Thursday, May 31, 2012

January Makamba awafunda wananchi

Best Blogger Tips
 NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bw. January Makamba amewataka wananchi wa Tarafa ya Mgwashi mkoani Tanga kutumia fursa mbalimbali ikiwemo kufanya biashara na Halmashauri mpya ya Bumbuli badala ya kuwaachia wageni waiuzie halmashauri hiyo hadi karatasi za ofisini.

Chanamoto hiyo aliitoa juzi wakati anahutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Mgwashi Kata ya Mgwashi wilayani Lushoto na kuwaeleza wananchi kuwa kwa kupata halmashauri ni ushindi mkubwa kwani pamoja na kufanya biashara, lakini pia huduma za jamii zitaboreka.

"Nitashangaa kama nitaona hata biashara ya kuuza karatasi (shajala) mtawaachia watu kutoka Arusha. Sasa ni wakati wenu kufanya biashara na Halmashauri ya Bumbuli kwa kuchukua zabuni mbalimbali ili kuinua vipato vyenu," alisema Bw. Makamba.

Bw. Makamba aliwatahadharisha wananchi wa tarafa hiyo kuwa uteuzi wa yeye kuwa Naibu Waziri hauwezi kumaliza changamoto zao bali ataendelea kupigana kama Mbunge kuona kero mbalimbali zikipatiwa ufumbuzi moja baada ya nyingine.

"Jamani mimi nilipokuja hapa niliomba kazi ya ubunge. lakini sio uwaziri, hivyo nafasi yangu ya unaibu Waziri hauwezi kumaliza kero na changamoto zenu, bali kama nilivyopigana kama mbunge wenu wa kupata umeme tangu dunia iumbwe kwenye Tarafa ya Mgwashi.

"Ndivyo nitakavyo hakikisha barabara ya kutoka Mbelei hadi Mashewa inatengenezwa huku ikihamishiwa kutoka halmashauri kwenda TANROADS (Wakala wa Barabara) ambayo itawezesha kusafirisha mazao yenu, lakini pia
tatizo la maji linakwisha," alisema Bw. Makamba.

Awali, Ofisa Tarafa ya Mgwashi Bw. Moka Urban alimueleza Bw. Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli kuwa Kituo cha Afya Mgwashi kinaletewa dawa kama kata badala ya kituo cha afya, hivyo kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Bw. Urban alisema pia barabara ya kutoka Soni hadi Mgwashi sio nzuri, umeme bado haujafika kwenye vijiji vingi pamoja na kufika makao makuu ya kata ya Mgwashi na baadhi ya vijiji havina mawasiliano ya simu.
Chanzo: Majira

Zitto afichua wizi wa silaha

Best Blogger Tips
 MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA), jana aligeuka mbogo na kuwafukuza watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Nchini (Tawiri) baada ya kubaini kupotea kwa silaha ambazo hadi sasa hazijulikani ziliko.

Zitto akiungwa mkono na wajumbe wa kamati hiyo, alisema kamati hiyo imepata hofu kubwa juu ya kutoweka kwa bunduki hizo, na zaidi baada ya kubainika kuwa moja ya silaha zinazoaminika kumilikiwa na taasisi hiyo kuhusishwa na tukio la mauaji mjini Mugumu, mkoani Mara.

Mbali na kuwafukuza watendaji wa taasisi hiyo, aliwaagiza kuwasilisha haraka ndani ya wiki mbili, ripoti kamili itakayoeleza kinagaubaga namna silaha hizo aina ya bunduki zilivyotoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu mwaka 1980.

Zitto alisema kuwa suala la upotevu wa silaha hizo, na nyingine kuhusika katika matukio ya kihalifu ni nyeti, na hivyo kamati hiyo ya Bunge inahitaji maelezo ya kina kutoka kwa watendaji hao, hivyo akawatimua, na kuwaagiza wawasilishe kwake ripoti ya kina mjini Dodoma wakati wa mkutano wa bajeti unaotazamiwa kuanza Juni 12, mwaka huu.

“Sisi kama kamati tumeamua kutoendelea kuijadili taarifa hii kutokana na kuwa na hofu na suala hilo kwani hivi sasa kuna taarifa ya silaha yenu namba 00980 ambayo inashikiliwa katika kituo cha polisi Mugumu tangu mwaka 1999 baada ya kudaiwa kutumika kwenye mauaji,” alisema Zitto.

Mwenyekiti huyo alishangazwa na kitendo kilichoonyeshwa na taasisi hiyo cha kushindwa kufuatilia zilipo silaha hizo jambo ambalo linatoa taswira kuwa zinaweza kuwa zinatumika katika uhalifu unaojitokeza nchini.

Alisema silaha hizo zinazomilikiwa na tawi la utafiti la Kingupira lililoko mbuga za wanyama za Serous ziligundulika kutokuwepo katika kituo hicho baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa mwaka 2008 na 2009.

Zitto alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida na inayotia mashaka, watendaji wa taasisi hiyo hadi sasa hawajatoa taarifa polisi kuhusu kutoonekana silaha hizo kwa kipindi chote hicho.

“Ninachofahamu ni kuwa kama silaha yako haionekani kitu cha kwanza ni lazima utaarifu vyombo vya dola …lakini ninyi wenzetu mmenyamaza kimya wala hamjawa na hofu na suala hilo,” alisema.
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora (CCM), alitaka kujua kwa nini baada ya mkaguzi kugundua suala hilo limechukua muda mrefu bila kushughulikiwa.

“Hivi mnafahamu unyeti wa suala hili? Mnajua kwa sasa nchi yetu iko katika wakati gani katika suala la uhalifu? Sio katika maeneo ya mijini tu bali hadi katika hifadhi zetu wanyama wengi wanauliwa hovyo. Inawezekana silaha hizo ndizo zinatumika,” alisema Lugora.

Akijitetea Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori, Paul Sarakikya, alisema kuwa hawajalipeleka suala hilo polisi kutokana na wizara kuanza kufanya uchunguzi.
Alimuomba mwenyekiti wa kamati hiyo kuwapa mwezi mmoja ili kukamilisha uchunguzi huo jambo ambalo halikuafikiwa.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Simon Mduma, alisema kuwa kutokana na uzito wa suala hilo Aprili mwaka huu walilazimika kuiandikia Wizara ya Maliasili na Utalii barua na kuhoji ziliko silaha hizo kwa kuwa hata katika vitabu vyao hakukua na taarifa zozote.
Chanzo: Tanzania Daima

Wednesday, May 30, 2012

Sabodo atoa rai ya ‘kubanana’ na ubadhirifu

Best Blogger Tips
Mustafa Sabodo
 MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mustafa Sabodo amewataka mawaziri kutembelea mashirika ya umma, idara, wakala na mamlaka za Serikali zilizo chini yao kwa kushitukiza.

Katika barua ya wazi aliyomuandikia Rais Jakaya Kikwete kwenye gazeti dada la Daily News jana, Sabodo alisema kazi hiyo ifanyike kila mwezi na baadaye kupeleka ripoti ya kila mwezi kwa rais.

Alisema tatizo la rushwa nchini si kubwa katika ngazi ya menejimenti ukilinganisha na idara, mashirika ya umma, wakala na mamlaka za Serikali.

Aidha, Sabodo amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhakikisha anatembelea kampuni ya madini kwa sababu yanaiibia nchi.

“Waziri wa Nishati na Madini lazima atembelee makampuni ya madini kwani yanatupora. Tafadhali pitia upya ripoti ya Mark Bomani,” ilisema sehemu ya barua hiyo ya Sabodo.

Pamoja na kuwataka mawaziri wote, lakini Sabodo pia ametilia mkazo kwa mawaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Profesa Anna Tibaijuka), wa Fedha (Dk. William Mgimwa) na wa Nishati na Madini kuhakikisha kila mwezi wanaripoti kwa rais na pia kutembelea kwa kushitukiza idara na mamlaka kama vile Mamlaka ya Mapato (TRA), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na zingine.

Akizungumzia hatua yake ya kukisaidia Chama cha Maendeleo na Demkorasia (CHADEMA), Sabodo ambaye ni kada wa CCM, alisema anafanya hiyo ili kukifanya chama hicho cha upinzani kuwa mwangalizi na kudhibiti matendo maovu ya baadhi ya watu, mawaziri, idara za Serikali ya chama tawala.

“Watu wanasema mimi ni mwanachama wa Chadema, kimsingi siyo, lakini ninakiunga mkono chama hicho kwa sababu ninataka kuwa mwangalizi na kudhibiti matendo mabovu ya baadhi ya watu, mawaziri, Idara za Serikali katika Serikali ya chama tawala,” alisema Sabodo.

“Mwaka 2004 nilishawahi kusema mpinzani si adui, ni mshirika na msaidizi muhimu katika kuleta maendeleo ya Taifa letu,” alisema na kuzungumzia fedha zake, akisema hana fedha haramu za kutoa misaada kwa jamii, na kwamba kipato chake kinatokana na kulipa kodi anazolipa nchini.

“Ukiachilia mbali kodi ninayolipa moja kwa moja Tanzania katika mamlaka husika, sioni ubaya wowote wa mtu kutumia kipato alichokipata nje kwa kushirikiana na masikini wa Tanzania,” alisema.

Aidha, Sabodo alisifu vitendo vya kibinadamu anavyovionesha Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa asiye na Wizara maalumu, Profesa Mark Mwandosya hasa kutokana na hatua ya kukataa kupewa msaada wa kuchimbiwa visima katika jimbo lake na kutaka vikachimbwe kwa watu wenye mahitaji zaidi.
Chanzo: HabariLeo

Tuesday, May 29, 2012

Jaribio la kumwondoa Papa lanukia Vatican

Best Blogger Tips
 TAARIFA za kuvuja kwa nyatraka za siri kutoka ofisi ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani zimeibua taswira mpya, wataalamu wakieleza kuwa zinaambatana na mchakato wa kuanza kumuandaa kiongozi mpya wa Kanisa hilo, atakayechukua nafasi ya kiongozi wa sasa, Papa Benedict XVI.

Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya kanisa hilo mjini Vatican, wameeleza kuwa hilo ni jaribio la kwanza la kumwondoa madarakani Papa Benedict XVI.

Nyaraka hizo za siri ambazo zimepewa jina la "Vatileaks" zimesababisha kashfa mpya katika kanisa hilo, zikifichua mpango wa kumwondoa madarakani, Tarcisio Bertone, Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican ambaye anaonekana kuwa na sauti na madaraka makubwa, kiasi cha kwenda kinyume na maadili ya kanisa hilo.

Huku Vatican ikiendelea kusafisha waovu na wanaovujisha nyaraka hizo kutoka dawati binafsi la Papa Benedict XVI, uvumi umezagaa kwamba mzozo huo unazidi kutanuka na kwa sasa ni vigumu kuuzima.

Kanisa Katoliki limekuwa na rekodi mbaya ya kuzima kashfa ambazo zimewahi kulikumba kama vile za utakatishaji fedha, udhalilishaji watoto na kashfa ya sasa inaweza kuanzisha mchakato wa kusaka Papa mpya.

"Kundi la makadinali kadhaa katika Vatican limeanza kwa siri mchakato wa kumwondoa  Waziri wa Mambo ya Nje, kufikiria pia mchakato wa kusaka mrithi wa Papa (conclave) wakiangalia ni nani anafaa miongoni mwao," limeeleza gazeti  La Repubblica la Italia.

"Nyaraka hizo zilizovujishwa zinamhusisha Kardinali Bertone kwa njia moja au nyingine," anaeleza Marco Politi, mtaalam wa masuala ya Vatican wakati akizungumza na Shirika la Habari la AFP.

"Huu ni mpango wa kumwondoa na kuweka waziri mwingine," ameongeza mtaalam huyo.

Bertone, ambaye ni mshirika na rafiki wa karibu wa Papa Benedict XVI, amezusha mijadala mkali hasa kuhusu uendeshaji wa benki ya Vatican, jambo ambalo limetia doa uongozi wa kanisa hilo.

Nyaraka hizo zimefichua siri nyingi za Vatican, zikiwamo za matatizo ya ulipaji kodi, udhalilishaji wa kijinsia wa watoto na majadiliano na makundi ya waasi wenye msimamo mkali ndani ya kanisa hilo.

Ingawa nyaraka hizo hazitoi habari za kushtua wala kushangaza, zimefungua ‘dirisha la sumu’ ambayo imekuwa ikisambaa miongoni mwa watendaji wa Vatican.

Taarifa hizo ambazo zilivuja Januari mwaka huu zinaonyesha kuwapo kwa mzozo mkubwa baina ya Bertone na Askofu Mkuu Carlo Maria Vigano, ambaye amekuwa akijaribu kusafisha hesabu za Vatican, kiasi cha kuondolewa ikidaiwa kwamba ni kutokana na kupambana na maovu.

Askofu Vigano alimwandikia barua Papa Benedict na kuomba asiadhibiwe kwa kuondoa waovu na wale waliohusika na matumizi mabaya ya fedha za Vatican ambazo zimesababisha benki inayomilikiwa na kanisa hilo kupoteza mamilioni ya euro kwa kuingia mikataba mibaya, lakini hakufanikiwa.

Watu walio karibu na Vatican wanamtuhumu Papa Benedict XVI kwa kutokuwa thabiti na kukosa nguvu za kupingana na uamuzi wa Bertone.

"Risasi hizi zinamlenga Bertone. Zinalenga kumwangusha na kumzamisha, kwa lengo la kutaka ajiuzulu," alieleza mtaalam wa theolojia wa Italia, Vito Mancuso akizungumza na wanahabari wiki jana.

Kardinali huyo mwenye umri wa miaka 78, pia anatuhumiwa kwa kulazimisha benki ya Vatican kumtimua kazi mkuu wake, Ettore Gotti Tedeschi,  ambaye ni mtaalam wa masuala ya fedha kwa kushindwa kufuata maagizo.

