Polisi watano watiwa mbaroni kwa mauaji
Via Tanzania Daima
ASKARI polisi watano wa Kituo cha Oysterbay cha jijini Dar es Salaam, wametiwa mbaroni wakihusishwa na kifo cha kupigwa risasi cha raia, Octavian Kashita (38) kilichotokea juzi Jumapili.
Kashita anaaminika aliuawa kwa risasi na polisi wakati yeye na wenzake wengine wanne walipokuwa wakipinga kitendo cha polisi hao cha kutaka kuwakamata, wakiwahusisha na tuhuma za kuhusika katika tukio la utekeji nyara.
Habari za kipolisi zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, zinaeleza kuwa, tukio hilo la mauaji lilitokea katika eneo la Victoria katika eneo la nyumba za serikali.
Kova aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa, polisi hao walikwenda eneo la tukio majira ya saa 1:00 jioni baada ya kupata taarifa za kutekwa nyara kwa mtu aliyetajwa kwa jina la Bariki Minja.
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, polisi hao walikwenda eneo hilo la tukio baada ya kupokea malalamiko ya dada wa Bariki anayedaiwa kutekwa nyara, aliyemtaja kwa jina la Sia Minja.
Alieleza kuwa kutokana na taarifa hizo, mlalamikaji aliwaongoza askari hadi eneo la Victoria walipokuwa wameelekea watekaji hao.
Kova alieleza kuwa walipofika eneo hilo, waliliona gari aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 864 BHC ambalo ndilo lililodaiwa kutumiwa na watekaji nyara hao.
“Kwa kupitia mlalamikaji (Sia), polisi waliwakamata vijana wanne waliosadikiwa kuhusika na utekaji huo kwa lengo la kuwahoji,” alisema Kova.
Alisema mara baada ya kuwakamata watuhumiwa hao wa utekaji, ikiwa ni pamoja na kumkuta mateka mwenyewe akiwa ndani ya gari hilo, kuliibuka mvutano kati ya polisi na watuhumiwa.
Endelea kusoma habari hii kwa undani............
Monday, May 17, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment