Thursday, July 7, 2011

Biashara zafungwa Uganda siku ya pili

Best Blogger Tips
Via BBC

Wafanya biashara katika mji mkuu wa Uganda, Kampala wamefunga maduka yao kwa siku ya pili mfululizo kulalamikia kiwango cha sarafu ya nchi hiyo kinachoshuka kila kukicha pamoja na idadi kubwa ya wachuuzi wenye asili ya Kichina.

Wauza maduka wanadai kuwa sarafu dhaifu inapandisha bei za bidhaa kutoka nje.

Wakati huo huo wanasema hawawezi kushindana na wafanya biashara wa Kichina waliomimina bidhaa zao kwa wingi na kwa bei rahisi.

Mgomo wao wa siku mbili ni tukio la hivi sasa katika mfululizo wa maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha nchini Uganda.

Polisi wa kuzuia fujo walikuwa mitaani kulinda doria katika mji wa Kampala, kuzuia uwezekano wa kuzuka ghasia.

Msemaji wa shirika la wafanyabiashara la jiji la Kampala, Issa Sekito amesema kua wamefunga maduka yao kuishinikiza serikali ishughulikie masaibu yao.

Bw.Sekito amesema kua shirika lake limeitaka serikali ushughikie biashara za Wachina ambao wamezidsha kujiimarisha nchini Uganda.

Bw.Sekito aliliambia gazeti moja la nchini Uganda kuwa ''Kwa mda sasa,tumekua tukiilalamikia serikali juu ya hawa wageni wanaoshiriki biashara ndogo ndogo,hususan Wachina, wanaokuja wakidai eti ni wawekezaji'.

Shilingi ya Uganda ilidondoka kufikia kiwango cha chini dhidi ya dola ya Marekani mwezi uliopita hadi Benki kuu ilipoingilia kati kujaribu kuiimarisha.

Shirika la habari la Reuters limearifu kuwa 'Mgomo huo umesababisha bei ya bidhaa kama sukari na chumvi kupanda nchini humo''.

Mkaazi mmoja wa mji wa Kampala aliyehojiwa na shirika hilo, Linda Sempijja alisema kuwa maisha yamekuwa magumu kwa sababu bei ya bidhaa zote imepanda.

Mkaazi huyo aliongezea kusema kuwa hawezi kuwalaumu wafanyabiashara, kwa sababu wao pia wanakabiliwa na hali ngumu. Nailaumu serikali, alisema.

Gazeti la kiserikali la New Vision limearifu kuwa Waziri wa Biashara na viwanda,Bi.Amelia Kyambadde alikutana na wafanyabiashara kwa mda wa saa sita.

Waziri huyo aliwasilisha ujumbe kutoka kwa Rais Museveni akiwahimiza wasimamishe mgomo wao, kwa mujibu wa gazeti hilo.

Wafanyabiashara, hata hivyo walisema hawatofungua maduka yao na kwamba mgomo wao utaendelea hata siku ya leo alhamisi.

Wadadisi wanasema kuwa mgomo wao ni ishara ya hivi karibuni inayoonyesha hali ya ongezeko la kutoridhia kwa wananchi kwa serikali ya nchi.

Mnamo mwezi Aprili, vyama vya upinzani vilianzisha maandamano ya kususia usafiri wa umma na kutembea kwenda kazini, kama ishara ya kuitaka serikali itambue ukweli wa kupanda kwa gharama za maisha.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa vikosi vya usalama viliua watu tisa walioshiriki maandamanao hayo.

Serikali ilivilaumu vikundi vya upinzani kwa kujaribu kuteka madaraka kupitia ghasia baada ya kushindwa katika Uchaguzi mkuu uliofanywa mwezi Febuari.

Andrew Chenge kikaangoni

Best Blogger Tips
Via Majira

SAKATA la ununuzi wa rada ya ulioingizia serikali hasara, limechukua sura mpya baada timu ya wabunge iliyotumwa Uingereza kufuatilia malipo ya
fedha hizo kutoka Kampuni ya BAE kupendekeza kuangaliwa uwezekano wa kuwafikisha wahusika hao mahakamani.

Pendekezo la timu hiyo iliyokuwa chini ya Naibu Spika, Bw. Job Ndugai na wenzake Bw. Azan Zungu, Bi. Angela Kairuki na Bw. John Cheyo yamefanana na yaliyotolewa na Kambi ya upinzani bungeni juzi, kuwa wahusika katika kesi hiyo washtakiwe.

Kamati ya Ndugai ilisema kuwa pamoja na kesi hiyo kufungwa au kumalizika nchini Uingereza lakini Tanzania inayo nafasi ya kuwaburuta mahakamani watuhumiwa wa kashfa hiyo.

Ingawa timu hiyo haikutaja majina ya wahusika, miongoni mwa waliokuwa wanachunguzwa na Taasisi ya Makosa ya Jinai ya Uingereza (SFO), ni aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa sakata hilo, Bw. Andrew Chenge, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Idris Rashid na mfanyabiashara Sailesh Vithlan.

Lakini baadaye jioni, akijibu hoja za wabunge kwenye kuhitimisha mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma jana, Waziri wa Utawala Bora, Bw. Mathias Chikawe alimkingia kifua Bw. Chenge akisema Uingereza ilikwishamsafisha na hivyo hastahili kushtakiwa.

Mbali na wabunge hao kuitaka serikali kuchukua hatua za haraka kwa watuhumiwa hao zikiwemo za kuwafikisha mahakamani, pia wamelitaka bunge kutenga muda wa kujadili suala hilo ili wajue undani wake.

Akikabidhi taarifa ya safari hiyo kwa Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda jana, Bw. Ndugai alisema kuwa baada ya kamati hiyo kujadiliana na SFO, wameona bado kuna uwezekano wa kuchukua hatua zaidi kwa wahusika wote.

“Wakati tukiwa huko, moja ya changamoto ambayo tulikumbana nayo ni pale tulipohojiwa ni hatua gani tulizochukua kama nchi kuhusiana na suala hilo,” alisema Bw. Ndugai.

Alisema kuwa wao walijibu kwamba wamekwenda kwa nia ya kushinikiza kulipwa fedha zilizoamuriwa na Mahakama ya Uingereza kama chenji ya rada iliyouzwa kwa Tanzania kwa bei ya kuruka, kupitia serikalini badala ya asasi za kiraia za nchi hiyo, kwa kuwa ni za wananchi na wao ni wawakilishi wao, hivyo suala la kufungua kesi ni suala la serikali.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia alikuwa miongoni mwa timu hiyo, Bw. Mussa Zungu, alisema kuwa mafanikio yaliyopatikana katika ziara hiyo, ni pamoja na bunge la Uingereza na Serikali kutambua mchezo mchafu uliofanywa na Kampuni ya kuuza zana za kijeshi iliyouza rada hiyo, BAE Sustem, kwa kuiba na kuidhalilisha Tanzania kwa kutaka kulipa fedha hizo kupitia asasi za kiraia.

Hata hivyo alisema kuwa Julai 19 mwaka huu, timu hiyo imekaribishwa kwenye mjadala wa wazi ambao utakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo SFO, BAE, Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Kimataifa, Wizara ya Sheria ya Uingereza kwa lengo la kuweka mambo wazi kuhusiana na kitendo kilichofanywa na BAE, pia hiyo itakuwa ni fursa kubwa kwa timu ya bunge la Tanzania kuhoji maswali mbalimbali kuhusiana na mchakato huo.

Timu hiyo inataka fedha hizo zilipwe kwa riba inayoendelea kupatikana kutokana na fedha hizo kuwa katika akaunti ya BAE ambako zimehifadhiwa.

Kutokana na hali hiyo, wameitaka serikali kushirikiana na bunge kuhakikisha fedha hizo zinarudi na kuwa endapo hazitarudi mpaka Septemba 2011 hatua zaidi zichukuliwe kwa kampuni ya BAE.

Bw. Musa Zungu alisema kuwa hata baada ya kukutana na wahusika wa kampuni ya BAE, bado wamebaki na msimamo wao kuwa fedha hizo si tozo bali ni msaada.

Aidha timu hiyo pia ilikutana na Mkurugenzi wa SFO ambaye aliomba radhi kwa Serikali ya Tanzania kutokana na kushindwa kuishirikisha katika kesi hiyo wakati ikiendeshwa.

Mara kadhaa, Chenge amekuwa akikana kuhusika kwa namna yoyote na ufisadi huo wa rada na mara ya mwisho alijitokeza hadharani na kutangaza usafi wake baada ya SFO kuitimisha kesi hiyo bila kutaja chochote juu yake.

Utetezi wa Chikawe

Waziri Chikawe jana aliweka msimamo kwa niaba ya serikali kuwa
haiko tayari kumchukulia hatua yoyote Bw. Chenge kwa tuhuma za ununuzi wa rada hiyo.

Ilisema kuwa haina ushahidi wowote dhidi ya Bw. Chenge kuhusiana na tuhuma zinazoelekezwa kwake hasa kwenye sakata la ununuzi wa Rada ambao unadaiwa ulighubikwa na rushwa.

Hata hivyo, Bw. Chikawe alisema kuwa kama kuna mbunge yoyote au mtu yoyote mwenye ushahidi dhidi ya Bw. Chenge autoe na serikali itafanyia kazi siku hiyo hiyo.

“Suala la Rada limezungumzwa sana na limepotoshwa kwa kiasi kikubwa, SFO kwa kushirikiana na TAKUKURU walifanya uchunguzi wa kashfa hiyo na kubaini kuwa kwa hapa Tanzania hakuna mtu hata mmoja aliyehusika bali waliobainika katika makosa hayo ni watuhumiwa watatu kutoka nchini Uingereza,” alisema Bw. Chikawe.

Alisema kuwa waliohusika na kashfa hiyo, ni Bw. Sailesh Vithlan ambaye alikuwa dalali wa rada hiyo, Meneja Biashara wa Kampuni ya BAE, Bw. Jonathan Calman na mwingine aliyetajwa kama Bw. Christopher.

“Tutafanya kama kanisani kuwa mwenye ushahidi alete na asipoleta  hatutakwenda mahakamani kwa kuwa hatuna ushahidi, mahakamani huwezi ukaenda mikono mitupu ni lazima uwe na ushahidi wa kutosha...Chenge hatuna ushahidi naye na hili suala sasa nadhani mngeliacha,” alisema Bw. Chikawe.

Msimamo wa Upinzani

Juzi, Kambi ya Upinzania ilipinga fedha za rada kulipwa kupitia serikalini kwa madai kuwa haiaminiki na hasa ikizingatiwa kuwa fedha hizo zilipotelea mikononi mwake.

Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Sazan Lyimo alisema, "Kambi ya upinzani tunaona kuwa bila watuhumiwa hao kuchukuliwa hatua, ni dhahiri kuwa taifa haliwezi kuwa na uhakika wa kuzilinda vizuri fedha hizo za rada pindi zikilipwa pamoja na fedha zingine za umma ambazo zinaendelea kupotea kwa kuwa umekuwa ni utamaduni wa serikali kutochukua hatua.

“Tunataka Bunge lako tukufu lijadili na liazimie kuanzishwa kwa akaunti ya muda ya fedha za rada, itakayosimamiwa kwa pamoja na wawakilishi wa Asasi zisizo za kiserikali za Tanzania, wawakilishi wa sekta binafsi na mwakilishi wa serikali na tunataka fedha hizi zilipwe haraka iwezekanavyo kupitia akaunti hiyo,” alisema Bi. Lyimo.
Endelea kusoma habari hii.........................

Tuesday, July 5, 2011

Serikali yamsafisha rasmi Chenge

Best Blogger Tips
Via Tanzania daima

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwa kimewaweka pabaya makada wake watatu kinaotaka kuwafukuza uongozi katika vikao vikuu vya chama katika dhana ya kukjivua gamba, serikali imemsafisha rasmi mmoja wao, Andrew Chenge, ikidai hauhusiki na kashfa anazotuhumiwa.

Chenge, ambaye amekuwa akihusishwa na ufisadi katika ununuzi wa rada nchini Uingereza, alisafishwa na serikali jana bungeni kwa kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu makadirio ya matumizi na mapato ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

Alisema Chenge hahusiki na kashfa ya ununuzi wa rada. Badala yake, serikali imewataja waliohusika katika tuhuma hizo kuwa ni dalali Sailesh Vithlani na vigogo wawili wa Kampuni ya BAE System ya Uingereza, inayotengeneza zana za kivita.

Alisema kwa mujibu wa Shirika la Uchunguzi wa Makosa Makubwa la Uingereza (SFO) na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa nchini (TAKUKURU), Chenge hakuonekana sehemu yoyote kuhusika katika sakata hilo.

“Hakuna ushahidi kuhusu Chenge kuhusika na mchakato huo wa rada, hivyo hatuwezi kwenda mahakamani kwa hisia, ndiyo maana hadi leo tulikaa kimya,” alisema Chikawe.

Alisema suala la rada limekuwa likizungumzwa kwa muda mrefu na kwa namna mbalimbali, ikiwamo kupotoshwa, hivyo ikiwa kuna mtu ana ushahidi dhidi ya Chenge aupeleke kwa serikali ili wamshitaki haraka iwezekavyo.

“Kama hakuna ushahidi, ndiyo maana tunatangaza kama kanisani kuwa kama kuna mtu ana ushahidi na yanayosemwa alete, tutaushughulikia hata leo,” alisema Chikawe kwa kujiamini.

Hatua hiyo inachukuliwa wakati zikiwa zimebaki siku chache kwa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kukaa kujadili, pamoja na mambo mengine, kuwafukuza uongozi makada walioamuliwa kujiondoa wenyewe kwa tuhuma za ubadhirifu, ambao hadi sasa hawajajiondoa.

Katika hatua nyingine, Kamati ya Bunge iliyotumwa kufuatilia fedha za rada imewasilisha ripoti yake kwa Spika jana mchana huku ikipendekeza waliohusika katika kashfa hiyo ya ununuzi wa rada wa Tanzania na Uingereza wachukuliwe hatua.

Mapendekezo hayo yalitolewa jana na mjumbe wa kamati iliyoundwa kufuatilia fedha hizo, Mussa Azzan Zungu, kwa niaba ya wenzake. Kwa niaba ya kamati, Naibu Spika Job Ndugai ndiye aliyemkabidhi Spika Anne Makinda ripoti hiyo.

Katika ziara ya Uingereza, mbali na Ndugai na Zungu, wajumbe wengine walikuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki (CCM) na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP).

Kamati ilipendekeza pia kwamba ifikapo Septemba, kama BAE Systems itakuwa haijatekeleza matakwa ya kukabidhi pesa hizo serikalini, ishitakiwe.

Zungu alisema walipokuwa Uingereza walisisitiza kwamba pesa hizo si msaada bali ni haki ya Watanzania.

Alisema kwa sasa Bunge la Uingereza na serikali wanatambua mchezo mchafu uliofanywa na BAE kwa kutaka kulipa fedha zetu kwa kutumia asasi za kiraia. Alisema Serikali ya Uingreza imeona uonevu huo wa BAE Systems.

Awali Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Job Ndugai, alikiri kwamba walipokuwa Uingereza walikuwa wakihojiwa kama serikali imekwisha kuchukua hatua zozote dhidi ya watuhumiwa waliosababisha pesa hizo kuibwa. Alisema hii ndiyo ilikuwa changamoto kubwa waliyokumbana nayo.

Hata hivyo, alisema kuna ugumu katika kuwashughulikia wahusika, kwani BAE walikwisha kujiondoa katika kashfa hiyo na kesi ilikwishafungwa, wakajisafisha.

Kwa mujibu wa Ndugai, kamati za Kampuni ya BAE na SFO zinatarajiwa kubanwa na Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza kujibu tuhuma za sakata hilo la rada.

Ndugai alisema kikao hicho cha wazi cha pamoja kinatarajiwa kufanyika Julai 19 mwaka huu kwa kushirikiana na Wizara ya Sheria, Taasisi ya Rushwa ya Uingereza na wengine.

Kamati hiyo ilikwenda Uingereza Juni 17, 2011 na kurejea Juni 28, 2011 kushawishi BAE ilipe pauni milioni 29.9 na riba yake kupitia katika akaunti ya BAE zilikohifadhiwa.

Saturday, July 2, 2011

Strauss-Khan aachiwa bila dhamana

Best Blogger Tips
Via BBC

Aliyekuwa mkuu wa shirika la fedha duniani, IMF Dominique Strauss-Khan ameachiwa huru baada ya kupewa kifungo cha nyumbani na kurejeshewa dhamana yake ya dola za kimarekani milioni 3.7.

Imeripotiwa waendesha mashtaka wamekubaliana kuwa Bw Strauss-Khan aachiliwe huru "kwa udhamini wake mwenyewe," ikimaanisha aahidi kufika mahakamani.

Anatuhumiwa kumdhalilisha kijinsia mhudumu kwenye hoteli moja mjini New York mwezi Mei 14.

Lakini kesi hiyo inakaribia kufutwa baada ya kuibuka mashaka makubwa juu ya uaminifu wa aliyemshtaki.

Mwanasiasa huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 62 - aliyeonekana kuwa miongoni mwa wagombea wa urais wanaoongoza- alifika mahakamani siku ya Ijumaa.

Baada ya kutathmini taarifa za mwendesha mashtaka kutoka kwenye ofisi ya mahakama ya wilaya ya Manhattan, jaji ametangua masharti makali ya dhamana aliyopewa na Bw Staruss-Khan, lakini aliamuru kushikiliwa kwa hati yake ya kusafiria ili asiweze kusafiri nje ya Marekani.

Miongoni mwa yaliyowasilishwa ni taarifa kuwa mhudumu huyo alitoa ushahidi usio wa kweli kwa wazee wa baraza, bila kusema alisafisha chumba chengine kabla ya kumwambia msimamizi wake juu ya madai ya kudhalilishwa kijinsia.

Friday, July 1, 2011

Profesa Mwandosya, Prof. Lipumba walazwa

Best Blogger Tips
Via New Habari

VIONGOZI wawili, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba; na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, wanaumwa.

Wamelazwa katika Hospitali ya Apollo iliyopo katika mji wa Hyderabad, nchini India.

Profesa Lipumba alifika hospitalini hapo siku tano zilizopita kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Kwenye uchunguzi huo, kwa mujibu wa watu walio karibu naye, ilibainika kuwa anasumbuliwa na maradhi ya figo.

Juzi, Profesa huyo wa uchumi alifanyiwa upasuaji. Alipoombwa azungumzie maendeleo ya afya yake, hakuwa tayari kufanya hivyo kwa maelezo kwamba bado alikuwa akikabiliwa na ‘ulevi’ wa dawa.

Aliahidi kuzungumza leo au kesho kadri afya yake itakavyoruhusu. Baadhi ya watu walio karibu na mwanasiasa huyo walisema maendeleo yake kiafya yanaridhisha.

Kwa upande wake, Profesa Mwandosya amelazwa hospitalini hapo kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

Imeelezwa kwamba waziri huyo aliugua ghafla wakati akishiriki Mkutano wa Bajeti mjini Dodoma. Alikodishiwa ndege kwa dharura na kupelekwa Muhimbili. Hata hivyo, hali yake iliendelea kuwa mbaya na kulazimika kupelekwa nchini India.

Watu walio karibu na Profesa Mwandosya walisema kwamba anasumbuliwa na maradhi ya uti wa mgongo.

“Mheshimiwa Waziri anasumbuliwa na uti wa mgongo, kuna pingili imelika,” kilisema chanzo chetu.
Ilielezwa kwamba Waziri Mwandosya ilikuwa arejee nchini jana ili awahi kusoma bajeti ya wizara yake, lakini hali yake ilibadilika ghafla kabla hajaondoka.

Kubadilika kwa hali yake kuliwalazimu madaktari wamshauri aendelee na matibabu.
“Hali ilibadilika ghafla, ikalazimu apelekwe katika chumba cha x-rays, ana maumivu makali, lakini wananchi wasiwe na wasiwasi,” kilisema chanzo chetu.

Watanzania wengi wamekuwa wakienda kutibiwa nchini India. Hatua hiyo inatokana na upungufu wa vifaa uliopo nchini. Serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha vifaa na wataalamu wanapatikana ili kupunguza mzigo kwa Serikali wa kugharimia matibabu ya raia wake.

Tayari mipango madhubuti imeshakamilika kwa ajili ya kufanya upasuaji wa moyo na usafishaji figo hapa hapa nchini.

Zito alianika Baraza la Mawaziri

Best Blogger Tips
Via Mwananchi

WAKATI Ofisi ya Bunge ikigoma kumsaidia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kupata nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kuthibitisha madai yake kuwa Baraza hilo limerubuniwa, mbunge huyo amewasilisha kurasa nne za ushahidi huo akitumia dokezo la kikao hicho cha siri.

Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel zilisema kuwa Zitto aliwasilisha ushahidi huo kwenye Ofisi ya Bunge jana mchana, huku taarifa zaidi zikionyesha kuwa aliwasilisha ushahidi huo ukiwa na hoja tatu kuthibitisha madai yake.

Kwa mujibu wa habari hizo, mbunge huyo aliwasilisha ushahidi wake uliosomeka “Tofauti kati ya mapendekezo ya Waraka wa Barazaa la Mawaziri na Pendekezo la Azimio la Bunge lililoletwa bungeni kuhusu kuongeza muda wa Shirika Hodhi la Mali za Mashnirika ya Umma, yaani Consolidated Holding Corporation (CHC)" .

"Amewasilisha ushahidi wake leo, uko hapa unafanyiwa kazi," alisema Joel alipoulizwa na gazeti hili.

Juzi, Spika Anne Makinda alimwongezea muda Zitto hadi Jumatatu Juni 4 mwaka huu, kuthibitisha madai yake hayo baada ya kueleza kuwa alishindwa kufanya hivyo juzi, Juni 29 kutokana na ofisi ya Spika kugoma kumsaidia kupata nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kwa kuwa ni siri.

Akithibitisha hoja zake katika ushahidi huo ambao gazeti hili umefanikiwa kuuona, Zitto alisema, Azimio la Bunge lililowasilishwa bungeni na Serikali kabla ya marekebisho lilitaka CHC iongezewe muda wa mpito wa miaka mitatu na baadaye kazi zitakazokuwa zimebaki zipelekwe kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina ni tofauti na mapendekezo ya kitaalamu yaliyofikishwa mbele ya Baraza la Mawaziri.

Kwa mujibu wa maelezo ya Zitto, waraka wa wataalamu ulikuwa na mapendekezo ya aina mbili na kwamba hakuna hata pendekezo moja katika mapendekezo hayo lililozungumzia CHC kuongezewa muda wa miaka mitatu.

"Pendekezo la kwanza linalopatikana katika Aya ya 11.0 ya waraka huo, lilitaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu. Pendekezo la pili linalopatikana katika Aya ya 12.0 ya waraka huo, liligusia mpango mbadala wa kuiongezea CHC muda wa miaka 5," ilisema sehemu ya ushahidi huo.

Katika ushahidi huo, Zitto alisema Aya ya sita ya Azimio la Bunge ilianza kujenga hoja ya kutaka CHC iongezewe muda wa mpito na baadaye majukumu yake yahamishiwe kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina. Alisema aya hiyo ilisomeka hivi:

"Na kwa kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuiongeza muda wa mpito wa shirika na Serikali inaandaa na kukamilisha utaratibu wa kuhamishia majukumu ya CHC kwenye Ofisi ya Hazina.

"Wakati Azimio lililoletwa bungeni lilijenga hoja hiyo ya kutaka majukumu ya CHC yaje kuhamishiwa kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, Waraka wa Baraza la Mawaziri katika pendekezo lake la pili, umetahadharisha kuwa mpango wa kuhamishia kazi za CHC kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, utakabiliwa na changamoto kubwa,"ilisema sehemu ya ushahidi huo.

Ushahidi wake huo kwenye hoja ya tatu ulisema kuwa, wakati Azimio hilo lililoletwa bungeni (kabla ya kurekebishwa) lilijikita katika kutaka CHC iongezewe miaka mitatu na baadaye majukumu yake yahamishiwe kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, hitimisho la waraka uliowasilishwa kwa Baraza la Mawaziri katika Aya ya 13 linasomeka:

"Waheshimiwa mawaziri, mnombwa kutafakari mapendekezo yaliyomo kwenye Aya ya 11 ya waraka huu na kumshauri Mheshimiwa Rais ayakubali na aagize utekelezaji wake

"Hivi ni dhahiri kuwa Baraza lamawaziri lilikiuka maoni na ushauri wa wadau na watalaamu wote waliotaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu; na dhahiri kuwa Seriakli ilikiuka mapendekezo na sababu zake zote za msingi zilizowasilishwa katika kikao hicho ambazo zilitaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu" inahitimisha taarifa hiyo.

Juni 23 mwaka huu wakati anachangia Azimio hilo, Zitto alisisitiza mara tatu kwamba Baraza la Mawaziri limerubuniwa kufikia hatua hiyo na akawataka wabunge kwa umoja wao kutokubali kupitisha azimio hilo kwa kuwa lipo kwa maslahi ya watu.

"Waheshimiwa wabunge, nawaombeni kwa umoja wetu tulikatae azimio hilo, hicho sicho tulichokubaliana kufanya. Tayari tumeiagiza CHC kufuatilia madeni yetu kwenye kampuni za umma halafu leo, tunataka kuliua shirika hili? alihoji Zitto kabla Spika Makinda hajamtaka athibitishe kauli hiyo.

Kadhalika, wakati Makinda akimwongezea Zitto muda wa kuthibitisha madai yake alisema “Waheshimiwa wabunge itakumbukwa kuwa tarehe 23 mwezi huu Mheshimiwa Zitto wakati akichangia Azimio la Serikali kutaka kuliongezea uhai Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC), alitoa tuhuma bungeni kwamba Baraza la Mawaziri, limerubuniwa kufikia maamuzi hayo."

Aliongeza: "Itakumbwa pia kuwa baada ya kauli hiyo, nilimtaka (Zitto) alete ushahidi ifikapo tarehe 29 Juni yaani leo. Sasa kwa kuwa siku yenyewe ya kuleta ushahidi ni leo, naona bora nitoe taarifa rasmi kwenu."

"Kwamba siku ileile ya tarehe 23, Mheshimiwa Zitto aliniandikia barua kuniomba nimsaidie kumpatia nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichopitisha uamuzi huo. Amefanya hivyo kwa kutumia Kanuni ya Haki, Sura na Madaraka ya Bunge zinazompa haki mbunge kuiomba ofisi ya umma kumpa nyaraka anazozihitaji.

Hata hivyo, Makinda alisema, ofisi yake haikuweza kumpatia Zitto nyaraka hizo kwa kuwa vikao vya Baraza la Mawaziri ni siri na nyaraka zake zote hazitolewi kwa umma.

Thursday, June 30, 2011

Urusi: Wafaransa wamekiuka maadili Libya

Best Blogger Tips
Via BBC

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amelaani hatua ya Ufaransa kuwapa silaha waasi wanaopinga utawala wa kanali Muammar Gaddafi.

Bw Lavrov anasema hatua hiyo ikiwa imedhibitshwa ni kosa kubwa kwani imekiuka azimio 1970 la umoja wa mataifa ambalo linazuia silaha kuingizwa nchini humo na pande zote husika kwenye mzozo huo.

Wanajeshi wa Ufaransa walikiri kuwaangushia silaha wapiganaji wa kabila la Berber wanaoishi kwenye maeneo ya milima kusini mwa mji mkuu wa Tripoli.

Umoja wa Afrika pia umelaani uaamuzi wa Ufaransa wa kuimarisha nguvu za kijeshi za waasi hao.

Mwenyekiti wa tume ya Umoja huo Jean Ping amesema kitendo hicho kinaweka eneo zima hatarini.

Waziri wa mambo ya nje wa urusi amepanga kukutana na mwenzake kutoka Ufaransa Alain Juppe mjini Moscow kudhibitisha suala hilo tete.

Serikali ya urusi ilisusia kupigia kura mswada uliowasilishwa kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa kuruhusu harakati za kijeshi nchini Libya.

Mzozo unaoendelea mjini Libya ndio umepewa kipa umbele katika mkutano wa viongozi wa Afrika unaoendelea nchini Equatorial Guinea.

Bw Ping amesema kuna uwezekano mkubwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vikazuka nchini humo sawa na hali iliyoko nchini Somalia.

Mwenyekiti wa tume hiyo ya Umoja wa Afrika amefahamisha BBC kuwa mpango wa amani uliyobuniwa mnamo mwezi March bado unazingatiwa.

Mpango huo unataka pande zote zisitishe mapigano ili mazungumzo ya amani yaweze kuanza.
Habari kwamba Ufaransa imedondosha silaha nchini Libya zilijitokeza kupitia gazeti la Ufaransa, Le Figaro la jumatano.

Gazeti hilo lilisema kuwa Ufaransa, nchi inayoongoza operesheni ya NATO nchini Libya haikufahamisha nchi wanachama wenzake kuhusu operesheni hio.

Uwamuzi huo ulifikiwa baada ya mkutano uliofanyika mwezi April kati ya Rais Nicolas Sarkozy na Mkuu wa vikosi vya waasi wa Libya Gen Abdelfatah Younis.

Slaa afufua upya ufisadi

Best Blogger Tips
Via Raia Mwema

WAKATI wafadhili wakikabidhiwa ripoti inayoonyesha bado Tanzania kuna ufisadi, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameibuka na kusema hatorudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa kutokana na serikali kuwaogopa wala rushwa na mafisadi wakubwa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Raia Mwema, jana, Jumanne, Dk. Slaa amesema wakati wote ambao yeye na wenzake katika Upinzani wakipigania hatua kuchukuliwa dhidi ya mafisadi na wala rushwa wakubwa, serikali imekuwa na kigugumizi katika kuchukua hatua; huku ikitumia mbinu za kuwafunga midomo.

Akitoa mfano wa kesi mbalimbali zikiwamo za wizi katika akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA) kupitia kampuni ya Kagoda Agricultural Limited na kashfa ya rushwa katika ununuzi wa rada ya kijeshi, Dk. Slaa amesema serikali inawalinda wahusika wakuu.

 “Kampuni kama Kagoda wahusika wanajulikana lakini hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika. Hii si dalili nzuri maana inaashiria kwamba wakubwa wanahusika ama wanawaogopa wahusika. Hatudanganyiki na hatunyamazishwi, tutaendelea kusema na kutaka hatua zichukuliwe,” anasema na kuendelea;

“Kashfa ya rada ni aibu kusikia serikali inadai fedha za rada wakati ilikuwa na kigugumizi wakati Uingereza wakichunguza wahusika wa rada na walishindwa kutoa ushirikiano kwa wachunguzi, lakini sasa eti wanasikia kuna fedha ndio wanazitaka. Kwa nini walikataa kushughulikia wahusika kwa sheria zetu za Tanzania na kuachia Waingereza kila kitu?” alihoji Dk. Slaa.
Endelea kusoma habari hii....................

Aibiwa gari baada ya kuleweshwa

Best Blogger Tips
Via habariLeo

DEREVA teksi Minaji Omary (39), ameibiwa gari baada ya abiria aliyempakia
kumnywesha soda inayodhaniwa kuwa na dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolfina Chialo alisema, tukio hilo limetokea jana saa 6 usiku kwenye baa ya Uhuru, mjini Morogoro.

Gari iliyoibwa ni yenye namba za usajili T321 BCU aina ya Toyota Corola ambayo dereva wake, baada ya kunywa soda hiyo alipoteza fahamu.

Kamanda Chialo alisema, alfajiri dereva huyo alipoamka hakuiona gari wala
abiria huyo na ndipo alipofika katika Kituo Kikuu cha Polisi na kutoa taarifa hizo. Polisi wanaendelea na uchunguzi.

Katika hatua nyingine, Kamanda Chialo alisema, mkazi wa Kihonda, Amina Maulid amefariki dunia baada ya kunywa vidonge ambavyo havifahamiki. Chanzo cha kujiua hakijajulikana.

Mtoto wa mwanamke huyo ambaye polisi haikutaja jina lake, ndiye aliyetoa taarifa Polisi kuwa mama yake alifariki dunia Juni 28 mwaka huu saa 5:30 usiku eneo la Kihonda, mjini Morogoro.

Alisema, baada ya polisi kufika nyumbani kwao, walikuta dawa za aina mbalimbali kwenye meza ndani ya chumba alichokuwa amelala mwanamke huyo.

Polisi inaendelea na uchunguzi wakati mwili ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa.

Posho kumfukuza Shibuda Chadema

Best Blogger Tips
Via Mwananchi

KITENDO cha Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda kupingana na sera ya chama chake kuhusu suala la posho za vikao (sitting allowance), kimeichefua Chadema ambayo imemuita msaliti ikisema, "adhabu yake ni kufukuzwa.

"Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliliambia Mwananchi mjini Dodoma jana kuwa, alikerwa na kauli iliyotolewa na Shibuda ya kwenda kinyume na msimamo kambi hiyo kupinga posho za vikao kwa wabunge na wafanyakazi wengine wa umma.

Mbowe alisema kwamba kwa kauli yake ya juzi ya kuunga mkono posho ilidhihirisha kwamba mbunge huyo ni msaliti wa kambi hiyo, hivyo sheria zitafuata mkondo wake.

"Kutokana na tukio la jana (juzi) bungeni, Shibuda kutusaliti katika suala la posho za vikao, taratibu za kisheria zitafuata mkondo wake kwani utovu wa nidhamu haukubaliki katika kambi yetu, hata katika chama chetu,"alisema Mbowe na kuongeza:

"Suala la posho si la mtu binafsi, lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa 2010 ya chama chetu na kama kuna kiongozi hafahamu hili basi hakustahili kugombea ubunge kwa sababu naamini Ilani ya Uchaguzi, Shibuda anayo."

"Posho zilijadiliwa na kupitishwa katika vikao maalumu vya chama, kwa hiyo kama Katiba yetu ya chama inavyotuongoza, Shibuda alitakiwa kulipinga katika vikao hivyo sio kutoka nje ya kikao na kuanza kupingana na maamuzi yake,"alisema Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema.


Akinukuu kifungu katika Katiba ya chama chake kinachoeleza maadili ya viongozi, Mbowe alisema, "Kiongozi anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa na viongozi wa ngazi ya juu au vikao halali na kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kwa kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye kanuni."

Kauli ya Zitto
Kwa upande wake, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe, aliliambia gazeti hili jana kuwa mbunge kupingana na sera ya chama chake, ni kutokiamini chama hicho.

"Maana yake hakiamini chama, hivyo hafai kuendelea kuwa mwanachama na mbunge wa chama hicho,"alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.

Aliendelea, "Hapa kuna mambo mawili; masuala ya kisera na masuala ya utaratibu. Mbunge anayepingana na taratibu adhabu yake ni kumwita na kumpa onyo, lakini mbunge anayepingana na sera, huyo hakiamini chama na dhabu yake ni kufukuzwa."

Kwa mujibu wa Zitto, suala la kupinga posho kwa Chadema ni sera kwa kuwa limo kwenye Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

"Hili (suala la posho), lipo kisera. Kwenye Ilani yetu ya uchaguzi tulisema, tutapunguza mishahara ya wabunge na posho zao. Sasa kama mbunge anachaguliwa kwa sera hiyo halafu anaipinga haradhani, huyo hakiamini chama na chama hakipaswi kumwamini."

Aliendelea,"Sasa, adhabu ya juu kabisa ya mbunge asiyekiamini chama, ni kufukuzwa. Huu ni usaliti. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mwenyekiti wa chama ameshalitolea tamko suala hilo halafu mbunge anakuja kumpinga hadharani maana yake nini,?" alihoji.

Tundu Lissu je?
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema kitendo cha Shibuda kupingana na sera ya chama chake, "ni uasi usiovumilika".

"Sasa nikiwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni nadhani ninahitaji kukaa naye. Nitamwita anieleze kulikoni. Aseme kulikoni ameamua kukiasi chama na upinzani kwa ujumla?"

Aliendelea, "Lakini kwa bahati mbaya sana, adhabu kubwa inayoweza kutolewa na kambi ya upinzani ni kumtenga na kambi. Lakini kwa mtu kama Shibuda ambaye tayari anaijua adhabu hiyo na kuitafuta kwa makusudi, inaonekana haitamtosha."

"Kwa sababu hiyo basi, kambi ya upinzani itaenda mbali zaidi baada ya kumtenga. Tutakiandikia chama barua kukijulisha usaliti huo wa mbunge wake halafu chenyewe kina taratibu zake za kinidhamu."
Endelea kusoma habari hii...........................

Wednesday, June 29, 2011

Mwanamke wa kwanza kuongoza IMF

Best Blogger Tips
Via BBC

Waziri wa Fedha wa Ufaransa Christine Lagarde ameteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha duniani IMF.

Kufuatia uteuzi huo Ufaransa itakuwa imeshikilia kiti hicho kwa miaka 26 kati ya miaka 33 iliyopita.

Christine Lagarde mwenye umri wa miaka 55, alikuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa waziri wa fedha katika muugano wa nchi saba zilizostawi maarufu kama G-7.

Lagade anatarajiwa kujiuzulu kutoka serikali ya Ufaransa ili kuandikisha historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kuongoza shirika la fedha duniani IMF.

Uteuzi wake umefuatia kujiuzulu wa mfaransa mwenzake Dominique Strauss Kahn, baada ya kukabiliwa na kashfa ya ubakaji.

Sio wengi walioshangazwa na uteuzi wa wakili huyo wa zamani ambaye ana sifa nzuri kote duniani.
Amekuwa msuluhishi wa matatizo mengi ya kiuchumi yanayokumba mataifa kadhaa barani ulaya katika miaka ya hivi karibuni.

Kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa ameungwa mkono na China na India na hivyo kuteuliwa kwake kama mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la fedha duniani ilikuwa jambo lililotarajiwa.

Kuna maelewano ambayo hayajanakiliwa kuwa raia wa mataifa ya bara ulaya pekee ndio wanaopaswa kuteuliwa kuhudumu kama mkurugenzi mkuu wa IMF huku raia wa marekani wakipewa nafasi za kuongoza benki kuu ya dunia.

Mataifa yaliostawi yanataka kupewa nafasi kuu katika siasa za dunia, lakini huu ni wakati mgumu kwa mataifa ya ulaya huku mzozo wa kiuchumi wa Ugiriki ukitishia kuathiri mataifa mengine katika kanda hiyo.

Muungano wa ulaya na IMF zimeishurutisha serikali ya Ugiriki kupunguza matumizi yake ili kuendelea kupata msaada kutoka kwao.

Lagarde amekuwa katika mstari wa mbele kujaribu kutatua matatizo hayo ya nchi wanachama wa EU.

Tuesday, June 28, 2011

Hawara amuua mwenye mume

Best Blogger Tips
Via HabariLeo

MWANAMKE mkazi wa Ronsoti mjini Tarime mkoani Mara, Debora James (30), anatuhumiwa kumuua mwenzake, Teresia Nago, kwa kumchoma kisu katika mauaji yanayohusisha kugombea mwanamume.

Kwa mujibu wa Polisi, Teresia aliuawa jana saa 4.30 asubuhi Bomani mjini Tarime, baada ya kuchomwa visu viwili tumboni na kifuani na mgomvi wake huyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rorya/Tarime, Sebastian Zakaria, alisema Debora alikuwa akituhumiwa kuwa na uhusiano na mume wa Teresia, John Nago ambaye ni mtumishi wa Idara ya Ujenzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

Kaimu Kamanda alisema, wanawake hao wawili walikuwa na ugomvi wa muda mrefu na vurugu wakigombea mwanamume huyo.

Alisema, jana Teresia na Debora walikwenda kusuluhishwa na mzee wa Kanisa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja eneo la Bomani.

Lakini wakiwa Bomani, kulitokea vurugu na Debora ambaye alikuwa na kisu alimshambulia Teresia kwa kumchoma kisu kifuani karibu na moyo na tumboni na kusababisha kifo chake papo hapo, baada ya kutokwa damu nyingi naye akajichoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake kwa lengo la kujimaliza.

Kamanda Zakaria alisema Debora amelazwa katika hospitali ya wilaya mjini hapa chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kujijeruhi.

Monday, June 27, 2011

Best Blogger Tips
Libya yapuuza hati dhidi ya Gaddafi

Via BBC

Waziri wa sheria nchini Libya Mohammed al Qamoodi amesema hati za mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita za kutaka Kanali Muammar Gaddafi akamatwe zimelenga kuficha uhalifu wa Nato.

Akizungumuza mjini Tripoli, Bw Qamoodi amesema operesheni za Nato zinazoendelea nchini humo ni uhalifu wa kivita dhidi ya raia wa Libya lakini ICC imezifungia jicho.

Waziri huyo ameongeza kuwa wanajeshi wa Nato sasa wamepata kisingizio cha kumuua kiongozi wao Kanali Gaddafi.

Hata hivyo ametangaza kuwa Libya imepata fursa ya kufungulia Nato mashtaka ya uhalifu wanaoendeleza nchini Libya.

Mahakama hiyo imemtuhumu Gaddafi kwa uhalifu dhidi ya binadamu na kuamuru mashambulio kwa raia baada ya machafuko dhidi yake kuanza kati kati ya mwezi Februari.

Mahakama hiyo iliyopo the Hague pia imetoa hati ya kukamatwa kwa mtoto wake wa kiume Saif al-Islam na mkuu wa idara ya ujasusi Abdullah al-Sanussi.

Hatua hio imeendelea kuzua hisia tofauti.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Urusi, Konstatin Kosachev amesema kuwa uamuzi wa jaji hao sasa utavuruga juhudi za kutafuta suluhu ya mzozo huo.

Bw Kosachev amesema nia kuu ya jumuiya ya kimtaifa ni kuwa Kanali Gaddafi ajiuzulu na atoke nchini humo lakini sasa hilo huenda lisifanyike.

Badala yake, Kosachev amesema huenda kiongozi huyo atafanya kila juhudi kushinda vita hivyo na hii sio habari njema kwa Libya.

Lakini kwa upande wao, wapinzani wamekaribisha uamuzi huo.

Msemaji wao Ibrahim Dabbashi amesema sasa jukumu lipo kwa washirika wa Gaddafi kuelewa kuwa wanafanya kazi na mhalifu na wamshauri aondoke madarakani.

Maelfu ya watu wanaaminiwa kufariki dunia kwenye ghasia hizo.

Saturday, June 25, 2011

Best Blogger Tips
Katiba mpya 2014

Via Tanzania Daima

SERIKALI imetangaza rasmi kuwa Katiba mpya itazinduliwa Aprili 26 mwaka 2014, siku ambayo itakuwa ni maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akifungua Semina Elekezi kwa wakuu wa mikoa na wa wilaya kuhusu mchakato wa Katiba Mpya.

Semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper, Pinda alisema mchakato wa uundwaji wa katiba hiyo umeshaanza ambapo wananchi wamepewa fursa ya kutoa maoni yao.

Alisema matarajio ya serikali ni kuwa mpaka ifikapo mwaka 2014 mchakato wa Katiba mpya utakuwa umekamilika na Aprili 26 Katiba mpya itazinduliwa.

“Ni matarajio ya serikali kuwa Katiba mpya itakuwa imekamilika na kuzinduliwa ifikapo Aprili 26, 2014 katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,” alisema.

Pinda alisema kama mambo yote yatakwenda kama yalivyopangwa, Muswada wa Sheria kuhusu Mapitio ya Marekebisho ya Katiba utawasilisha bungeni mwishoni mwa Mkutano wa Nne wa Bunge unaoendelea hivi sasa.

Alisema iwapo muswada huo hautawasilishwa katika mkutano wa nne basi utawasilishwa mwanzoni mwa mkutano wa tano unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Waziri Mkuu, aliwataka wakuu wa mikoa na wa wilaya kutoa ushirikiano kwa Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni itakayoundwa ili kuwezesha mikutano ya hadhara ya kukusanya maoni kufanyika kama ilivyokusudiwa kwa kuhamasisha wananchi kuhudhuria na kutoa maoni yao.“Suala hili ni kubwa na la kitaifa, ni vyema viongozi wasiingize siasa na wajiepushe kuwashawishi wananchi katika kutoa maoni yao, bali wawaache watoe maoni kwa uhuru au pasipo shinikizo lolote,” alisema.

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa hatua ya sasa si ya kutunga Katiba Mpya bali ni kuunda Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi kuelekea kutungwa kwa Katiba Mpya.

Mchakato huo wa kuelekea uundwaji wa Katiba Mpya, umekwishaanza na katika hatua ya awali, serikali imeandaa rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba (The Constitutional Review Act) ya mwaka 2011.

Hata hivyo mchakato huo ulipata upinzani mkali kutoka kwa wadau mbalimbali wakipinga vipengele kadhaa vilivyomo kwenye muswada huo uliopelekwa bungeni kwa hati ya dharura katika Mkutano wa Tatu wa Bunge uliofanyika Aprili mwaka huu.

Miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa na wadau ni kuwa muswada huo uliandikwa kwa lugha ya Kiingereza ambayo ni watu wachache wanaoizungumza na kuielewa.

Wadau walipinga pia vituo vya kutolea maoni kuwa vitatu, ambavyo ni Zanzibar, Dar es Salaam na Zanzibar.

Hata hivyo serikali ililazimika kuuondoa muswada huo katika mkutano wa tatu wa Bunge na kuahidi kuwa utaandikwa kwa lugha ya Kiswahili na kuufanyia marekebisho kulingana na maoni ya wadau.

Wednesday, June 22, 2011

Best Blogger Tips
Pinda aacha kutumia Mercedes Benz

Via HabariLeo

KATIKA kile kinachotafsiriwa kuwa ni kuwatega mawaziri na viongozi wa Serikali wanaotumia magari ya kifahari na yenye gharama kubwa, Waziri Mkuu,Mizengo Pinda ameanza kuachana na matumizi ya magari yenye gharama kubwa.

Hatua hiyo inadaiwa kuwa inalenga kuwafanya mawaziri na viongozi wengine wa juu
wa Serikali, kupima, kutafakari na kuchukua hatua juu ya matumizi ya magari
ya gharama kubwa wanayotumia sasa ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele na
baadhi ya wabunge na wananchi.

Uchunguzi wa gazeti hili ambao ulithibitishwa pia jana jioni na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijjah, ulibaini kuwa Waziri Mkuu,
ameacha kutumia magari ya kifahari aina ya Mercedes Benz na Toyota
Land Cruiser VX na kuanza kutumia Toyota Land Cruiser GX.

Katika mahojiano maalumu na HABARILEO, Khijjah amethibitisha Pinda kuanza
kutumia aina hiyo ya magari katika misafara yake ambayo alisema ni ya gharama ya
chini ikilinganishwa na Benz na VX ambayo gharama yao ni kubwa sana.

“Ni kweli Mheshimiwa Pinda sasa ameamua kutumia magari haya ya GX, hajatangaza
popote juu ya uamuzi wake huu, lakini nahisi ni kama ujumbe kwa viongozi wengine
wa juu wa Serikali wanaotumia magari ya gharama kubwa ili kuwafanya nao wapime
na kuchukua hatua,” amesema Khijjah.

Katibu Mkuu huyo wa Hazina, alisema ipo mikakati kabambe iliyowekwa na Serikali
ili kudhibiti matumizi holela ya fedha za umma, lakini akasema si kila kitu lazima kisemwe bungeni, kwani mambo mengine yanahitaji utekelezaji wa moja kwa
moja.

“Mfano hatua hii ya magari ya msafara wa Waziri Mkuu kuwa ya gharama ya chini
unaonesha dhamira ya dhati ya kuanza kuokoa fedha za umma kwa matumizi yasiyo na sababu. Kama Waziri Mkuu anatumia gari kama hili kuna haja gani kwa kiongozi wa
chini kuagiza gari la thamani zaidi, haiwezekani,” alisema Khijjah.

Tuesday, June 21, 2011

Best Blogger Tips
Michelle Obama akutana na Nelson Mandela


Michelle Obama mke wa Rais wa Marekani amekutana na kiongozi wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake katika nchi mbili za kusini mwa Africa.

Wakfu wa Mandela umesema kuwa Bi Michelle Obama, mama yake na binti zake wawili wamemtembelea Bw. Mandela na kuzungumza nae kwa muda mfupi.

Mwandishi wa BBC Karen Allen ambaye yuko Johannesburg anasema kuwa shujah huyo wa ukombozi dhidi ya ubaguzi wa rangi mwenye umri wa miaka 92 anaonekana hafifu na ni nadra yeye kuwapokea wageni.

Ziara hii ya Michelle Obama inanuiwa kupigia debe umuhimu wa vijana uwongozini.

Ziara hii ni ya pili rasmi ambayo Michelle Obama amefanya peke yake tangu mumewe achukuwe hatamu za uwongozi mwaka 2009.Anatarajiwa kukutana na kiongozi wa sasa wa Afrika Kusini Jacob Zuma kabla ya kuelekea Bostwana.

Bi Michelle Obama pia anatarajiwa kuyatembelea makumbusho ya enzi za utawala wa ubaguzi wa rangi na mji wa mabanda wa Soweto ambao ulikuwa katikati ya harakati za kukabiliana na utawala wa wazungu waliochache katika enzi hizo za ubaguzi wa rangi.

Ziara hii pia itajumuisha kutembelea kisiwa cha Robin ambako Bw. Mandela alihudumu 18 kati ya miaka 27 aliyokuwa gerezani.

Bi Obama alikaribishwa Afrika Kusini jumanne jioni baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kijeshi mjini Pretoria ambako binti zake wawili Malia na Sasha walipewa blanketi kubwa zilizokuwa na rangi ya bendera ya Afrika Kusini kujikinga baridi.

Jumatano Michelle atakutana na viongozi vijana wa kike atakapotoa hotuba yake.
Source: BBC

Sunday, June 19, 2011

Best Blogger Tips
Familia ya Kawawa yagombea nyumba

FAMILIA ya aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu hayati Rashidi Kawawa, imesema itapigania kulinda heshima ya mwanasiasa huyo baada ya kuwapo tishio la nyumba yao iliyopo Kilimani mjini Dodoma inauzwa na kupangishwa na mama yao wa kambo.

Mama huyo, Asina Kawawa, anadai kuwa nyumba hiyo ni mali yake.

Kwa mujibu wa familia hiyo, nyumba hiyo inataka kupangishwa na mama huyo anayedai kwamba alirithishwa na Kawawa, licha ya familia kueleza kutotambua hilo, lakini pia ni makumbusho na moja ya maeneo ya kihistoria ya mwanasiasa huyo aliyepigania Uhuru wa Tanganyika.

Ingawa mama huyo anadaiwa kuwa mbioni kupangisha nyumba hiyo iliyopo kiwanja namba 34 eneo la Uzunguni mjini hapa, lakini ipo hatarini kuuzwa na benki ya CRDB baada ya kutumika kama dhamana ya mkopo wa Sh milioni 350 kwa ajili ya kujenga nyumba nyingine pembeni mwa hiyo, mali ya Asina.

Mmoja wa wanafamilia ya Kawawa, Zainab Kawawa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), aliwaeleza waandishi wa habari akiwa katika nyumba hiyo, kwamba familia inataka kulinda na kutunza heshima ya Mzee Kawawa, kwa sababu hakuwa mtu wa kukopakopa ovyo.
“Tunataka kulinda heshima ya Mzee Kawawa, tumemweleza mama kuwa tuko tayari kulipa deni hilo, lakini hayuko tayari, kwa sababu anaamini tukilipa deni nyumba hii itakuwa yetu, lakini zaidi ni kwamba tayari kuna notisi ya CRDB ya kuuza nyumba kutokana na deni,” alisema Zainab.
Alisema licha ya kuomba mkopo wa Sh milioni 350, ambao ulikuwa ukitolewa kwa awamu, mama huyo alipewa Sh milioni 74 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba hiyo ya ghorofa moja nyuma ya nyumba ya Mzee Kawawa, lakini sasa deni hilo limefikia Sh milioni 102.

“Kama familia, tulikaa na kuzungumzia deni hili na kukubaliana kuwa linatuhusu, hivyo baadaye lilisimamishwa na sasa limefikia Sh milioni 102, na tayari CRDB wanataka kuja kuuza nyumba hii kwa sababu ya deni,” alisema Zainab ambaye alizungumza na wanahabari baada ya mkutano kati yake na mama yake na mwanasheria Ngonyani kutoka makao makuu ya CCM.

Alisema kwa mujibu wa maelezo ya mama yao, nyumba hiyo aliyokuwa akiishi Mzee Kawawa kwa muda mrefu, aliinunua kwa ubia mwaka 2007 kutoka serikalini na inadaiwa kuwa ilikuwa na kipengele cha kuwa mmojawapo akifariki dunia, basi anayebaki atairithi. 
Endelea kusoma habari hii.....................

Thursday, June 16, 2011

Best Blogger Tips
Zawahir sasa ni mkuu wa Al-Qaeda


Ayman al-Zawahiri, ambaye kwa muda mrefu mno amekuwa msaidizi wa Osama Bin Laden katika kuiongoza Al-Qaeda, na akishikilia nafasi ya pili katika kutoa amri, sasa ataliongoza kundi hilo.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa katika wavuti ya kundi hilo.

Bin Laden aliuawa nchini Pakistan alipopigwa risasi na kikosi maalum kutoka nchini Marekani mwezi Mei.
Kundi la Al-Qaeda limeonya kwamba litaendelea na vita vyake dhidi ya Marekani na Israel chini ya uongozi wa Zawahiri.

Wadadisi wa masuala ya Al-Qaeda wanaelezea kwamba Zawahiri, mwenye umri wa miaka 59, na aliyezaliwa nchini Misri, ni mtu mwerevu sana, lakini hana uwezo wa kuwavutia wafuasi wengi kama alivyofanya Osama.

Baadhi ya wadadisi wanasema yeye ndiye aliyepanga na kuendesha shughuli nyingi zilizohusiana na shambulio la Marekani la 9/11.

Kwa muda wa miaka mingi, msaidizi wa Bin Laden, ambaye atakayefanikiwa kumpata atapokea dola milioni 25 (pauni milioni 15), alitazamiwa kurithi madaraka hayo.

Taarifa iliyotangaza madaraka hayo ilichapishwa katika wavuti ya Al-Qaeda, na kusemekana imetolewa na uongozi wa juu unaotoa amri katika kundi hilo.

"Sheikh Dk Ayman al-Awahiri, Mungu amsaidie, katika kuendelea na uongozi wa kundi", taarifa ilielezea.
Endelea kusoma habari hii..............

Monday, June 13, 2011

Best Blogger Tips
Mavs know Dirk is the primary reason they won an NBA title

Dirk Nowitzki had taken 12 shots, missed 11. He was -- for a shooter, for a scorer, for a leader -- having a nightmarish offensive game.

And since he and his Dallas Mavericks had mentally framed Game 6 as their Game 7, with a championship on the line not across 72 hours but right now, right then, Nowitzki could not have picked a worse time to suffer through a horrible, potentially crushing half of basketball.

OK, OK, Dallas actually was in front at that point, 53-51. So it wasn't a worst-case scenario, just a bad-case scenario. Especially if Nowitzki's just-off-the-mark shots kept missing, if the Miami Heat found their rhythm or (yikes) both.

His pal, Steve Nash, had Tweeted in the afternoon that he sensed a "monster" game from Nowitzki, and he wasn't far off. His many misfires were scaring small children.

"It was weird," Nowitzki said. "I had so many good looks. I can't even explain it. I had some threes, top of the key. I had a wide-open three in the corner. I had some pull-ups. I had some one-leg fadeaways that I normally make.

"The team always told me, 'Stay with it. Stay with it. You're too good of a shooter, too good of a player to keep missing.' "

Ya think?

Nowitzki isn't LeBron James, a player versatile enough or self-conscious enough -- you be the judge -- to turn away from his duties as a scorer. He did what shooters do and kept shooting.

He drained a 17-footer 12 seconds after halftime. He hit a pull-up bank shot on the break minutes later. He splashed a 3-pointer that made it 71-65 with 5:08 left in the third.
 Access the full story..................

Saturday, June 11, 2011

Best Blogger Tips
Marekani yathibitisha kifo cha Fazul

Via BBC

Waziri wa mashauri ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton, amesema kifo cha Fazul Abdullah Mohammed, aliyeshukiwa kuwa mkuu wa Al Qaeda Afrika Mashariki, "ni pigo kubwa" kwa kundi hilo na washirika wake.

Jumamosi serikali ya Marekani imethibitisha kifo cha Fazul Abdullah Mohammed, katika tukio la kufyatuliana risasi na vikosi vya Somalia mjini Mogadishu.

"Kifo cha Harun Fazul ni pigo kubwa kwa Al Qaeda, washirika wake wa siasa kali, na shughuli zake Afrika Mashariki," Clinton aliwaeleza waandishi wa habari akiwa mjini Dar es Salaam, Tanzania.

"Ni mwisho unaostahili kwa gaidi aliyewaletea wengi kifo na huzuni watu wasiokuwa na hatia Nairobi, Dar es Salaam na kwingineko; Watanzania, Wakenya, Wasomali na wafanyakazi wetu wa ubalozi".

Awali afisa mmoja wa cheo cha juu katika serikali ya Marekani alithibitisha kifo cha kiongozi huyo wa Al Qaeda Afrika Mashariki, na kuipongeza serikali ya muda nchini Somalia.

Kiongozi huyo wa Al Qaeda katika kanda ya Afrika ya Mashariki Fazul Abdullah Mohammed, alishukiwa kuhusika na shambulio dhidi ya balozi za Marekani katika Kenya na Tanzania mnamo mwaka 1998.

Fazul Abdullah amekuwa mtu anayetafutwa sana barani Afrika baada ya zaidi ya watu 220 kuuawa na zaidi ya 5000 kujeruhiwa katika mashambuliio ya mwaka 1998.

FBI iliahidi dola milioni 5 kwa kichwa chake.
Endelea kusoma habari hii......................

Friday, June 10, 2011

Best Blogger Tips
Tetemeko latikisa Dar

Via Majira

WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam jana walikumbwa na taharuki baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi lililodumu kwa sekunde kadhaa.

Tetemeko hilo lililotokea majira ya saa 5:28 asubuhi ambapo kwa mujibu wa wataalamu wa hali ya hewa lilitokea kilometa 52 kusini mashariki mwa jiji hilo.

Baadhi ya watu waliokuwa kwenye majengo marefu waliamua kuzikimbia ofisi zao kwa lengo la kujiokoa licha ya tetemeko hilo kutoleta uharibifu wa mali.

Vikundi vya wananchi vilionekana kujazana katikati ya mitaa mbalimbali nje ya majengo vikijadili tukio hilo.

Abdul Juma, mfanyabiashara aliyepanga katika jengo la PPF, alisema waliamua kutoka katika ofisi hizo kwa hofu kuwa huenda tetemeko hilo lingetokea tena.

“Ndugu yangu maisha ni matamu, mimi sijui nimeshukaje kutoka ghorofa ya tano, nilijawa na hofu baada ya kusikia tetemeko hilo.

Katika jengo la PPF House, askari polisi walionekana kurandaranda huku na huku kwa lengo la kuhakikisha kuna usalama wa raia na mali zao.

Taarifa za mtandao wa Geolojia zilisema kuwa tukio hilo lilikuwa na nguvu ya 4.8 upana kilometa 10.

“Tetemeko hilo limeonekana katika latitudo kusini mwa mstari wa greenwhich limekuwa kwa 7 na mashariki ni longitudo 39,” ilifafanua.

Taarifa hiyo iliyataja maeneo ambayo tetemeko hilo lilipita kuwa ni Zanzibar, Tanga na Nairobi nchini Kenya.

Tuesday, June 7, 2011

Best Blogger Tips
Rais Saleh wa Yemen 'aliumia' sana

Rais wa Yemen, Ali Abdullah Saleh, alijeruhiwa zaidi katika shambulio la makombora katika boma lake juma lililopita kuliko ilivyodhaniwa, maafisa wa Serikali wameambia vyombo vya Habari vya Marekani.

Maafisa wa Serikali waliambia shirika la Habari la AP kuwa Bwana Saleh alichomeka asilimia 40 ya mwili wake na anavuja damu katika fuvu lake kutokana na shambulio hilo la Ijumaa.

Rais anaendelea kupata matibabu nchini Saudi Arabia baada ya kushambuliwa katika Ikulu yake katika Mji Mkuu wa Yemen, Sanaa.

Afisa wa cheo cha juu Serikalini aliambia BBC kuwa hawatasema lolote kuhusiana na afya ya Rais Saleh.

"Sisi si madaktari. Na kama Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Bi Hillary Clinton alivyosema jana, sisi tuko hapa na Sanaa na tunafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa tunaleta mabadiliko kwa utaratibu, amani na bila ghasia, kama inavyosema Katiba ya Yemen," afisa huyo alisema.
Endelea kusoma habari hii....................

Sunday, June 5, 2011

Best Blogger Tips
Binti mbaroni kwa 'kubaka kavulana'

Via Majira

MSICHANA mwenye umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa), mkazi wa Kigogo, Luhanga, Dar es Salaam anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za 'kumbaka' mtoto wa
kiume mwenye umri wa miaka mitatu.

Msichana huyo anadaiwa kumbaka mtoto huyo mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo alimuiba nyumbani kwao na kumpeleka kwenye pagale, nyuma ya Shule ya Msingi Kawawa.

Mama mzazi wa mtoto aliyefanyiwa unyama huo, ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema, wakati akifanya usafi ndani ya nyumba yake siku ya tukio saa 4 asubuhi, mtoto wake alikuwa nje akicheza na wenzake.

Alisema alipomaliza ndani alitoka nje kumchukua mwanaye huyo ili ampe kifungua kinywa, lakini hakumwona ndipo, akaanza kumtafuta zaidi ya saa nzima bila mafanikio.

Mama huyo alisema, baada ya kuhangaika kumtafuta mwanaye, akili ilimtuma kuchungulia ndani ya nyumba hiyo inayojengwa na alipofanya hivyo alikuta mwanaye amelaliwa na msichana huyo.

Alisema kuona hivyo alikwenda mbio kuita mama mwingine jirani yake ili ashuhudie kitendo anachofanyiwa mwanaye.

"Nikiwa na jirani yangu tulishuhudia msichana huyo akifanya kitendo hicho kwa mtoto wangu," alisema.

Baada ya kushuhudia yote hayo, walipiga kelele na kumkamata akiwa uchi na kumpeleka Kituo Kidogo cha Polisi Kigogo- Luhanga.

Msichana huyo alishikiliwa kwa muda katika kituo hicho kidogo cha polisi kisha akahamishiwa Kituo cha Urafiki kwa hatua zaidi za kisheria ambapo mtoto aliyebakwa akilipelekwa katika Hospitali ya Amana kupatiwa matibabu.
Best Blogger Tips
UKIMWI uliginduliwa mwaka 1981

Mwaka wa 1981, daktari mmoja wa California Marekani aliona vijana wa kiume watano, walioshiriki katika mapenzi ya jinsia moja, wakiwa na ugonjwa usiokuwa wa kawaida.

Walikuwa na homa ya pneumonia na saratani ya ngozi.

Dakta Gottlieb hakujua kuwa ripoti zake, ndio zitakuwa historia ya kwanza kuandikwa juu ya ugonjwa ambao baadae utakuja kuwa janga kubwa la AIDS, au UKIMWI.

Virusi vya HIV viligundulikana miaka miwili baada ya ugunduzi huo wa Dakta Gottlieb.

Tena damu ikaweza kupimwa kama ina virusi vya HIV, na baadae zikapatikana dawa kadha za kudhibiti ugonjwa huo.

Umoja wa Mataifa unakisia kuwa tangu mwaka wa 1981, UKIMWI umeuwa watu milioni 30, na idadi kama hiyo hivi sasa wanaishi na virusi vya HIV.

Lakini juma lilopita, umoja huo uliripoti kuwa idadi ya watu wanaoambukizwa inapungua katika nchi kadha, lakini mamilioni ya wagonjwa bado hawapati dawa wanazohitaji.

Matabibu wanasema virusi vya HIV sasa wanavifahamu sawasawa, na wagonjwa wanaofululiza kula dawa kwa wakati, wanaweza kuishi karibu maisha ya kawaida.
Source: BBC

Saturday, June 4, 2011

Best Blogger Tips
NY-born twin friars die on same day at age 92

BUFFALO, N.Y. – Identical twins Julian and Adrian Riester were born seconds apart 92 years ago. They died hours apart this week. The Buffalo-born brothers were also brothers in the Roman Catholic Order of Friars Minor. Professed friars for 65 years, they spent much of that time working together at St. Bonaventure University, doing carpentry work, gardening and driving visitors to and from the airport and around town.

"It was fun to see them, just quiet, gentle souls," Yvonne Peace, who worked at the St. Bonaventure Friary for nearly 21 years, said Friday.

They died Wednesday at St. Anthony Hospital in St. Petersburg, Fla., Brother Julian in the morning and Brother Adrian in the evening.

Both died of heart failure, said Father James Toal, guardian of St. Anthony Friary in St. Petersburg, where the inseparable twins lived since moving from western New York in 2008.

"It really is almost a poetic ending to the remarkable story of their lives," St. Bonaventure spokesman Tom Missel said. "Stunning when you hear it, but hardly surprising given that they did almost everything together."

Julian and Adrian Riester were born Jerome and Irving on March 27, 1919, to a couple who already had five daughters. They took the names of saints upon their ordination in the Catholic church.
"Dad was a doctor and he said a prayer for a boy," Adrian once said, according to St. Bonaventure. "The Lord fooled him and sent two."

After attending St. Joseph's Collegiate Institute, the brothers were turned away by the military because of their eyesight, the university said. One had a bad left eye, the other a bad right eye.

Eventually they joined the friars of Holy Name Province in New York City. They received separate assignments before reuniting at the seminary at St. Bonaventure from 1951 to 1956. After serving parishes in Buffalo for 17 years, they returned to St. Bonaventure in 1973 and spent the next 35 years there.

They had separate rooms in the friary but one telephone extension that rang into both, Peace recalled. It was usually the more talkative Adrian who answered, though Julian possessed a quiet authority. They never said who was born first.

"Brother Julian was like the big brother. Brother Adrian would defer to him," Peace said. "They picked up one of our friars at the airport one time and the friar said, `Can I take you to dinner?'
"Brother Adrian looked at Brother Julian and said, `We aren't going to dinner?' `No, we'll go home,'" Peace said. "So that was it. No discussion, no contradicting. `No, we aren't going today.'"

Funeral services are scheduled for Monday at St. Mary Our Lady of Grace Church in St. Petersburg. Afterward, the brothers' bodies will be flown to Buffalo and buried Wednesday at St. Bonaventure Cemetery, across the street from the university.
Source: Associate Press

Friday, June 3, 2011

Best Blogger Tips
Mjane wa Sisulu A Kusini afariki dunia

Afrika Kusini inaomboleza kifo cha mmoja wa watu walioongoza harakati za kupambana na ubaguzi wa rangi, Albertina Sisulu, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.

Bi Sisulu alikuwa mjane wa Walter Sisulu, rafiki na mshauri wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela.

Mwanasiasa mashuhuri wa aina yake, alikuwa mpambanaji katika shirikisho la wanawake wa African National Congress (ANC).

Msemaji wa ANC Brian Sokutu alisema Bi Sisulu alikuwa wakati wote wa maisha yake akiwa katika harakati za kuleta demokrasia nchini Afrika Kusini.

Gazeti la Afrika Kusini la South Africa Times limemnukuu akisema, " Komredi Sisulu ametumia muda wake wote kuitumikia ANC na kuikomboa Afrika Kusini. Tunatoa heshima zetu kwa kiongozi huyu na mama wa harakati hizi."
Endelea kusoma habari hii...................

Thursday, June 2, 2011

Best Blogger Tips
Hillary Clinton kutembelea Afrika

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, atasafiri wiki ijayo kuelekea nchi tatu barani Afrika, kuzungumzia biashara, maendeleo  na masuala ya usalama wa kieneo.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema Clinton atatembelea Zambia, Tanzania na Ethiopia, kisha ataelekea Umoja wa falme za  kiarabu, ambapo atalenga mgogoro wa Libya.

Clinton amepangiwa kuhudhuria mkutano wa biashara nchini Zambia, utakaofanyika Ijumaa ya Juni 10 na kukutana na Rais wa Zambia, Rupiah Banda. Akiwa nchini Tanzania, wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani inasema Clinton, ataelezea mafanikio ya nchi mbili  ikiwa ni pamoja na program kadhaa zilizopo huko.

Clinton anatarajiwa kutembelea Umoja wa Afrika wakati akiwa Ethiopia na kukutana na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Jean Ping. Wakati wa safari yake, Clinton pia atakutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia,  Meles Zenawi na Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Source: VOANews

Monday, May 30, 2011

Best Blogger Tips
America's Best Affordable Places, 2011 

As the old saying goes, you get what you pay for. Unfortunately in real estate, value is a trade-off. Someone in Manhattan is willing to pay $2,200 per month to rent a studio apartment so as to be near jobs and cultural amenities, sacrificing square footage. For someone in Las Vegas, where housing is inexpensive—the city's median home value is about $115,000, according to real estate site Zillow.com—and the labor market is tough, the reverse is true. What if you could have both proximity to work and quality of life at an affordable cost?

While this may sound too good to be true, it's the status quo in some places.

In an exclusive ranking for Businessweek.com, Bloomberg Rankings analyzed government-gathered data on more than 3,000 counties across the U.S. to select the best affordable place in each state. We then scored each county by state. Next we tallied the top-ranked county in each state to arrive at a national ranking. Factors that were most heavily weighted include housing cost, crime, unemployment, and educational attainment in the county, in addition to such other metrics as family income, poverty, commute time, air quality, diversity, and share of families with children.

The Midwest made out well in the ranking. No. 1 on Bloomberg's list: North Dakota's Cass County, home to Fargo and West Fargo. Other areas with high scores include Brown County, S.D., Cleveland County, Okla. (in the West South Central region), Story County, Iowa, and Olmsted County, Minn.
Coastal states with high unemployment such as California, Florida, and Rhode Island ranked lower, as did states with a generally high cost of living, such as Hawaii.
Access the full story................

Friday, May 27, 2011

Best Blogger Tips
Hospitali kubwa ya moyo kujengwa Mlimani City

Via HabariLeo

HOSPITALI kubwa ya moyo itaanza kujengwa eneo la Mlimani City Dar es Salaam wakati wowote kuanzia sasa na kukamilika ndani ya miezi 30 ijayo, ili kutoa huduma ya upasuaji na tiba ya moyo.

Ujenzi huo utafanywa na Shirika la Hifadhi ya Jamii Nchini (NSSF) kwa ushirikiano na Hospitali ya Apollo za India, chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Tanzania.

Mkataba wa ujenzi huo ulisainiwa Ikulu Dar es Salaam jana mbele ya Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu wa India, Dk. Manmohan Singh na umelenga kuimarisha uwezo wa Tanzania kukabili magonjwa ya moyo, saratani na figo yanayohitaji utaalamu zaidi.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Rais Kikwete alisema hayo ni matunda ya ujio wa Dk. Singh nchini.

Rais alisema, ujenzi wa hospitali hiyo utaokoa mabilioni ya fedha za Serikali yanayotumika kupeleka wagonjwa wa moyo nchini India kwa ajili ya upasuaji na tiba nyingine pamoja na gharama za mafunzo ya madaktari.

Madaktari hao wamekuwa wakitumwa kupata utaalamu zaidi katika Hospitali ya Apollo nchini India lakini Rais Kikwete alisema fedha hizo za mafunzo zitaokolewa kwa kuwa wanachokifuata huko kitapatikana nchini.

Rais Kikwete alitoa mfano wa mwaka jana amabo Serikali ilitumia Sh. bilioni 11 kupeleka wagonjwa wake India kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa moyo wakati gharama hizo zingeweza kupungua zaidi kama huduma hiyo ingepatikana nchini.

“Kwa kuanzia, tutahakikisha hospitali hiyo mpya inakuwa na wataalamu bora wa kutosha wa kutibu ugonjwa wa moyo ndipo tuendelee na ule wa saratani na figo. Wenzetu wa Apollo wamekubali kuja kutumegea utaalamu kwa kutoa mafunzo hapa hapa nchini hospitali hiyo itakapo anza kazi miaka miwili na nusu ijayo.

“Hatutakuwa na sababu ya kuhamishia wagonjwa wetu wa moyo India tena kwa sababu mkataba tulio saini unaeleza wazi kuwa hospitali hiyo itatoa huduma kama tunayoifuata katika nchi hiyo. Vifaa vya tiba na wataalamu watakao wapa ujuzi wataalamu wa nchini pia watatoka India kwa makubaliano ya ushirikiano,” alisema Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa Kikwete, baada ya kusainiwa kwa mkataba huo wagonjwa wanaotakiwa kuhudhuria kliniki za moyo nchini humo kila baada ya miezi mitatu, hawatafanya hivyo kwa sababu madakitari wao watakuja nchini mara kwa mara kuwaona.

“Utaratibu huu upo kwenye makubaliano yetu na utatuondolea gharama tunazozipata sasa. Madaktari wa India wataanza kuwafuata wagonjwa wao nchini. Huu ni ushirikiano wenye faida,” alisema.

Akizungumzia uwezo wa madaktari wanaopata mafunzo kutoka kwa wataalamu wa India, Rais Kikwete alisema umedhihirika pale walipofanikisha operesheni 155 za moyo nchini.

Alisema, madaktari na wauguzi 29 wa magonjwa ya moyo na mengine yanayoambatana na ugojwa huo walipata mafunzo India na kufaulu kwa kiwango kizuri cha kuendesha huduma hiyo kwa upana zaidi nchini.

Mbali na hilo, Rais alimweleza Dk. Sigh kuwa uwekezaji wa nchi yake Tanzania ni Sh. bilioni 1.3 tu, kiasi alichosema kuwa ni kidogo sana ikilinganishwa na uzuri wa uhusiano wa nchi hizo mbili.

Alisema anaamini baada ya kusainiwa kwa mkataba huo kuhusu ukataji kodi, uwekezaji utaimarika maradufu kwa sababu kampuni iliyowekeza katika nchi hizo mbili itawajibika kulipa kodi kwenye nchi moja pekee.

Dk. Singh alimuhakikishia Rais Kikwete kuwa atafanya ushawishi wa kutosha kuuimarisha wawekezaji kuwekeza nchini.

Mbali makubaliano ya ushirikiano katika uwekezaji na ulinzi, Dk. Singh alimhakikishai Rais Kikwete kuwa nchi yake itaiwezesha Tanzania kupata ujuzi wa teknolojia mbalimbali na biashara ili iwe kitovu cha maendeleo katika Afrika Mashariki kwa kuwa ni mshirika wake wa karibu katika masuala ya kiuchumi.

Dk. Singh anayerejea nchini kwake leo alizindua mradi wa Kituo cha Ubora katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano cha Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) ulioanzishwa kwa ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Thursday, May 26, 2011

Best Blogger Tips
Wabunge, Waziri watunishiana misuli

Via Newhabari

WAZIRI wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Gaudensia Kabaka jana alivutana vikali na wabunge wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii waliokuwa wanataka kutembelea Kiwanda cha Vyombo vya Nyumbani cha Jambo Plastiki kilichoko Dar es Salaam.


Wakati wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa wamekwisha kujiandaa kwenda katika kiwanda hicho jana, ghafla Waziri Kabaka aliwaeleza kuwa ziara hiyo imeahirishwa hadi wakati mwingine.

Kabaka alitoa sababu za kutaka kuahirisha ziara hiyo kuwa ni mgogoro wa wafanyakazi na mwajiri kiwandani hapo ambao upo mahakamani hivyo ziara hiyo itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Baada ya kutolewa taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jenista Mhagama alikuja juu na kumweleza Kabaka kuwa kamwe kamati yake haiwezi kuahirisha ziara hiyo bila kutolewa sababu za kuridhisha. Alisema kitendo alichokifanya Waziri kinadhalilisha kamati yake.

“Mheshimiwa Waziri kitendo ulichokifanya unaingiza mgogoro mkubwa katika kamati ya Bunge… kwa mazingira ya sasa Watanzania hawana mahali popote pa kutolea shida zao zaidi ya bunge na hii inadhihirika wazi wataalamu wako hawakukushauri vizuri,” alisema Mbunge huyo wa Peramiho kwa tiketi ya CCM na kuongeza:
“Basi kama ni hivyo, Mheshimiwa Waziri mimi nakupisha uwe mwenyekiti wa kamati ya Bunge maana naona hutaki kutuelewa.”

Kuona hivyo, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alikwenda mbali zaidi kwa kusema kwa uzoefu uliopo nchini unaonyesha kuwa ziara hiyo tayari imekwicha kuchakachuliwa na wahusika kwa manufaa wanayoyajua wao.

Alisisitiza kwamba kama ziara itaahirishwa basi yeye hatakuwamo kwenye orodha hiyo.

Naye Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) alisema kama kamati haitaki kwenda kwenye kiwanda hicho yeye atapanga ziara yake kama mbunge wa Chadema na kwenda kusikiliza na kukagua mazingira kiwandani hapo.
Endelea kusoma habari hii.......................

Wednesday, May 25, 2011

Best Blogger Tips
Nato yaishambulia Libya usiku kucha

Takriban milipuko mikubwa mitano imeitikisa Tripoli usiku kucha, wakati harakati za majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato zikiendelea kwenye mji mkuu wa Libya.

Kwa usiku wa pili, mashambulio ya anga yalilenga ngome ya Bab al-Aziziya ya Kanali Muammar Gaddafi.

Nato inatekeleza azimio la umoja wa mataifa la kulinda raia wa Libya, kufuatia maandamano dhidi ya uongozi wa Kanali Gaddafi.

Lakini Urusi, ambayo haikuunga mkono azimio hilo, imesema uvamizi huo ni ukiukwaji wa umoja huo.

Mwandishi wa BBC Andrew North mjini Tripoli alisema mashambulio ya Jumanne usiku si makubwa kama yaliyofanyika Jumatatu usiku, lakini bado yalitikisa majengo eneo kubwa.

Moshi ulionekana kutanda kwenye mji huo.

Nato ilisema ngome hiyo ya Bab al-Aziziya imekuwa ikitumika kama kituo cha majeshi na magari ya kijeshi yaliyotumika kushambulia raia.

Lakini serikali ya Libya imesema Nato inajaribu kumwuua Kanali Gaddafi na mashambulio ya usiku yanawatisha raia wa Tripoli.
Source: BBC
Best Blogger Tips
Aliyekuwa mume wa mfanyakazi wa ndani aongea

Aliyekuwa mume wa  mwanamke ambaye ametangazwa na vyombo vya habari kwamba ni mama wa mtoto wa Arnold Schwarzenegger  aliyezaa nje ya ndoa, anasema kwamba anahisi kuzungukwa  na  aliyekuwa Gavana wa Califonia.

Katika mahojiano na jarida la Entertainment Tonight, Rogelio Baena anasema kwamba juma lililopita ndipo alipofahamu kwamba yeye siye baba mzazi wa mtoto huyo. Amesisitiza kwamba ataendelea kumtambua mtoto huyo kama ni wa kwake na si vinginevyo.

Jarida la “The Insider” siku ya jumanne lilionyesha video ya aliyekuwa mke wa Schwarzenegger, Maria Shriver akimsifia mwanamke huyo Mildred Baena katika sherehe ya mmoja wa jamaa zake, kwamba ni mwanamke jasiri na mfanyakazi hodari, huku Schwarzenegger akisikika kusema kwamba mfanyakazi huyo wa nyumbani amefanya kazi “nzuri sana”.

Mildred Baena, ametambuliwa kwamba ni mama mzazi wa mtoto wa Schwarzenegger na jarida la New York Times na  vyombo vingine vya habari.

Tuesday, May 24, 2011

Best Blogger Tips
Tiba ya Babu Samunge: Mwingine adai kupona ukimwi

Via Mwananchi

MKAZI wa Kijiji cha Galapo, Babati, mkoani Manyara, Abdalah Ally (38), aliyekuwa mgonjwa wa Ukimwi, amedai kupona ugonjwa huo na kinga zake za mwili (CD4) kuongezeka baada ya kunywa dawa ya Mchungaji, Ambilikile Mwasapila.Ally anakuwa mtu wa pili kujitangaza kupona Ukimwi baada ya kunywa kikombe cha dawa hiyo, baada ya Wilia John Lengume wa Samunge aliyekuwa wa kwanza kutangaza kupona ugonjwa huo baada ya kupata dawa hiyo.

Akizungumza jana kijijini hapa, Ally alisema kwamba amekuwa akitumia Dawa za Kupunguza Makali ya Ukimwi (ARV), tangu mwaka 2009 kabla ya kupata kikombe cha Babu, Januari 5, mwaka huu.

Akiwa na vyeti vya vilivyoonyesha kwamba alikuwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), Ally alisema kuwa Aprili 22, 2009 alipimwa na kukutwa na maambukizi hayo wakati huo akiwa mfungwa katika Gereza la Babati.

Alisema alipima afya yake Februari 25, mwaka huu wilayani Babati na katikia Kituo cha Msalaba Mwekundu na kukutwa hana tena VVU. Alipima tena katika Hospitali ya Wilaya ya Babati ambako pia alikutwa kinga yake ya mwili ni ya kutosha na hana tena VVU ndipo alipoamua kuacha kutumia ARV.

Alidai kwamba hata baadhi ya maofisa wa afya waliokuwa wakisimamia matibabu yake wilayani Babati walishangazwa na kupona kwake kwa tiba ya Mchungaji Mwasapila na hilo liliwafanya nao kufunga safari kuja Samunge Aprili 28, mwaka huu kupata kikombe.

"Ninavyo vyeti vinavyothibitisha kuwa sina tena Ukimwi na mwezi huu pia natarajia kupima kuona afya yangu ipo vipi," alisema Ally.
Endelea kusoma habari hii.....................
Best Blogger Tips
Mfugale bosi mpya TANROADS

WAZIRI wa Ujenzi John Magufuli amemteua, Patrick Mfugale, kuwa mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ephraim Mrema.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyopatikana Dar es Salaam jana kisha kutiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Herbert Mrango, kabla ya uteuzi huo Mfugale alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa uteuzi huo ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Mei 20 mwaka huu. Mfugale amewahi kushika nafasi mbalimbali serikalini ikiwemo kusimamia ujenzi wa barabara na daraja la Mkapa.

Katika taarifa yake, katibu mkuu alieleza kuwa injinia huyo ana shahada ya uhandisi (BSc Civil Engeneering) kutoka Chuo Kikuu cha Roorkee nchini India na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Loughborough, Uingereza.

Kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Barabara nafasi aliyoenguliwa na Rais, siku chache kabla ya kuingia TANROADS. Desemba Mosi mwaka jana, Mfugale aliteuliwa kukaimu nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS.

Sunday, May 22, 2011

Best Blogger Tips
Mali: Mabadiliko ya kura kombe la Dunia

Via BBC 

Rais wa Shirikisho la Soka la Mali Hammadoun Kolado Cisse ametaka mabadiliko yafanyike ya mfumo wa upigaji kura kutafuta nchi itakayoandaa Kombe la Dunia.

Pia amesema bado hajaamua nani atampigia kura katika uchaguzi unaokuja wa Rais wa Fifa.
Kauli hiyo ameitoa licha ya Shirikisho la Soka barani Afrika kueleza litamuunga mkono Rais wa sasa wa Fifa Sepp Blatter na sio mpinzani wake pekee Mohamed Bin Hammam.

"Kwa wakati huu siwezi kuzungumzia mgombea gani tutakayemuunga mkono," alisema Cisse.
Katika mkutano uliofanyika mjini Cairo siku ya Jumatatu, Shirikisho la Soka barani Afrika, lilisema kamati yake kuu imekuwa na kura ya siri na imepitisha muswda wa kumuunga mkono Blatter katika uchaguzi wa Fifa.

"Kamati kuu inaweza kutoa mapendekezo, lakini chama au shirikisho la soka la nchi huamua kivyake nani wa kumpigia kura," Cisse alifafanua.

"Hawapaswi kufuata mapendekezo ya kamati na baadhi ya nchi zinamuunga mkono Blatter na nyingine bin Hammam.

"Tunataka mabadiliko ya kweli ndani ya Fifa - namna tunavyofanya kazi, jinsi usimamizi wa fedha ulivyo - lakini siwezi kusema iwapo hicho ndio kigezo cha kubadilisha Rais."

Cisse anataka Mkutano Mkuu wa Fifa kuliko wajumbe 24 wa kamati ya utendaji kutoa uamuzi wa mwisho ni nchi gani ya kuandaa Kombe la Dunia.

Mchakato huo umezongwa na tuhuma za rushwa.

"Iwapo kila nchi itaweza kupiga kura kwa nchi itakayoandaa Kombe la Dunia, hiyo itasaidia sana kupunguza tuhuma za rushwa kwa sababu huwezi kuhonga vyama na mashirikisho 203 ya soka."

Cisse ameongeza kundi la nchi za Afrika litashauri mabadiliko haya kabla ya uchaguzi haujafanyika tarehe 1 mwezi wa Juni, lakini akakataa kusema iwapo nchi nyingine zitaunga mkono.

Pia amesema angefurahi mfumo wa wajumbe wa Kamati Kuu ya Fifa nao ungeangaliwa na kuwa na wajumbe zaidi ya wanne wa sasa kutoka nchi za Afrika.

Saturday, May 21, 2011

Best Blogger Tips
Mamia wamzika Sheikh Yahya


Via Tanzania Daima

MAELFU ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakiongozwa na viongozi wa serikali, dini, vyama vya siasa na makundi ya jamii jana walijitokeza kwenye mazishi ya mnajimu mashuhuri nchini na Afrika Mashariki ya Kati, Sheikh Yahya Hussein aliyefariki dunia juzi.
Sheikh Yahya Hussein (87), aliyefariki dunia juzi majira ya saa nne asubuhi, muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mtakatifu Ukombozi, Kinondoni baada ya kuugua ghafla alizikwa katika makaburi ya Tambaza.
Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mufti, Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Shaaban bin Simba, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), la Ubungo Kibangu, Anthony Lusekelo, ni miongoni mwa viongozi waliokuwapo kwenye mazishi hayo yaliyowafanya wakazi wa jiji hilo kuacha shughuli zao kwa muda ili kushiriki.

Baadhi ya viongozi waliokuwapo nyumbani kwa marehemu Sheikh Yahya, Mwembe Chai eneo la Magomeni, walisema kuwa kifo chake ni pigo kubwa kwa Watanzania na hasa Jumuiya ya Waislamu kwa kuwa alikuwa mstari wa mbele kupigania haki za Waislamu.

Mchungaji Lusekelo, alisema kuwa kifo cha Sheikh Yahya ni pigo kubwa kwa Waislamu na hata watu wa dini nyingine kutokana na kuwa msuluhishi mkubwa ilipotokea kuna kutokuelewana kwa viongozi wa dini hizo au makundi mengine ya kijamii.

“Siku tatu nyuma niliota Sheikh Yahya amepandishwa daraja kubwa la uongozi… lakini siku iliyofuata nikasikia taarifa za kifo chake, nilimheshimu na kumpenda kutokana na hekima na busara zake wakati wa uhai wake na hata ulikuwa ukija kwa ajili ya kuomba ushauri hakusita kufanya hivyo kwa wakati.

“Yapo aliyoyafanya na kuwa mchango mkubwa wa nchi yetu, lakini kutokana na aliyoyafanya Mungu amuweke mahali panapostahili, tupo pamoja katika kuomboleza msiba wa Sheikh Yahya na subira ni jambo jema kwa wafiwa,” alisema
Endelea kusoma habari hii..................

Friday, May 20, 2011

Best Blogger Tips
Sheikh Yahya Hussein afariki dunia

MTABIRI maarufu ndani na nje ya Tanzania, Sheikh Yahya Hussein leo asubuhi amefariki kutokana na tatizo la ugonjwa wa moyo baada ya  kukimbizwa Hospitali ya Ukombozi, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo asubuhi na  ilipotimu saa tatu asubuhi alikataka roho akiwa hospitalini hapo. Kwa mujibu wa mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye Hassan, baba yake atazikwa kesho saa saba mchana kwenye makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.

Sheikh Yahya ambaye wakati wa uhai wake alipata umaarufu mkubwa kutokana na kutabiri matukio makubwa katika maeneo mbalimbali duniani, alizaliwa wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, mashariki mwa Tanzania mwaka 1932.

Alipata elimu yake ya awali katika shule ya Al Hassanain jijini Dar es Salaam, kabla ya kwenda visiwani Zanzibar ambako aliendelea na masomo katika chuo cha Muslim Academy.

Baada ya kuhitimu alikwenda nchini Misri alikopata elimu ya juu zaidi katika masuala ya dini ya Kiislam katika chuo kikuu cha Al Azhar kilichoko jijini Cairo.

Sheikh Yahya Hussein baadae alirejea nchini Tanzania mwanzoni mwa miaka ya sitini na kuanza shughuli zake za utabiri wa elimu ya nyota akiwa mtabiri wa mwanzo kabisa kueneza shughuli za utabiri wa nyota katika magazeti mbalimbali ya ukanda wa Afrika Mashariki.

Mnajimu huyo, amewahi kuendesha shughuli zake katika nchi za Afrika Mashariki na maeneo mengine duniani.

Pamoja na elimu yake ya unajimu, vile vile Sheikh Yahya Hussein alikuwa kiongozi wa dini ambaye pia alijihusisha na uchambuzi wa masuala ya siasa kupitia utabiri hususan wakati wa uchaguzi, ingawa hakushiriki kikamilifu katika kuwania nyadhifa zozote za kisiasa.

Pia alivuma sana katika kutabiri matokeo ya mechi kubwa za soka katika michuano ya Gossage na hata timu za Simba na Yanga za Tanzania bila kusahau vifo vya watu mashuhuri kama wanasiasa na wasanii pamoja na matukio makubwa duniani.

Marehemu Yahya Hussein ameacha mjane na watoto wapatao ishirini.

Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits