Wednesday, May 12, 2010

Best Blogger Tips
David Cameron Waziri Mkuu mpya Uingereza


Kiongozi wa chama cha Conservative, David Cameron, ndiye Waziri Mkuu wa Uingereza baada ya Gordon Brown kujiuzulu Jumanne jioni.

Maelezo mafupi kuhusu David Cameron

David Cameron wakati fulani alijitaja kama ‘mrithi wa Tony Blair’. Hakika kuna mfanano wa namna alivyoweza kwa kutumia kikundi kidogo cha wanasiasa wa ‘kisasa’ kulazimisha mabadiliko ndani ya chama ambacho husita kufanya mabadiliko.

Pia bwana Cameron mwenye umri wa miaka 43 anafanana na Waziri Mkuu wa zamani bwana Blair kwa umahiri wake wa kuongea mbele ya kamera za runinga.

Akiwa ni mtoto wa dalali wa hisa (stock broker), Bwana Cameron alikua katika eneo la Newbury, Berkshire, pamoja na kaka yake aitwaye Alec na dada wawili Tania na Claire.

Baada ya elimu ya awali, akafuata jadi ya kifamilia na kusoma Eton na baadae chuo kikuu cha Oxford, ambapo alipata daraja la juu kabisa (la kwanza) katika Falsafa, Siasa na Uchumi. Mhadhiri wake wa Oxford aitwaye Vernon Bogdanor anamtaja bwana Cameron kama mmoja wa wanafunzi wenye uwezo mkubwa aliowahi kufundisha.

Chuoni Oxford hakujishughulisha na siasa za wanafunzi, lakini alikuwa mwananchama wa klabu ya Bullingdon dining, maarufu kwa unywaji wa pombe na mienendo mibaya. Hata hivyo bwana Cameron siku zote ameepuka kuongelea suala hili la unywaji mkali wa pombe chuoni na amekanusha kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya wakati akiwa mwanafunzi. Lakini inaweza kuwa ni makosa kufikiri kuwa bwana Cameron alikuwa tu mtu wa tabaka la aina ya viongozi wa chama cha Tory wa zama zilizopita. Hii ni kwa kuwa sehemu muhimu ya mvuto wake kisiasa imekuwa ni madai yake ya yeye kuwa sambamba na Uingereza ya leo kuliko wapinzani wake kutoka chama cha Labour. Anakamilisha maneno yake haya pale anapokiongoza chama chake kukumbatia dhana zenye mvutano wa kisiasa leo hii kama vile mabadiliko ya hewa duniani na haki za wasenge (gay rights).
Endelea kusoma habari hii............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits