Monday, April 23, 2012

Kortini kwa kumbaka mtoto wa kaka yake

Best Blogger Tips
MKAZI wa Kiluvya, wilaya ya Kinondni jijini Dar es Salaam, Mustafa Wachega (39), amefikishwa katika mahakama ya Kinondoni akikabiliwa na mashtaka ya kumbaka mtoto wa kaka yake.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi, Athuman Nyamlani, mwendesha mashtaka wa polisi, Magina Magoma, alidai kuwa Aprili 17 mwaka huu katika maeneo ya Manzese Tip top mshtakiwa anadaiwa kumbaka mtoto wa miaka 16 (jina linafadhiwa).

Mshtakiwa alikana shtaka hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti na kesi hiyo na itatajwa tena Mei 7.
Chanzo: Tanzania Daima

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits