombea kujipima.
Chanzo: Mwananchi
Wednesday, September 26, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment