WAKRISTO nchini wameonywa kuacha mzaha na Mungu kwa kujitokeza kwa wingi
katika siku maalumu tu za Jumatano ya Majivu na Ijumaa Kuu ili kubusu
msalaba kwani
kufanya hivyo ni kupoteza maana ya kipindi hicho cha toba.
Wametakiwa kujitokeza siku zote katika Misa na kuwa na muda binafsi
wa kufanya toba, kufunga na kusaidia wahitaji ili kuleta maana ya kweli
ya Kwaresima na Ukristo.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigirwa alisema hayojana
alipokuwa akihubiri katika Misa ya Jumatano ya Majivu kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam.
“Kuna msemo wa Kiswahili unasema mtu amekuja bila kitu duniani na ataondoka bila kitu,
mimi nasema si kweli, tumekuja bila kitu lakini tutaondoka na mizigo ya matendo yetu yawe
mema au mabaya, hilo lazima tujue, tusifunge kujiandaa kwa Pasaka bali kifo chema,” alisema Nzigirwa.
Kutokana na ukweli huo, aliwataka waumini kutofanya mzaha katika kipindi pekee cha
Kwaresima cha siku 40 akiwakumbusha wengine kuwa huenda ikawa Kwaresima ya mwisho katika maisha yao.
Kwa upande wake Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhashamu Method Kilaini
amewataka Wakristo kote nchini hasa Wakatoliki kujitenga na starehe kwa kujinyima ili kuwasaidia wahitaji.
Akizungumza na gazeti hili jana kwa simu, alisema Kwaresima ni
kipindi pekee cha kujiweka karibu na Mungu kwa kuwasaidia yatima, wajane
na wasiojiweza huku akiwataka
wanandoa, kuongeza ukaribu na upendo kwa familia.
Jumatano ya Majivu ni mwanzo
wa kipindi cha Kwaresima cha siku
40 ambapo Wakristo kote duniani hupakwa majivu usoni na kukumbushwa
kuwa binadamu ni
mavumbi namavumbiniatarudiiliaishimaisha mema.
Chanzo: HabariLeo
Thursday, February 23, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment