Ajali ya Kikwete yaivuruga Ikulu
Via Tanzania Daima
TAASISI za usalama zimeanza kufanya uchunguzi kubaini kiini hasa kilichosababisha magari mawili aliyoyapanda Rais Jakaya Kikwete kukumbwa na hitilafu kwa nyakati tofauti, wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja, jijini Dar es Salaam juzi.
Kikubwa kinachoonekana kuvishtua vyombo vya habari ni kuchomoka kwa gurudumu la nyuma la gari mojawapo, muda mfupi tu baada ya rais kuteremka kwa dharura na kupanda gari jingine.
Vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka ndani ya serikali, vimelieleza Tanzania Daima Jumatano kuwa kinachochunguzwa ni kubaini iwapo hitilafu hizo zilitokea kwa uzembe, hitilafu za kawaida au hujuma.
Katika siku za hivi karibuni, Rais Kikwete amekuwa akijikuta katika taarifa zisizo sahihi kwa kupotoshwa na wasaidizi wake, hali ambayo baadhi ya wadadisi wa mambo ya kisiasa, wakiamini kama ni hujuma dhidi ya kiongozi huyo.
Vyanzo vyetu vya habari kutoka duru za usalama, ziliiambia Tanzania Daima Jumatano jana kuwa idara ya usalama imekuwa ikifanya vikao nyeti juu ya tukio hilo ambalo limechukuliwa kwa uzito mkubwa na serikali.
Wakati idara ya usalama ikihaha kupata chanzo cha tukio hilo, Ikulu kwa upande wake nayo ilikuwa ikihaha kubaini chanzo cha tukio hilo na ikiwezekana kuchukua hatua.
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdallah Msika, alipoulizwa na Tanzania Daima Jumatano kuhusiana na tukio hilo, kwanza alisita kusema kwa madai kuwa liko ngazi ya juu zaidi na kumtaka mwandishi wa habari hizi aonane naye saa saba mchana.
Hata ilipofika muda huo, Msika alisema polisi imelichukulia tukio hilo kama ajali ya kawaida na halina mpango wa kuunda kamati kulichunguza.
Huku akiwa makini kuchagua maneno ya kuzungumza, Msika alisema tatizo hilo ni la kawaida kwani uchunguzi umebaini kuwa lilitokana na hitifalu za kiufundi na si vinginevyo.
Endelea kusoma habari hii..............
Tuesday, May 25, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment