Kikwete azikataa kura za TUCTA
• Asema wasipompa, wengine watampigia
HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete amewatisha wafanyakazi ambao wamepanga kushiriki kwenye mgomo ulioitishwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) uliopangwa kuanza kesho kuwa watakumbana na mkono wa sheria endapo watathubutu kutekeleza azma yao hiyo.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana jioni jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wazee wa mkoa huo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alisema kuwa mgomo unaoshinikizwa washiriki ni batili na kinyume cha sheria kwa kuwa umeitishwa katikati ya mazungumzo.
“Mie ndiye muajiri mkuu nisikilizeni mimi, msimsikilize Mgaya (Kaimu Katibu Mkuu TUCTA) mtafukuzwa kazi wala Mgaya hamtamuona! Mtapoteza haki zenu…akili ni nywele kila mtu ana zake mtu mzima dawa,” alisema Kikwete ambaye alikuwa akishangiliwa na wazee hao.
Akiwa ameongozana na Makamu wa Rais, Dk, Ali Mohamed Shein, Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi na viongozi wengine wa chama na serikali, Rais Kikwete alianza kwa kusema kuwa ana mambo mawili ya kuzungumza na wazee hao, na akatamka moja kati ya hayo kuwa ni tishio la mgomo wa TUCTA.
Wengine waliohudhuria mkutano huo wa Kikwete ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema na viongozi wengine wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Rais Kikwete alisema kuwa hakupenda kulizungumzaia suala hilo kwa sababu alikwishalitolea ufafanuzi mwezi Machi mwaka huu lakini amelazimika kulizungumzia baada ya kuwasilikiliza viongozi wa TUCTA wakiwashawishi wafanyakazi kugoma katika maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi za Mei mosi za mwaka huu.
“Nimesikia wakiwashawishi kugoma wakitutuhumu sisi kuwa ni serikali isiyoambilika, huo ni uongo na hawa viongozi wa TUCTA ni waongo, wanafiki…nilieleza katika hotuba yangu ya mwezi Machi jinsi serikali ilivyochukua hatua kuboresha maslahi ya wafanyakazi, na dhamira ya kuendelea kuwajali.
Endelea kusoma habari hii kwa undani...........
No comments:
Post a Comment