SIKU chache baada ya kuuawa kwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar
Gaddafi, walibya na dunia kwa ujumla imeingia katika mitizamo tofauti
kuhusu kiongozi huyo huku wengi wakikumbuka mafanikio aliyoleta kwa
taifa hilo tofauti na viongozi wengine waliong’olewa kwa udikteta.Baadhi
ya vyombo vya habari vimekuwa vikimtangaza na kutafuta namna zote za
kujenga picha ya udikteta bila kuangalia upande wa pili wa Libya
iliyooachwa na Gaddafi.
Baadhi ya mambo ambayo yamekuwa
yakizungumziwa ni iwapo Libya ya sasa itaweza kuneemeka na kile ambacho
ilikuwa ikipata kutoka kwa kiongozi huyo, ambaye hivi karibuni aliuawa
na wapinzani wake.
Gaddafi, tofauti na viongozi wengine
waliowahi kutajwa kuwa madikteta duniani, ana mengi ya kukumbukwa na
kusifiwa kwayo.Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kiuongozi
wamekuwa wakieleza kusikitishwa kwao na kutotambua aina ya demokrasia
ambayo baadhi ya watu wa Libya wanaililia kwa sasa na iwapo itaboresha
au kuharibu kabisa maisha yao.
Hii inawekwa wazi kwamba pamoja
na kwamba Gaddafi ametumia fedha nyingi za Libya katika masuala
binafsi, lakini je, kwa wastani Libya ni maskini? Wapo viongozi
waliozitumia nchi zao na kuziharibu kabisa, Gaddafi aliwahi kuifilisi
Libya?
Haya ni baadhi ya mambo ambayo Gaddafi aliyasimamia na
kuyatekeleza katika utawala wake wa miaka 42 kwa Libya.Kwa mujibu wa
taarifa zilizotolewa na tovuti za mawasiliano za Libya na Zimbabwe
zimeeleza kuwa nchini Libya hakuna mwananchi aliyewahi kulipa bili ya
umeme, umeme ulikuwa bure kwa raia wake wote.
Hakukuwa na riba
katika mikopo, benki zote Libya zilikuwa chini ya Serikali, mikopo
ilitolewa kwa wananchi bila riba ya kiasi chochote .
Taarifa hizo
zikafafanua kuwa makazi ni haki ya msingi nchini Libya, Gaddafi aliwahi
kusisitiza kwamba wazazi wake hawawezi kupata makazi hadi kila raia
apate makazi. Baba wa Gaddafi alifariki dunia wakati yeye, mama yake
wakiwa wanaishi katika hema.
Wanandoa wote wapya nchini humo
walipata Dola 50,000 kwa Serikali kwa ajili ya kununua makazi yao
kuwasaidia kuanzisha familia mpya.Elimu na huduma za kiafya vilitolewa
bure. Wakati Gaddafi nachukua nchi asilimia ya waliokuwa na elimu
ilikuwa 25, kwa sasa inafikia 83.
Kwa waliotaka kuwa wakulima,
walipewa ardhi bure, nyumba katika shamba lao, vifaa, mbegu na mifugo
kwa ajili ya kuanzisha miradi.Iwapo kuna waliokuwa hawawezi kupata
huduma za elimu na afya wanazostahili, Serikali iliwalipia kwa ajili ya
kuzipata nje ya nchi, hizi hazikuwa bure, walitakiwa kuchangia, walipata
Dola2,300 kwa mwezi kwa ajili ya makazi na usafiri.
Kwa
waliokuwa wakitaka kununua magari, Serikali ililipia kwa asilimia 50 ya
bei. Bei ya petroli ilikuwa karibu na bure, lita ililipiwa kwa Dola
0.4.
Libya haidaiwi nje, pia ina akiba inayofikia Dola150 bilioni
nje ambayo kwa sasa imezuiliwa.Kwa waliomaliza vyuo, Serikali
iliwapatia posho sawa na mshahara wa maofisa hadi watakapopata ajira
yenye uhakika. Sehemu ya mauzo ya mafuta ya Libya iliwekwa moja kwa moja
kwenye akaunti ya raia wake.
Kila mwanamke aliyejifungua alipata
posho ya Dola5000, mikate 40 iliuzwa kwa dola0.15, asilimia 25 wa
Walibya, wana shahada ya chuo kikuu.Kama hiyo haitoshi taarifa hizo
zimeeleza kuwa alisimamia mradi mkubwa kabisa wa umwagiliaji, uliopewa
jina la Great Man-made River, kuhakikisha maji yanakuwepo kwenye maeneo
yote ya nchi yenye jangwa.
Wakati wa vikwazo kwa Serikali yake
miaka ya 1980, Libya ilikuwa miongoni mwa nchi tajiri kabisa kwa msingi
wa pato la ndani, ikwa na kiwango cha juu cha maisha kuliko Japan.
Ilikuwa ni nchi tajiri kuliko zote kabla ya vuguvugu la mapinduzi.
Wastani
wa kiwango cha maisha kwa pato la kichwa ni Dola11,314 . Gaddafi
amewahi kutumia fedha nyingi kwa ajili ya safari zake na miradi yake,
lakini amefanya mabo makubwa ambayo hakuna dikteta aliyewahi kuyafanya
kwa watu wake. Alirejesha pato kwa watu wake, aliwajali.
Wosia wa Gaddafi kabla ya kifo
Katika wosia wake, Kanali Gaddafi aliwaasa wafuasi wanaomuunga mkono kuendelea kupambana.
Alielezea
msimamo wake kuwa amechagua kupambana hadi hatua ya mwisho na kufia
katika ardhi ya Libya kuliko kuchagua njia nyepesi, ambayo kwa mtizamo
wake, ni kitendo cha kujidhalilisha kisichokuwa na heshima, kukimbilia
uhamishoni nje ya nchi yake, ambapo tayari alishapata ahadi nyingi za
ulinzi.
Katika lugha ya Kiingereza, waraka wake wa wosia
umetafsiriwa ukisomeka: “Hii ni hiyari yangu. Mimi Muammar bin Mohammad
bin Abdussalam bin Humayd bin Abu Manyar bin Humayd bin Nayil al Fuhsi
Gaddafi, ninaapa kwamba hakuna Mungu mwingine zaidi ya Allah na Muhammad
ni Mtume wake, amani iko kwake. Ninaahidi nitakufa nikiwa Muislamu.
“Iwapo
nitauawa, nitapenda kuzikwa kwa mujibu wa taratibu za kiislamu, nikiwa
nimevaa mavazi nitakayokuwa nimevaa wakati kifo change kikitokea, bila
mwili wangu kuoshwa, katika makaburi ya Sirte, jirani na familia na
jamaa zangu.
“Nitapenda kwamba familia yangu, hasa wanawake na
watoto, watunzwe vyema baada ya kifo changu. Watu wa Libya wana wajibu
wa kulinda wasifu, mafanikio, historia na heshima ya waasisi na mashujaa
wake.
“Watu wa Libya hawatakiwi kupuuza kujitapa na lazima wawe
watu huru wa kuthaminiwa. Ninawataka wale wanaoniunga mkono kuendelea
kupambana, kuwakabili wote wanaosimama kutoka nje dhidi ya Libya, leo,
kesho na siku zote.
“Hata kama hatutashinda mapema, tutatoa
funzo kwa vizazi vyetu vijavyo, kwamba kuchagua kulinda utaifa ni
heshima na kuliuza ni uasi mkubwa ambao historia haitausahau milele,
pamoja na juhudi za wengine kuwaeleza kinyume cha hayo”.
Endelea kusoma habari hii.....................
Monday, October 24, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment