Tuesday, February 21, 2012

Sugu, Ruge wamaliza bifu

Best Blogger Tips
KAMA ndoto vile, hatimaye lile ‘bifu’ la aina yake kati ya mkongwe wa Bongo Fleva hapa nchini, Joseph Mbilinyi, ‘Mr II au Sugu’ ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), na Meneja wa Clouds, Rugemalila Mutahaba, limemalizika.

Ugomvi huo wa Ruge na Sugu, ambao hivi karibuni ulizidi kushika kasi katika jamii, umefika ukingoni baada ya kumalizika kwa amani kwa pande zote mbili kufikia makubaliano, baada ya upatanishi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki, (CHADEMA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Dk. Nchimbi jijini Dar es Salaam jana, muafaka kati ya Sugu na Ruge ulitokana na usuluhuhishi ulioongozwa naye na Lissu.

Nchimbi alisema, katika upatanishi huo, pande zote ziliridhika kuwa, msingi wa mgogoro wao ni kila upande kuwa na kundi la wasanii na kuamini, upande mmoja hautendi haki kwa mwingine.

“Katika upatanishi huo, pande zote mbili ziliridhika kuwa, mgogoro huo unajenga uhasama wa wasanii nchini na utengano mkubwa miongoni mwa wasanii, ambao wanapaswa kuungana kudai na kusimamia masilahi yao,” alisema Waziri Nchimbi na kuongeza:.
“Hivyo basi, Mh. Joseph Mbilinyi na Rugemalila Mutahaba wanakubaliana kuwa wanamaliza mgogoro na uhasama baina yao kuanzia leo, wanashirikiana kufanikisha haki na jitihada ya kuinua masilahi ya wasanii, wanawaomba watu wote wanaowaunga mkono wamalize uhasama na kufungua ukurasa mpya na ushirikiano baina yao.

Pia kufanya jitihada ya pamoja ya kuunganisha vyama vya wasanii vya TUMA na TFU ili kutetea masilahi ya wasanii wakiwa na umoja zaidi,” alisisitiza Dk. Nchimbi.
Chanzo: Tanzania Daima

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits