WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amesema uchunguzi
kuhusiana afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe bado
unaendelea na ni yeye atakayetangaza matokeo ya kama alipewa sumu au la
baada ya kukamilika huku akiikana ripoti iliyotolewa na Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna, Robert Manumba.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Nahodha kutoa tamko hilo tangu kuibuka kwa mjadala
kuhusu afya ya Dk Mwakyembe hasa baada ya DCI Manumba kuutangazia umma
kwamba ripoti kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaonyesha kuwa
Naibu Waziri huyo hakulishwa sumu, kauli ambayo ilipingwa na Waziri
mwenye dhamana ya Afya, Dk Haji Mponda na Dk Mwakyembe mwenyewe.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Nahodha
alisema uchunguzi kuhusu afya ya Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na hauwezi
kufanyika ndani ya wiki mbili au mwezi.
“Ninachosema ni kwamba
uchunguzi nilioutangaza bado unaendelea,” alisema na kuongeza: Sasa mimi
nimetangaza matokeo ya uchunguzi? Mimi ndiyo Waziri nasema uchunguzi
bado unaendelea na mimi ndiyo nitatangaza hitimisho la jambo hilo.”
Alisema
suala la Dk Mwakyembe ni zito na siyo la mtu kukurupuka kwani linagusa
hisia za watu na kutahadharisha baadhi ya watu wanaojaribu kulifanya
jepesi wanachezea kitu hatari.
“Ndiyo maana nasema ni jambo
linalohitaji weledi wa hali ya juu katika kulichunguza. Ni jambo zito la
kisayansi, naomba nipewe muda ili uchunguzi nilioagiza ufanyike kwa
kina. Nasisitiza ni jambo linalohitaji weledi wa kisayansi.”
Waziri
Nahodha alisema uchunguzi huo unafanyika kwa kuhusisha jopo la
wataalamu wa sayansi hivyo kuwataka Watanzania kutambua kwamba uchunguzi
huo unaendelea na ni vigumu kutamka utakamilika lini.
Kuhusu ripoti ya DCI
Alipoulizwa
ni kwa nini asimchukulie DCI Manumba hatua kwa kutoa tamko wakati
uchunguzi alioagiza haujakamilika alisema: “Ndiyo maana nasema,
uchunguzi wa suala hili unaendelea. Sasa hatima yote hayo unayozungumza
nasema nipeni muda.”
Alipoulizwa ni wapi DCI Manumba alipata
ripoti ya Dk Mwakyembe wakati mgonjwa mwenyewe na Waziri wa Afya
wameikana, alijibu: “Sasa, hilo ni vyema ukamtafuta yeye mwenyewe DCI
aseme. Mtafute aseme yeye na Waziri wa Afya, hao watu wawili wanaweza
kuzungumzia ripoti hiyo, lakini mimi nasema uchunguzi wa jambo hili la
Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na bado unaendelea.”
Alisema
alichokisema DCI Manumba kinaweza kuwa na msingi ambao anaujua mwenyewe
hivyo, ni vyema akaulizwa yeye kuhusu undani wa ripoti yake huku
akisisitiza: "Mimi ninavyoliangalia jambo hili la Dk Mwakyembe
linahitaji umakini wa hali ya juu katika kulishughulikia. Hilo la DCI
mtafute mwenyewe akueleze.”
Nahodha pia hakutaka kuzungumzia
suala hilo kwa undani hata pale alipoulizwa ikiwa haoni kwamba kukanwa
kwa kiwango hicho kikubwa kwa ripoti ya DCI Manumba kunawafanya wananchi
waanze kutilia shaka utendaji kazi wa jeshi la polisi.
Hata
hivyo, alipoulizwa jana kuhusu kukanwa kwa ripoti yake na mawaziri,
akiwemo wa Mambo ya Ndani ambayo ndiyo wizara mama inayosimamia Jeshi la
Polisi, DCI Manumba alisema kimsingi hawezi kujibizana na waziri yeyote
kwani kufanya hivyo itakuwa ni utovu wa nidhamu katika utumishi wa
umma.
Alisema alichokifanya ni kuandaa jalada ambalo tayari liko
kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambaye kwa mamlaka na utaalamu wake wa
kisheria, ataamua cha kufanya baada ya kulipitia.
“Siwezi
kujibizana na waziri wangu au waziri yeyote. Kama amesema uniulize mimi,
ninachoweza kusema ni kwamba tayari nimeandaa jalada liko kwa DPP. Sasa
nikianza kuzungumza hili au lile itakua haina maana watu watasema
nimeanza kujitetea,” alisema.
DCI, Dk Mwakyembe na Dk Mponda
Akizungumza
na waandishi wiki mbili zilizopita, DCI Manumba alisema: “Ukweli kuhusu
kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo nayo imewasiliana na hospitali
aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa
hakuna sumu.”
“Hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya jambo hilo, kwa sasa litashughulikiwa kwa kufuata misingi ya kisheria,” alisema Manumba.
Hata
hivyo, siku moja baada ya kauli hiyo ya DCI Manumba, Dk Mwakyembe
alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema: "Napata tabu kuamini kama
DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yangu au
walisoma taarifa ‘nyingine’ na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au
‘walisomewa!’
“Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba
kwa waandishi wa habari, hakifanani kabisa na picha iliyoko kwenye
taarifa halisi ya Hospitali ya Apollo inayotamka wazi kuwa kuna kitu
kwenye bone marrow (uboho) kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho
mabingwa wanahangaikia kukijua, kukidhibiti au kukiondoa huku vyombo
vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa
kisayansi wala aibu: “Hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu.”
Dk
Mwakyembe pia alitoa sababu kuu tatu za kupinga ripoti ya DCI Manumba:
“Kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina
kuhusu kiini chake, unaoendelea katika Hospitali ya Apollo, India ambako
bado sijahitimisha matibabu yangu, pili kwa ufinyu wa uelewa
unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa
‘sikunyweshwa sumu’ wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru,
inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu.
Tatu ni kitendo cha
Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima sasa,
halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali
na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.
Januari 19, mwaka huu
gazeti hili pia lilifanya mahojiano maalumu na Waziri Mponda ambaye naye
alisema kwa utaratibu, ripoti ya daktari ni ya mgonjwa... “Sisi
hatujaandika ripoti, muulizeni DCI Manumba awape ufafanuzi.”
Alisema
wanaoweza kuzungumzia maradhi ya Dk Mwakyembe ni familia yake au yeye
mwenyewe kwani ndiye mwenye ripoti. Lakini wizara haiwezi kufanya hivyo.
Chanzo: Mwananchi
Monday, February 27, 2012
Thursday, February 23, 2012
Wakristu watakiwa kujitakasa
WAKRISTO nchini wameonywa kuacha mzaha na Mungu kwa kujitokeza kwa wingi
katika siku maalumu tu za Jumatano ya Majivu na Ijumaa Kuu ili kubusu
msalaba kwani
kufanya hivyo ni kupoteza maana ya kipindi hicho cha toba.
Wametakiwa kujitokeza siku zote katika Misa na kuwa na muda binafsi wa kufanya toba, kufunga na kusaidia wahitaji ili kuleta maana ya kweli ya Kwaresima na Ukristo.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigirwa alisema hayojana
alipokuwa akihubiri katika Misa ya Jumatano ya Majivu kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam.
“Kuna msemo wa Kiswahili unasema mtu amekuja bila kitu duniani na ataondoka bila kitu,
mimi nasema si kweli, tumekuja bila kitu lakini tutaondoka na mizigo ya matendo yetu yawe
mema au mabaya, hilo lazima tujue, tusifunge kujiandaa kwa Pasaka bali kifo chema,” alisema Nzigirwa.
Kutokana na ukweli huo, aliwataka waumini kutofanya mzaha katika kipindi pekee cha
Kwaresima cha siku 40 akiwakumbusha wengine kuwa huenda ikawa Kwaresima ya mwisho katika maisha yao.
Kwa upande wake Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhashamu Method Kilaini
amewataka Wakristo kote nchini hasa Wakatoliki kujitenga na starehe kwa kujinyima ili kuwasaidia wahitaji.
Akizungumza na gazeti hili jana kwa simu, alisema Kwaresima ni kipindi pekee cha kujiweka karibu na Mungu kwa kuwasaidia yatima, wajane na wasiojiweza huku akiwataka
wanandoa, kuongeza ukaribu na upendo kwa familia.
Jumatano ya Majivu ni mwanzo wa kipindi cha Kwaresima cha siku 40 ambapo Wakristo kote duniani hupakwa majivu usoni na kukumbushwa kuwa binadamu ni mavumbi namavumbiniatarudiiliaishimaisha mema.
Chanzo: HabariLeo

Tuesday, February 21, 2012
Sugu, Ruge wamaliza bifu
KAMA ndoto vile, hatimaye lile ‘bifu’ la aina yake kati ya
mkongwe wa Bongo Fleva hapa nchini, Joseph Mbilinyi, ‘Mr II au Sugu’
ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), na Meneja wa Clouds,
Rugemalila Mutahaba, limemalizika.
Ugomvi huo wa Ruge na Sugu, ambao hivi karibuni ulizidi kushika kasi katika jamii, umefika ukingoni baada ya kumalizika kwa amani kwa pande zote mbili kufikia makubaliano, baada ya upatanishi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki, (CHADEMA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Dk. Nchimbi jijini Dar es Salaam jana, muafaka kati ya Sugu na Ruge ulitokana na usuluhuhishi ulioongozwa naye na Lissu.
Nchimbi alisema, katika upatanishi huo, pande zote ziliridhika kuwa, msingi wa mgogoro wao ni kila upande kuwa na kundi la wasanii na kuamini, upande mmoja hautendi haki kwa mwingine.
“Katika upatanishi huo, pande zote mbili ziliridhika kuwa, mgogoro huo unajenga uhasama wa wasanii nchini na utengano mkubwa miongoni mwa wasanii, ambao wanapaswa kuungana kudai na kusimamia masilahi yao,” alisema Waziri Nchimbi na kuongeza:.
“Hivyo basi, Mh. Joseph Mbilinyi na Rugemalila Mutahaba wanakubaliana kuwa wanamaliza mgogoro na uhasama baina yao kuanzia leo, wanashirikiana kufanikisha haki na jitihada ya kuinua masilahi ya wasanii, wanawaomba watu wote wanaowaunga mkono wamalize uhasama na kufungua ukurasa mpya na ushirikiano baina yao.
Pia kufanya jitihada ya pamoja ya kuunganisha vyama vya wasanii vya TUMA na TFU ili kutetea masilahi ya wasanii wakiwa na umoja zaidi,” alisisitiza Dk. Nchimbi.
Chanzo: Tanzania Daima

Sunday, February 19, 2012
Waziri amruka Manumba ripoti ugonjwa Mwakyembe
WINGU zito limetanda kuhusu afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison
Mwakyembe baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda,
kusema kuwa ripoti ya ugonjwa wa Mwakyembe, anayo mwenyewe na kwamba
wizara haina ripoti iliyotolewa na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert
Manumba, kwa waandishi wa habari.
Lakini wakati Dk Mponda akitoa kauli hiyo, baadhi ya watu wa kada tofauti wakiwamo viongozi wa dini na wasomi, wamekosoa ripoti hiyo ya polisi.
Mmoja wa watu hao, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa alisema,"hata mimi simwamini Manumba."
Malumbano hayo yanakuja wakati Dk Mwakyembe ambaye ni pia ni Mbunge wa Kyela, akitarajiwa nchini jana kwenda India kwa matibabu katika Hospitali ya Apollo.
Mahojiano na Waziri Mponda
Gazeti: Salaam Mheshimiwa waziri. Nimekupigia kutaka ufafanuzi kuhusu ripoti iliyotolewa na DCI Manumba kuhusu ugonjwa wa Dk Mwakyembe. Ninyi wizara mnaitambuaje?
Waziri: Kiutaratibu ripoti ya daktari ni ya mgonjwa. Sisi hatujaandika ripoti, muulizeni DCI Manumba awape ufafanuzi kama kuna kitu mnataka kuuliza zaidi kwa alichokizungumza na ninyi waandishi.
Gazeti: DCI Manumba alitoa taarifa kwa waandishi lakini aki-refer (rejea) ripoti kutoka wizarani (afya), baada ya kuwasiliana nanyi, kwa nini wewe usiizungumzie?
Waziri: Narudia tena, muulizeni yeye DCI au Dk Mwakyembe mwenyewe, wao wanaweza kuwapa ufafanuzi.
Gazeti: Tayari Dk Mwakyembe mwenyewe amekwishatoa tamko kwamba ripoti iliyosomwa na polisi, haina uhusiano na ripoti aliyokuwa nayo yeye kuhusu uchunguzi wa maradhi yake. Je, ripoti hii ya polisi ambayo wamedai wameipata kwenu (wizara) mmeitoa wapi?
Waziri: Ni hivi, baada ya daktari kumchunguza mgonjwa, hutoa ripoti na kumpa mgonjwa. Kwa hiyo, ripoti ya Hospitali ya Apollo anayo Dk Mwakyembe mwenyewe. Tena yeye kaeleza vizuri kabisa kwamba hata uchunguzi bado unaendelea. sasa hapo mnataka niseme nini tena?
Gazeti: Sasa kama ripoti anayo Dk Mwakyembe mwenyewe na tayari amesema ripoti ya polisi waliyosema imetoka kwenu siyo sahihi, je wizara iliwahi kupata ripoti ya Hospitali ya Apollo.
Waziri: Sisi tulichokifanya ni kumpa rufaa Dk Mwakyembe kwenda India. Ripoti hadi sasa anayo mwenyewe ingawa huwa tunapata taarifa baada ya yeye mgonjwa kuzileta kwetu. Hizo ndizo kanuni za taaluma ya udaktari, kwa hiyo ripoti anayo mwenyewe.
Gazeti: Sasa kama ripoti anayo Dk Mwakyembe mwenyewe, hii iliyosomwa na DCI imetoka wapi?
Waziri: Kumbuka DCI ana njia zake nyingi za kupata taarifa. Kwa hiyo ndiyo maana nasisitiza, muulizeni mwenyewe awape ufafanuzi kwa aliyozungumza na waandishi. Sisi wizara mnatuonea tu.
Gazeti: Lakini, hata kama ugonjwa ni siri, huoni mheshimiwa waziri kwamba kuna haja ya kuondoa utata kuhusu suala hili ikizingatiwa kuwa Dk Mwakyembe ni kiongozi anayegusa hisia za watu tofauti?
Waziri: Wanaoweza kuzungumzia maradhi yake, ni familia yake au yeye mwenyewe kwani ndiye mwenye ripoti. Mtafuteni au iulizeni familia yake iwapatie majibu. Lakini wizara haiwezi kufanya hivyo. Narudia tena, kuhusu hilo la DCI muulizeni mwenyewe awape ufafanuzi, mimi sijaona ripoti ya DCI aliyozungumza na waandishi wa habari.
Alichosema DCI
Akizungumza na waandishi mwishoni wa wiki iliyopita, Manumba alisema, “ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu."
Jana, alipoelezwa kwamba Dk Mwakyembe ameikana ripoti yao, Manumba alisema "sasa suala hilo litashughukiliwa kisheria."
Alisisitiza kuwa suala hilo litashughulikiwa kwa kufuata misingi ya kisheria na kwamba, Jeshi la Polisi haliko tayari kuendeleza malumbano kupitia vyombo vya habari.
"Hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya jambo hilo, kwa sasa litashughukiliwa kwa kufuata misingi ya kisheria kama nilivyokwishaeleza awali,"alisema Manumba.
Kauli ya Dk Mwakyembe
Juzi, akitoa tamko baada ya kukerwa na kauli ya Jeshi la Polisi alisema mbunge huyo alisema ‘napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yangu au walisoma taarifa “nyingine”, na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au “walisomewa”!
"Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa waandishi wa habari, hakifanani kabisa na picha iliyoko kwenye taarifa halisi ya Hospitali ya Apollo inayotamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua, kukidhibiti au kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala aibu: “hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu”
Dk Mwakyembe pia alitoa sababu kuu tatu za kupinga ripoti o ya DCI akisema:
"Kwanza, kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake, unaoendelea katika Hospitali ya Apollo, nchini India, ambako bado sijahitimisha matibabu yangu, pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa “sikunyweshwa sumu” wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu.
Alisema sababu ya tatu ni kitendo cha Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima sasa, halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.
Dk Slaa
Akizungumzia sakata hilo, Dk Slaa alisema hana imani na ripoti ya uchunguzi iliyofanywa na Jeshi la Polisi na kutolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, kuhusu hali ya Mwakyembe.
"Mimi siwezi kuzungumzia ugonjwa wa mtu, lakini niseme tu kwa kifupi kuwa ripoti ya DCI Manumba siwezi kuiamini. Sina imani na Manumba kwa sababu mimi mwenyewe imenitokea,"alirusha kombora kwa Manumba.
"Niliwekewa vipaza sauti kwenye kitanda changu mjini Dodoma, taarifa za tukio hilo zilifika kwake lakini hadi leo hajatoa majibu yoyote ya uchunguzi wake," alisisitiza.
"Nani asiyemfahamu Manumba ndiye alishuhudia watu 50 wakipoteza maisha kwa kufukiwa mgodini na kesi ikaenda mahakamani, ikafutwa, Kwa nini Serikali yetu inamweka mtu wa aina hiyo kwenye nafasi kubwa kama hiyo," alihoji Dk Slaa.
Alisema hata katika tukio la kuwekewa vinasa sauti kwenye kitanda huko Dodoma, hakuwahi kuitwa na kuhojiwa.
Askofu Ruwa'ich
Akizungumzia mvutano huo, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Yuda Thadeus Ruwa'ichi, alisema kinachoendelea kati ya jeshi na Dk Mwakyembe, ni ishara ya kutosha kuwa taifa liko kwenye ubabaishaji.
"Malumbano hayo yanaonyesha kuwa taifa liko kwenye ubabaishaji na hiki siyo kitu kizuri. Ushauri wangu turudi na kuwa wakweli, tufanye kazi kwa uadilifu,"alisema askofu Ruwa'ichi.
Rais huyo wa TEC, pia aliwataka waandishi wa habari kufanya uchunguzi wao na kutoa taarifa za kubaini ukweli kuhusu jambo hilo, ili kuondoa utata uliopo.
Jukwaa la katiba
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alielezea kushangazwa kwake juu ya nguvu aliyopata Manumba ya kupishana na mawaziri.
Alisema kinachotakiwa ni jopo la madaktari bingwa wa nchini, kuunda tume ili kuja na jibu litakalowawezesha wananchi waache kuihofia Serikali.
"Mabishano baina ya viongozi wa Kikwete (Rais), yanaonyesha dhahiri kwamba Serikali ina ulegevu, unaotokana na kiongozi wake mkuu kukaa kimya," alisema.
Kibamba alisema wakati umefika kwa Rais wa nchi kujitokeza hadharani na kuwawajibisha mawaziri, kama anaamini kuwa yanayoongelewa ni ya uwongo.
“Kilichoelezwa na Manumba hakiingii akilini kwa mwananchi wa kawaida, hii nchi sasa ni ya kisanii maana umegeuka mchezo wa Bongo land wa kuongea bila kuthitibishwa na madaktari bingwa,”alisema.
“Afya za mawaziri si suala la siri hasa ikizingatiwa kuwa wanatumia fedha za Watanzania katika kutibiwa . Kama kiongozi anataka kuweka siri aondoke kwenye uongozi atumie fedha zake,” alisisitiza.
“Siamini kama DCI Manumba ni daktari , kinachotakiwa ni kuundwa jopo la madaktari bingwa na Rais kuwaeleza Watanzania kinachowasibu viongozi wake,” aliongeza.
Alisema Watanzania wanaamini kuwa Dk Mwakyembe alilishwa sumu na kwamba ni vema Serikali ikaondoa mkanganyiko huo.
Akizumngumzia sakata hilo kwa njia ya simu, Mbunge wa Nyamagana, jijini Mwanza, Hezekiah Wenje alisema ni dhahiri kwamba kuna kitu ambacho Jeshi la Polisi linakificha.
“Hali halisi inaonyesha wazi kuwa kuna ukweli mwingi unaofichwa na Jeshi la Polisi na ndiyo maana kunakuwa na upotoshaji wa wazi,” alisema Wenje.
Mbunge huyo alisema kuna haja sasa ripoti ya madaktari kuwekwa wazi ili watu wajue.
Kwa upande wake, wakili wa kujitegemea mkoani Mwanza, Stephen Magoiga alisema Jeshi la Polisi, linaonyesha wazi kwamba lina matatizo makubwa ya kiutendaji linapotaka mlalamikaji kuwasilisha ushahidi.
Akikumbushia Dk Mwakyembe kudaiwa ushahidi alipopeleka malalamiko yake juu ya maisha yake kuwa hatarini, Magoiga alisema ushahidi ni suala la kitaalamu ambalo si mtu yoyote anaweza kukusanya.
“Jeshi la Polisi ndilo lenye utaalamu wa kukusanya ushahidi na wanalipwa kwa kazi hiyo, sasa wanapodai mlalamikaji alete ushahidi na baadaye kupingana na madai yake, ni dhahiri kwamba jeshi hilo linasema uwongo,” alisema Magoiga.
Alisema polisi wanapaswa kufanya kazi kisayansi kwa kuzingatia kwamba tuhuma za Dk Mwakyembe kulishwa sumu zimetolewa mara ya kwanza na mtu mzima mwenye hadhi yake katika jamii ya Kitanzania.
Alisema ni jambo la kushangaza kuona polisi wakioonyesha dharau za waziwazi kwa tuhuma zilizotolewa na mtu kama Waziri Samwel Sitta.
“Kama kauli ya Sitta inaweza kutendewa hivi na polisi je, ya mtu wa kawaida itakuwaje," aliohoji wakili huyo.
Ijumaa iliyopita Manumba alitoa tamko kuhusu kauli zilizowahi kutolewa na Sitta akiziita kuwa ni za uwongo na kuwataka watu wazipuuze.
Pia alitishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Waziri huyo wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Gaudence Mpangala, alisema mabishano yanayoendelea ndani ya Serikali, yanaonyesha kuwa kuna kitu kinachofichwa.
Profesa Mpangala alihoji kuhusu mahali ambako kumpa nguvu Manumba kuongelea afya ya Dk Mwakyembe.
Alisema kitendo hicho kinapingana na msimamo wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye aliwahi kukaririwa akisema Dk Mwakyembe ndiye anayepaswa kueleza hadharani maradhi yanayomsumbua.
Alisema Jeshi la Polisi limedharau kauli ya Pinda na kwamba hiyo inaonyesha kuwa Serikali, imekosa msemaji wa mwisho.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Musa Salim, alisema hatua ya viongozi kupishana inaonyesha kuwa hawafanyi kazi kwa umoja.
“Kilichoongelewa na Jeshi la Polisi ni sahihi kwa sababu limepewa jukumu la kuchunguza na kama kuna viongozi hao wanapinga majibu hayo, nadhani wanapaswa kuja na jibu,” alisema.
“Mimi sijui chochote lakini kama unachoeleza ni hivyo, maoni yangu ni kwamna tunatakiwa kuheshimu uchunguzi wa polisi ambao wamepewa dhamana ya kuchunguza,” alisema Sheikh Salim.
Historia ya ugonjwawa Mwakyembe
Dk Mwakymbe alianza kuumwa Oktoba 9 mwaka jana na baadaye kupelekwa India ambako alilazwa katika Hospitali ya Apollo kwa matatibu.
Alirejea nchini Desemba 11 mwaka jana, baada ya kulazwa hospitalini kwa takribani miezi miwili.
Msemaji wa familia ya Dk Mwekyembe ambaye ni Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa alisema mara baada ya mbunge huyo wa Kyela kuwasili nchini kuwa, afya yake ni nzuri na ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitalini.
Kauli za Waziri Sitta
Mara kadhaa Waziri Sitta amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisisitiza kuwa ugonjwa wa Dk Mwakyembe, umetokana na kulishwa sumu.
Akiwa kwenye uzinduzi wa Programu ya Neno la Hekima kutoka kwa kiongozi, iliyoanzishwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Jijini Dar es Salaam Januari 28 mwaka huu, Sitta alisema “ Dk Mwakyembe kapewa sumu, kama vyombo vya uchunguzi vinasema siyo, basi watueleze ukweli, tena haraka.”
“Ni vipi uone binadamu ambaye ukimshika katika ngozi unga unamwagika chini, mhudumu anakuja kuufagia, lakini baada ya saa moja unarudia tena, kitu hicho si cha kawaida,” alisisitiza Sitta.
Sitta alisema wamejaribu wameshindwa kwa kuwa Dk Mwakyembe analindwa kwa jina la Yesu ambalo ni kubwa kuliko yote.
Waziri Nahodha
Hata hivyo, akijibu moja ya kauli hizo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nohodha alimtaka Waziri Sitta awasilishe ushahidi wake ili ufanyiwe kazi badala ya kuzungumza nje ya vyombo vya sheria.
Lakini, Sitta alisema hatapeleka ushahidi kuhusu madai kwamba Dk Mwakyembe alilishwa sumu kwa kuwa polisi tayari wana ushahidi.
Alilaumu kuwa hata yeye aliwahi kupeleka tuhuma za kutaka kuawa lakini alipuuzwa.
Alisema inachotakiwa kufanywa na polisi ni uchunguzi kuhusu madai ya Dk Mwakyembe kulishwa sumu.
“Waziri Nahodha anataka ushahidi gani ikiwa taarifa za madaktari zinazomhusu Dk Mwakyembe kuhusu sumu aliyopewa zilishapelekwa polisi, anataka mimi nitoe ushahidi gani,” alisema Waziri Sitta.

Saturday, February 18, 2012
Mwakyembe awasha moto
SIKU moja baada ya Jeshi la Polisi kudai Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk
Harrison Mwakyembe hajalishwa sumu, kiongozi huyo ameibuka na kusema
amekerwa na jeshi hilo kutoa taarifa za uongo kwa wananchi ikiwa ni
pamoja na kuingilia utaratibu wa matibabu bila ya idhini yake.
Mwakyembe alifafanua kuwa sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, bali inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa na kusisitiza kuwa, aliwahi kulieleza jeshi hilo kwamba kuna kundi limejipanga kumdhuru, lakini lilifanya mzaha. Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyela, alisema tangu alipoanza kutumiwa ujumbe wa vitisho na wabaya wake aliowaita ni mafisadi mwanzoni mwa mwaka jana, alikuwa akitoa taarifa kwa jeshi hilo, lakini mpaka sasa limeshindwa kuwachukua hatua zozote.
Kauli hiyo ya Dk Mwakyembe inafuatia Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai(DCI), Robert Manumba kuwaeleza waandishi wa habari juzi kwamba wananchi wanatakiwa kupuuza madai yaliyotolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta kuwa Waziri Mwakyembe amelishwa sumu.
DCI Manumba alieleza kuwa waliwasiliana na Wizara ya Afya ili kubaini chanzo cha ugonjwa wa Naibu Waziri huyo, lakini taarifa iliyowasilishwa na wizara hiyo kwa Jeshi la Polisi imeonyesha kuwa, hajalishwa sumu. Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Mwakyembe alisema anapata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yake, au walisoma taarifa nyingine na kama waliisoma, taarifa hiyo wenyewe ama walisomewa.
Katika taarifa hiyo, alisema alichokisema DCI Manumba kwa waandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Hospitali ya Apollo ya nchini India anakotibiwa. “Ripoti inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow (ndani ya ute wa mifupa) kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua,” “Lakini vyombo vyetu vya dola vinapelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala aibu kwamba ‘sikulishwa sumu’, sikulishwa sumu,” alisema Mwakyembe katika taarifa hiyo.
Aliongeza kuwa,“Nimelazimika leo Jumamosi (jana) kutoa taarifa hii kwa vyombo vya habari kufuatia mkutano wa DCI Robert Manumba na waandishi wa habari uliofanyika jana (juzi) kuongelea, pamoja na mambo mengine, hali yangu ya afya na kuhitimisha, kienyejienyeji tu kuwa, “sikunyweshwa sumu”. Mwakyembe alisema taarifa hiyo ya DCI Manumba imeshindwa kufafanua ugonjwa wake wa ngozi umesababishwa na nini. Waziri huyo alisema msimamo huo wa Jeshi la Polisi umemkera katika hali aliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yake na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea Hospitali ya Apollo ambako bado anatibiwa.
Alisema kuna ufinyu wa uelewa uliojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi uliosisitiza kuwa ’hakunyweshwa sumu’ wakati sumu si lazima unyweshwe ili imdhuru mtu, bali inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa. Waziri huyo alisema kuwa ni hatari kwa Jeshi hilo kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.
Alifafanua kwamba Februari 9, mwaka jana, alimwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP) Said Mwema, kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yake na ya viongozi wengine. Alisema kuwa kwa kutambua kuwa Polisi wa Tanzania husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo wafanye kazi, alihakikisha ameainisha katika barua hiyo kila ushahidi alioupata au kupewa.
Hata hivyo, Dk Mwakyembe alisema anashangazwa na utaratibu unaotumiwa na Jeshi hilo wa kusubiri ushahidi mezani bila ya kuchunguza na kuwafananisha na mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani. Alisema utaratibu huo haupo popote duniani ila ni Tanzania peke yake, kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. “ Polisi duniani kote wanachohitaji ni kupata clue au tetesi tu. Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika,” Mwakyembe alisema katika taarifa hiyo. Naibu waziri huyo alisema pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi aliokuwa nao, yapo mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo.
Mambo manne Akifafanua mambo hayo katika taarifa hiyo, alisema siku chache baada ya kumkabidhi IGP Mwema barua hiyo, alitumiwa timu ya wapelelezi ofisini kwake ili kuchukua maelezo yake ya ziada. Alifafanua kuwa timu hiyo ilikuwa inaongozwa na Ofisa wa polisi ambaye wiki chache zilizopita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia dawa za kulevya mtoto wa mmoja wa wafanyabiashara maarufu nchini, suala alilodai kuwa mpaka sasa uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha.
Alisema kwa msingi huo, aliona ameletewa mtuhumiwa wa rushwa na ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi jambo ambalo haliwezekani na kwamba suala lake limefanyiwa mzaha. Mwakyembe alisema wiki chache baada ya barua yake kuwasilishwa kwa IGP na timu ya polisi kuanza kazi, Jeshi hilo likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari aliowatuhumu kushirikiana na majambazi. “Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza,”ilibainisha taarifa hiyo.
Alisema tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari, wale aliowatuhumu kwenye barua yake, walihamishiwa mikoa mingine. Mwakyembea alisema ili kumkatisha tamaa kabisa, barua yake ya ‘siri’ kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari iliyokebehi na kukanusha taarifa nzima aliyoitoa “Sijui kwa faida ya nani,” alihoji katika taarifa hiyo na kuongeza, “ Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa Jeshi la Polisi. Akitoa mfano wa Waziri Sitta, kuwa hivi karibuni, kiongozi huyo alihojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, lakini taarifa ya mahojiano ikaonekana kwenye moja ya magazeti, ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta na kubainisha kuwa uadilifu wa uongozi wa Jeshi la Polisi, umefikia pabaya.
Mwakyembe alisema, katika barua yake kwa IGP alieleza kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kumuua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wao. Waziri huyo alieleza kushangazwa na msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama alipewa sumu au la na kuamua kutoa tamko hata kabla ya kumchunguza alivyo.
Alisema polisi hawajawahi kumhoji yeye wala wasaidizi wake ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaomfanyia uchunguzi nchini India. Waziri huyo aliwashangaa polisi badala ya kumshukuru, Waziri Sitta kwa sababu amekuwa akiwapa tahadhari kuhusu afya yake ili suala hilo lichunguzwe kwa kina, badala yake sasa anaonekana adui wao. “Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam eneo la Mlimani na DCI Manumba.
Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa Sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua,” alilalamika katika taarifa yake hiyo. Alisema viongozi hao wanajua kuwa hawezi kukaa kimya au kumung’unya maneno pale anapoona haki inakanyagwa bila ya kujali matokeo ya uamuazi huo. Katika taarifa hiyo, Dk Mwakyembe aliwataka Watanzania kuombeana afya na uhai ili waweze kutenda haki na waendelee kuitetea nchi yao ikiwemo kumalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA na Kagoda kwa maslahi mapana ya Taifa. Historia ya ugonjwa wa Mwakyembe Dk Mwakymbe alianza kuumwa Oktoba 9 mwaka jana na baadaye kupelekwa nchini India na kulazwa katika Hospitali ya Apollo kwa matatibu. Alirejea nchini Desemba 11, mwaka jana baada ya kulazwa hospitalini humo kwa takribani miezi miwili.
Msemaji wa familia ya Dk Mwekyembe na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa, alisema baada ya mbunge huyo kurejea nchini, afya yake ni njema ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitali.
Kauli za Waziri Sitta Mara kadhaa Waziri Sitta amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisisitiza kuwa ugonjwa wa Dk Mwakyembe, umetokana na kulishwa sumu. Akiwa kwenye uzinduzi wa Programu ya Neno la Hekima kutoka kwa Kiongozi iliyoanzishwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, jijini Dar es Salaam Januari 28 mwaka huu, Sitta alisema:
“ Nasema Dk Mwakyembe kapewa sumu, kama vyombo vya uchunguzi vinasema siyo, basi watueleze ukweli, tena haraka,” alisisitiza Waziri Sitta katika hafla hiyo.
Sitta alihoji “ Ni vipi uone binadamu ambaye ukimshika katika ngozi unga unamwagika chini, mhudumu anakuja kuufagia, lakini baada ya saa moja unarudia tena, kitu hicho si cha kawaida.” Sitta alisema wamejaribu wameshindwa kwa kuwa Dk Mwakyembe analindwa kwa jina la Yesu ambalo ni kubwa kuliko yote.
Waziri Nahodha Akijibu moja ya kauli hizo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nohodha alimtaka Waziri Sitta awasilishe ushahidi wake ili ufanyiwe kazi badala ya kuzungumza nje ya vyombo vya sheria. Hata hivyo, Sitta alisema hatapeleka ushahidi wa madai aliyotoa kuwa Dk Mwakyembe alilishwa sumu kwa kuwa polisi tayari wanao ushahidi.
Alisema wanachotakiwa kufanya Polisi ni kufanya uchunguzi kuhusu madai hayo ya Dk Mwakyembe kulishwa sumu kwa kuwa ushahidi wanao na wasianze kurushiana mpira.
“Waziri Nahodha anataka ushahidi gani ikiwa taarifa za madaktari zinazomhusu Dk Mwakyembe kuhusu sumu aliyopewa zilishapelekwa polisi, anataka mimi nitoe ushahidi gani?” Alisema Waziri Sitta.
Source: Mwananchi

Thursday, February 16, 2012
Obama poised to win 2012 election with 303 electoral votes: The Signal Forecast
With fewer than nine months to go before Election
Day, The Signal predicts that Barack Obama will win the presidential
contest with 303 electoral votes to the Republican nominee's 235.
How do we know? We don't, of course. Campaigns and candidates evolve,
and elections are dynamic events with more variables than can
reasonably be distilled in an equation. But the data--based on a
prediction engine created by Yahoo! scientists--suggest a second term is
likely for the current president. This model does not use polls or
prediction markets to directly gauge what voters are thinking. Instead,
it forecasts the results of the Electoral College based on past
elections, economic indicators, measures of state ideology, presidential
approval ratings, incumbency, and a few other politically agnostic
factors.We'll dip into what the model says in a moment, but first a note about models in general: there are a lot of them, from complex equations generated by nerdy academics (like the team at The Signal) to funny coincidences like the Redskins Rule, which holds that the incumbent party keeps the White House if Washington's football team wins its last home game. (This is true in 17 of the last 18 elections!) Every year, some of these models are right and some are wrong, and the difference is often just luck. As a result, models get a bad rap as being very good at predicting the past and lousy at predicting the future.
But every election gives researchers more data to work with and a better idea of what works and what doesn't. Not all models are bogus just because many of them are. Our model combines powerful scientific algorithms with both real-time and historical data sources. We have examined the last 10 presidential elections and found that the Yahoo! model, which is the work of Yahoo Labs economists Patrick Hummel and David Rothschild, would have correctly predicted the winner in 88 percent of the 500 individual state elections.
The following chart shows our predictions for each state in the general election, based on this model.
Yahoo Signal election predictions
In addition to predicting winners, you'll see that the Yahoo! model predicts by how much each candidate will win each state. These estimates are, on average, under 3 percentage points off. (We exclude Washington, D.C., in the model and assume it will go for the Democratic candidate.)
The Yahoo! model assumes that the president's approval rating will stay the same between now and mid-June, that each of the 50 states will report personal income growth that is average for an election year, and that certain key indicators of state ideology will remain unchanged this year. Although the model currently predicts that Obama will win 303 electoral votes in November, please note that it predicts only probabilities of victory, and that many states are nearly toss-ups.
Because Mitt Romney has the lead in the delegate race for the Republican presidential nomination, for this table we assume that the Republican candidate's home state is Massachusetts and that the Republican candidate's home region is the East.
This may be a conservative estimate for Obama, because January's economic indicators suggest that the states are likely to experience greater-than-average income growth in the first quarter. We will update our predictions accordingly when the actual data from the current year is available.
A key finding of the model is that economic trends—whether things are getting better or worse than they were a month ago—are more meaningful than the level state of the economy. In other words, whether the unemployment rate is increasing or decreasing is more important than what the unemployment rate actually is.
Another lesson of this model is that, while campaigns and candidates matter, they don't matter all that much. Despite the varying quality and positions of the campaigns and candidates over the last 10 presidential elections, variables beyond their immediate control describe the outcome very well. A brilliant or lucky campaigner is at an advantage, but the net effect of politics and strategy, averaged over the past 40 years, is just the small variation that the Yahoo! model cannot predict.
In the following weeks, The Signal will have more posts that describe how the model was built and what its implications are. Rothschild is scheduled to give a talk on an academic paper that he and Hummel are writing on the Yahoo! model in May at the American Association for Public Opinion Research national convention.
Source: Yahoo News
Monday, February 13, 2012
Zambia wapokelewa kwa shangwe Lusaka
Mabingwa wapya wa soka wa Afrika, Chipolopolo wa Zambia wamepokelewa kwa shangwe katika mji mkuu Lusaka.
Mwandishi wa BBC anasema mashabiki waliokuwa wakisubiri, walilipuka kwa kelele za shangwe, wakati nahodha Christopher Katongo alipotoka kwenye ndege akiwa amelibeba Kombe la dhahabu la Mataifa ya Afrika.
Zambia waliwashinda Ivory Coast kwa mikwaju ya penati 8-7, katika mchezo wenye msisimko hasa baada ya dakika za kawaida na za nyongeza kumalizika.
Ushindi huu una umuhimu wa kipekee hasa kwa sababu miaka 19 iliyopita karibu kikosi kizima cha Zambia kiliteketea katika ajali ya ndege nchini Gabon.
Mwandishi wa BBC Mutuna Chanda anasema barabara ya kwenda uwanja wa ndege wa Lusaka imetapakaa rangi ya ijani, nyekundu, machungwa na nyeusi, huku maelfu ya mashabiki wakijipanga kutaka kuwaona wachezaji wakirejea rasmi.
Kutakuwa na sherehe katika viwanja vya wazi mjini Lusaka.
Kutuza
Takriban watu 1,000, wengi wao wakiwa wametembea kilomita 25, walikuwepo uwanjani kuwalaki wachezaji wa timu ya taifa.
Shughuli hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na rais wa zamani Rupiah Banda na Kenneth Kaunda, ambao wote ni mashabiki wakubwa wa kandanda.
Wananchi wengi wa Zambia wamejipa likizo hii leo ili kusherekea ushindi wa kwanza kabisa wa Zambia wa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Kikosi hiki kilichoibuka na ushindi, kiliondoka katika uwanja ule ule wa ndege wa Libreville, ambao ndege ya kijeshi iliongeza mafuta ikielekea Senegal kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwezi Machi 1993 - na ndege hiyo kuanguka muda mfupi baada ya kupaa.
Wachezaji wa Zambia, maarufu kama Chipolopolo Boys (yaani risasi za shaba), walitoa heshima zao kwa wachezaji 18 waliokufa katika ajali hiyo ya ndege - na kutuza ushindi huu kwa kikosi hicho kilichopotea.
Amani
"Wachezaji waliokufa katika ajali ya ndege nchini Gabon ndio walitupa hamasa, na nguvu katika michuano hiyo," amesema golikipa Kennedy Mweene akiwaambia waandishi wa habari kabla ya kuondoka Libreville.
"Hatukutaka kuondoka mikono mitupu," alisema.
Winga Felix Katongo aliwaambia waandishi wa habari: "Tulitaka kushinda kombe hili ili wananchi wa Zambia wajivunie na kwa wale waliokufa, kupumzika kwa amani. Sasa roho zao zitakuwa na amani."
Chanzo: BBC

Saturday, February 11, 2012
Whitney Houston, superstar of records, films, dies
LOS ANGELES
(AP)
–
Whitney Houston, who reigned as pop music's queen until her majestic voice and regal image were ravaged by drug use, has died. She was 48.
Publicist Kristen Foster said Saturday that the singer had died, but the cause and the location of her death were unknown.
At
her peak, Houston the golden girl of the music industry. From the
middle 1980s to the late 1990s, she was one of the world's best-selling
artists. She wowed audiences with effortless, powerful, and peerless
vocals that were rooted in the black church but made palatable to the
masses with a pop sheen.
Her success carried her beyond music to movies, where she starred in hits like The Bodyguard and Waiting to Exhale.
She
had the he perfect voice, and the perfect image: a gorgeous singer who
had sex appeal but was never overtly sexual, who maintained perfect
poise.
She influenced a generation of younger singers, from Christina Aguilera to Mariah Carey, who when she first came out sounded so much like Houston that many thought it was Houston.
But
by the end of her career, Houston became a stunning cautionary tale of
the toll of drug use. Her album sales plummeted and the hits stopped
coming; her once serene image was shattered by a wild demeanor and
bizarre public appearances. She confessed to abusing cocaine, marijuana
and pills, and her once pristine voice became raspy and hoarse, unable
to hit the high notes as she had during her prime.
"The
biggest devil is me. I'm either my best friend or my worst enemy,"
Houston told ABC's Diane Sawyer in an infamous 2002 interview with
then-husband Brown by her side.
It was a
tragic fall for a superstar who was one of the top-selling artists in
pop music history, with more than 55 million records sold in the United States alone.
She seemed to be born into greatness. She was the daughter of gospel singer Cissy Houston, the cousin of 1960s pop diva Dionne Warwick and the goddaughter of Aretha Franklin.
Houston first started singing in the church as a child. In her teens, she sang backup for Chaka Khan, Jermaine Jackson and others, in addition to modeling. It was around that time when music mogul Clive Davis first heard Houston perform.
"The time that I first saw her singing in her mother's act in a club … it was such a stunning impact," Davis told Good Morning America.
"To hear this young girl breathe such fire into this song. I mean, it really sent the proverbial tingles up my spine," he added.
Before
long, the rest of the country would feel it, too. Houston made her
album debut in 1985 with "Whitney Houston," which sold millions and
spawned hit after hit. Saving All My Love for You brought her her first Grammy, for best female pop vocal. How Will I Know, You Give Good Love and The Greatest Love of All also became hit singles.
Another multiplatinum album, "Whitney," came out in 1987 and included hits like Where Do Broken Hearts Go and I Wanna Dance With Somebody.
The New York Times
wrote that Houston "possesses one of her generation's most powerful
gospel-trained voices, but she eschews many of the churchier mannerisms
of her forerunners. She uses ornamental gospel phrasing only sparingly,
and instead of projecting an earthy, tearful vulnerability, communicates
cool self-assurance and strength, building pop ballads to majestic,
sustained peaks of intensity."
Her decision
not to follow the more soulful inflections of singers like Franklin drew
criticism by some who saw her as playing down her black roots to go pop
and reach white audiences. The criticism would become a constant
refrain through much of her career. She was even booed during the Soul
Train Awards" in 1989.
"Sometimes it gets down
to that, you know?" she told Katie Couric in 1996. "You're not black
enough for them. I don't know. You're not R&B enough. You're very
pop. The white audience has taken you away from them."
Some saw her 1992 marriage to former New Edition
member and soul crooner Bobby Brown as an attempt to refute those
critics. It seemed to be an odd union; she was seen as pop's pure
princess while he had a bad-boy image, and already had children of his
own. (The couple had a daughter, Bobbi Kristina, in 1993.) Over the
years, he would be arrested several times, on charges ranging from DUI to failure to pay child support.
But Houston said their true personalities were not as far apart as people may have believed.
"When
you love, you love. I mean, do you stop loving somebody because you
have different images? You know, Bobby and I basically come from the
same place," she told Rolling Stone in 1993. "You see somebody, and you
deal with their image, that's their image. It's part of them, it's not
the whole picture. I am not always in a sequined gown. I am nobody's
angel. I can get down and dirty. I can get raunchy."
It would take several years, however, for the public to see that side of Houston. Her moving 1991 rendition of The Star Spangled Banner at the Super Bowl, amid the first Gulf War, set a new standard and once again reaffirmed her as America's sweetheart.
In 1992, she became a star in the acting world with The Bodyguard. Despite mixed reviews, the story of a singer (Houston) guarded by a former Secret Service agent (Kevin Costner) was an international success.
It
also gave her perhaps her most memorable hit: a searing, stunning
rendition of Dolly Parton's "I Will Always Love You," which sat atop the
charts for weeks. It was Grammy's record of the year and best female
pop vocal, and the Bodyguard soundtrack was named album of the year.
She returned to the big screen in 1995-96 with Waiting to Exhale and The Preacher's Wife.
Both spawned soundtrack albums, and another hit studio album, "My Love
Is Your Love," in 1998, brought her a Grammy for best female R&B
vocal for the cut "It's Not Right But It's Okay."
But
during these career and personal highs, Houston was using drugs. In an
interview with Oprah Winfrey in 2010, she said by the time The Preacher's Wife
was released, "(doing drugs) was an everyday thing. … I would do my
work, but after I did my work, for a whole year or two, it was every
day. … I wasn't happy by that point in time. I was losing myself."
In
the interview, Houston blamed her rocky marriage to Brown, which
included a charge of domestic abuse against Brown in 1993. They divorced
in 2007.
Houston would go to rehab twice
before she would declare herself drug-free to Winfrey in 2010. But in
the interim, there were missed concert dates, a stop at an airport due
to drugs, and public meltdowns.
She was so startlingly thin during a 2001 Michael Jackson
tribute concert that rumors spread she had died the next day. Her crude
behavior and jittery appearance on Brown's reality show, Being Bobby Brown,
was an example of her sad decline. Her Sawyer interview, where she
declared "crack is whack," was often parodied. She dropped out of the
spotlight for a few years.
Houston staged what
seemed to be a successful comeback with the 2009 album "I Look To You."
The album debuted on the top of the charts, and would eventually go
platinum.
Things soon fell apart. A concert to promote the album on Good Morning America went awry as Houston's voice sounded ragged and off-key. She blamed an interview with Winfrey for straining her voice.
A
world tour launched overseas, however, only confirmed suspicions that
Houston had lost her treasured gift, as she failed to hit notes and left
many fans unimpressed; some walked out. Canceled concert dates raised
speculation that she may have been abusing drugs, but she denied those
claims and said she was in great shape, blaming illness for
cancellations.
Thursday, February 9, 2012
Wamarekani watafuta uwekezaji katika nishati
Rais Kikwete akiwa pamoja wageni kutoka Marekani |
Ujumbe huo wa wafanyabiashara uliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika, Johnnie Carson na ulifanya majadiliano na Rais kuhusu sekta ya nishati Tanzania na fursa mbalimbali za uwekezaji kwa kampuni za nishati kutoka Marekani.
Naibu Waziri Carson na ujumbe wake waliwasili jijini Dar es Salaam Februari 8, mwaka huu ikiwa ni sehemu ya ziara ya nchi nne zikiwamo Msumbiji, Nigeria na Ghana ili kuona fursa za uwekezaji hususan katika miradi ya uzalishaji umeme.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Ubalozi wa Marekani ilieleza kuwa ujumbe huo ulidhaminiwa pia na Baraza la Wafanyabiashara wa Marekani kwa Afrika (The Corporate Council on Africa) na unathibitisha dhamira ya dhati ya Serikali ya Marekani ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na Tanzania wakati huo huo ikitangaza fursa nyingi zilizopo hapa nchini.
"Ujumbe wa Naibu Waziri Carson unajumuisha wawakilishi wa Kampuni za Anadarko Petroleum, Caterpillar, Chevron, Energy International, General Electric, Pike Enterprises, Strategic Urban Development Alliance LLC, Symbion, na Zanbato Group,"ilieleza taarifa hiyo na kuongeza; "Wajumbe wengine wanaoiwakilisha Serikali ya Marekani ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa U.S. Export-Import Bank, Wanda Felton na viongozi wa Idara ya Rasilimali za Nishati ya Marekani."
Ilieeza kuwa juzi, ujumbe huo ulishiriki pia katika majadiliano na maofisa wa sekta ya nishati wa Serikali ya Tanzania na wa sekta binafsi yaliyofanyika katika Hoteli ya Serena na baada ya hapo unatarajiwa kukutana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO William Mhando.
Ubalozi huo katika taarifa yake umeeleza kuwa leo, ujumbe wa Naibu Waziri Carson utatembelea Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) ambako watakuwa na majadiliano na wawakilishi wa kituo hicho, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA). mwisho
Chanzo: Mwananchi
Saturday, February 4, 2012
Maghorofa Dar es Salaam yadaiwa kujengwa kwa fedha ‘chafu’
BAADHI ya maghorofa
yanayochipuka kama uyoga jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini,
yanatokana na shughuli za usafishaji wa fedha haramu.
Shughuli hiyo inafanyika kwa wafanyabiashara hao kuingiza fedha haramu kutoka nje ya nchi na kununua bidhaa na huduma na kuziuza kihalali nchini kwa muda kabla ya kuzibadilisha katika fedha za kigeni na kuondoka nazo.
Akichangia Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu wa Mwaka 2012 bungeni jana, Kabwe Zitto alidai hata upandaji holela wa bei za viwanja katikati ya miji umekuwa ukisababishwa na wafanyabiashara wa fedha chafu.
Alidai mabilioni ya fedha yalitoroshwa nchini kati ya mwaka 2000 hadi mwaka juzi kwa njia mbalimbali ambapo zinakadiriwa kufikia dola bilioni 2.9 za Marekani. Hali hiyo alidai inachangia pia upandaji holela wa bei za viwanja vya kujenga katikati ya miji hususan Dar es Salaam.
Alidai kuanguka kwa sarafu ya Tanzania kati ya Septemba na Novemba mwaka jana, ni matokeo ya shinikizo la wasafishaji hao wa fedha, ambao walinunua fedha nyingi za kigeni na kuondoka nazo. Muswada huo ambao ulisomwa kwa mara ya pili jana na kuanza kuchangiwa na Zitto kati ya wachangiaji sita walioruhusiwa kabla ya kuhitimishwa, umelenga kufanya marekebisho katika vifungu kadhaa na kutoa adhabu kali kwa wahusika.
Hata hivyo, pamoja na mchango wa Zitto, kambi rasmi ya upinzani katika hotuba yake, ilisema sifa ya Tanzania na nchi jirani kuwa wasafishaji wa fedha haramu inatokana na Taifa kutotumia sheria iliyotungwa mwaka 2006 inavyostahili. Kwenye hotuba hiyo iliyosomwa na Naibu Waziri wa Fedha Kivuli, Christina Mughwai, Upinzani ulihoji Serikali kutaka kufanya mabadiliko katika sheria ambayo haijaona utekelezaji wake.
Mwaka 2006, Bunge lilipitisha Muswada wa Sheria ya Kuzuia Fedha Haramu lakini haikutungiwa kanuni za utekelezaji. “Kwa mfano sheria iliyopo kifungu cha 23 (1) iliweka utaratibu wa fedha ambazo zinaingia na kutoka nje ya nchi, lakini la kustaajabisha, tangu wakati huo kwa kipindi cha miaka sita sasa, mipaka ya nchi imekuwa ‘wazi’ na fedha nyingi zinatoka bila kujulikana, kutokana na kukosekana kwa utekelezwaji wa kifungu hiki cha sheria,“ alisema Waziri Kivuli.
Alisisitiza, kwamba kifungu hicho kilimpa Waziri mwenye dhamana ya fedha, mamlaka ya kuamua ni kiasi gani cha fedha kinaweza kusafirishwa nje ya nchi kikiwa ni kiasi taslimu, ambacho mtu anapaswa kuwa nazo, lakini hakuna kilichofanyika mpaka sasa. Katika hotuba hiyo pamoja na kupendekeza kikomo cha fedha za kigeni anazoruhusiwa mtu kubeba zikiwa taslimu kuwa dola 10,000, walihoji kama kweli Serikali ina dhamira ya kutekeleza sheria hiyo.
Walidai kuwa hata kwenye mkutano wa Maseru (Lesotho), Serikali ilikataa kusaini mkataba wa fedha haramu kwa tuhuma kwamba Tanzania na Malawi ndizo zinatumika sana kusafisha fedha.
Mkutano huo wa Agosti 2009 ulikuwa na lengo la kuangalia namna bora za kukabiliana na fedha haramu ambazo zinatishia uchumi wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Upinzani pia ulizungumzia vifungu kadhaa vinavyotakiwa kubadilishwa na kusema vingine havina uhalisia.
Ulitolea mfano kifungu cha 28B kinachopendekeza adhabu ya jumla kwa mtu kuwa faini ya juu Sh milioni 500 na kiwango cha chini Sh milioni 100 au kifungo kisichozidi miaka mitatu jela, wakati kwa kampuni au taasisi kiwango cha adhabu ni kuwa faini isiyo chini ya Sh milioni 500 .
“Utaratibu huu wa kutoza faini ni dhahiri kuwa haukufikiwa kwa kuzingatia kigezo chochote kile, kwani haijabainisha kuwa ni kiwango gani cha fedha kitapaswa kulipiwa faini hiyo na hivyo kinaweza kutumika kama kishawishi katika kuvutia wahalifu na hasa kampuni kutumia mwanya huu kupitisha fedha nyingi haramu,“ alisema Mughwai.
Alisema Kambi ya Upinzani, inaona faini hizo haziko kiuhalisia, hivyo kutaka faini ziwekwe kwa kutumia asilimia ya fedha atakazotuhumiwa nazo na kiwango kiwekewe jedwali.
Muswada huo una marekebisho mbalimbali manane yaliyoombwa na Serikali yashughulikiwe, yakiwamo ya Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu, sura ya 423 ili iweze kutumika Tanzania Bara pekee na kurekebisha sheria ili kuwezesha Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) kujitegemea.

Wednesday, February 1, 2012
Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
Kwa
muda sasa nchi yetu imepitia kwenye tatizo kubwa la mgomo wa madaktari
katika hospitali nyingi hasa za umma ambao kwa kiasi kikubwa mgomo huo
umekuwa na madhara makubwa kwa watanzania masikini ambao ni wengi, kiasi
cha kugharimu hata maisha yao.
Chama
Cha Mapinduzi kinachukua nafasi hii kuwapa pole sana wale wote
walioathiriwa kwa namna moja ama nyingine na mgomo huu. Na kwakweli
tunasikitishwa sana na hali inayoendelea!
Chama
Cha Mapinduzi kinawapongeza na kuwashukuru madakitari walioonyesha
ubinadamu na uzalendo kwa kuamua kurudi kazini na ambao hawakugoma
kabisa. Tunawashukuru na kuwapongeza kwani hakuna masilahi yanayovuka
thamani ya uhai wa binadamu mwenzako!
Tunachukua
fursa hii pia kuwashukuru sana na kuwapongeza askari wetu wa jeshi la
wananchi wa Tanzania kwa uamuzi wao wa kizalendo wa kuamua kuitikia wito
wa serikali kwenda kwenye baadhi ya hospitali kusadia kuwatibu
watanzania wenzao. Moyo huu ni wa kizalendo na wa mfano. Tunajivunia
uzalendo wa jeshi letu!
Tunachukua
nafasi hii kuwaomba madaktari wanaoendelea na mgomo kurudi kazini huku
wakiendelea na mazungumzo na serikali. Tunaamini madai yao yanawezekana
kushughulikiwa ikiwa pande zote mbili zitaamua kukaa chini kwa dhati na
kuzungumza.
Serikali
kwa upande mmoja watafute kwa makini chanzo cha mgogoro huu na kutafuta
majibu, na madakitari nao kwa upande wa pili, wawe tayari kukaa mezani
na kuzungumza. Tunasisitiza thamani ya maisha ya binadamu ni kubwa
kuliko masilahi na madai wanayoyaomba!
Serikali
ni vizuri ikajenga utamaduni wa kushughulikia matatizo haya ambayo
yanaathiri wananchi wengi kwa uharaka na udharura unaostahili badala ya
kusubiri hali inapokuwa mbaya zaidi.
POSHO ZA WABUNGE
Kwa
upande mwingine Chama Cha Mapinduzi kinapenda kurudia wito kilioutoa
juu ya swala la posho za wabunge. CCM iliwaomba na kuwasihi wabunge na
mamlaka zinazohusika na mchakato wa swala hili kuliangalia upya na
kutumia busara, ikiwezekana kuachana nalo kwasasa.
CCM
inaupongeza na kuunga mkono msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kama ulivyonukuliwa na taarifa ya
Ikulu kwa vyombo vya habari, kuwa ni vizuri wabunge wakalitafakari upya
swala hili kwa masilahi mapana ya wale waliowapa dhamana ya
kuwawakilisha bungeni.
CCM
inaendelea kuwasihi waheshimiwa wabunge walitafakari upya swala hili na
busara itumike katika kuliamua huku wakifungua masikio kusikiliza sauti
za Watanzania kwani huko bungeni wana wawakilisha hawa Watanzania, ni
vizuri kusikiliza hiki kilio chao! Si busara kupuuza kilio cha waliokupa
dhamana ya kuwawakilisha.
Msimamo
wa Rais Kikwete kama sehemu moja ya mamlaka inayohusika na mchakato huo
ni uthibitisho wa usikivu wake kwa wananchi anaowaoongoza, yeye
katimiza wajibu wake, tunawasihi waheshimiwa wabunge wetu nao
walitafakari hili na kuona busara ya kuachana nalo kwasasa.
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM
Itikadi na Uenezi
Subscribe to:
Posts (Atom)