Gotti Tedeschi alikabidhiwa jukumu la kusafisha Vatican na kuirejesha katika nchi zenye vitabu safi vya hesabu, lakini alishindwa baada ya Bertone kusisitiza kwamba benki hiyo inao uhuru wa kujiendesha, bila kuingiliwa.

"Bertone ana madaraka makubwa. Tunatakiwa kuondoa uoza ndani ya kanisa," alieleza mmoja wa maofisa wa Vatican akizungumza na gazeti la La Repubblica. "Wale wanaovuisha siri, wanafanya hivyo kwa maagizo ya papa," kilieleza chanzo hicho.

Mzozo huo uliingia sura mpya baada ya Vatican kutishia kumshitaki mwandishi wa habari Gianluigi Nuzzi  kwa kitabu chake kipya "His Holiness", ambacho kimeandikwa kwa kutumia nyaraka hizo zilizovujishwa.

Kama njia ya kuzuia kuvuja zaidi kwa nyaraka hizo, Msaidizi wa Papa Benedict, Paolo Gabriele amekamatwa kwa tuhuma za kuvujisha nyaraka hizo na amekuwa akihojiwa na watu wengine walioko karibu na Papa.

Uvumi umezagaa kuhusu watu 20 ambao wamekuwa wakivujisha siri hizo kwa vyombo vya habari, huku wawili kati yao ambao wamezungumza kwa masharti ya kutotajwa wakieleza kwamba Vatican imechafuka haiwezi kujisafisha.

"Kitu dhahiri ni kwamba Tarcisio Bertone hawezi kujiondoa katika kashafa hii kwa sasa," alieleza mtaalamu wa masuala ya Vatican, Sandro Magister.

"Hawezi kupona, kuna kila dalili kwamba papa atachukua uamuzi wa kumwondoa na kumweka mwingine katika muda mfupi ujao."

Kulingana na mtaalam mwingine, Bruno Bartoloni, siri hizo za "Vatileaks" ni kashfa ambayo inakamilisha miongo ya utawala mbovu na rushwa unaoitesa Vatican.
Chanzo: Mwananchi

Monday, May 28, 2012

Umri wa Lulu bado utata

Best Blogger Tips
 MAWAKILI wa Serikali katika kesi ya mauaji inayomkabili mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, wamepinga maombi ya mawakili wa mshitakiwa huyo kutaka umri wake uchunguzwe.

Maombi hayo yalipangwa kusikilizwa jana mahakamani hapo mbele ya Jaji Fauz Twaib, lakini kabla ya kusikilizwa, mawakili wa Serikali walidai kuwa na pingamizi la kusikilizwa maombi hayo.

Awali kabla ya pingamizi hilo, mawakili wanaomtetea Lulu waliiomba Mahakama Kuu ichunguze umri wa msanii huyo au kuiamuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ifanye hivyo.

Lakini Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro aliiomba Mahakama hiyo isisikilize maombi ya Lulu kwa madai kwamba yaliwasilishwa mahakamani hapo kimakosa, huku pia sheria iliyotumika ina kasoro.

Sheria iliyotumiwa na mawakili wa utetezi ni Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, kifungu cha 113 inayoruhusu Mahakama kufanya uchunguzi wa umri wa mshitakiwa.

Kimaro alidai kuwa maombi hayo yalikwishatolewa katika Mahakama ya Kisutu na ‘kugonga mwamba’ na kuongeza kuwa mawakili wa utetezi walitakiwa kuukatia rufaa uamuzi huo au kuomba mapitio yake, lakini si kuwasilisha maombi mapya.

Vile vile Kimaro aliyekuwa akisaidiwa na Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda, alidai kuwa maombi ya pili kwa Mahakama hiyo ya kusitisha kesi ya Kisutu ni batili.

Alidai ubatili huo ni kwa sababu kesi ya Lulu Kisutu haisikilizwi, iko katika hatua ya uchunguzi na sheria inataka kesi kusimama ikiwa katika hatua ya kusikilizwa.

Hata hivyo mawakili wa Lulu, Peter Kibatala, Fulgence Masawe na Kennedy Fungamtama na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Joaquine De- Melo aliyetambulishwa kama mtazamaji, walipinga.

Mawakili hao walidai kuwa waliwasilisha maombi yao mahakamani hapo kutokana na uamuzi wa Mahakama ya Kisutu uliotamka kama kuna maombi yoyote yawasilishwe katika Mahakama hiyo.

Walidai kuwa Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kutoa uamuzi wa maombi yao kwa mujibu wa sheria na hakuna walipokosea na kuiomba Mahakama ipuuze maombi ya mawakili wa Serikali.

Baada ya kusikiliza maombi hayo, Jaji Twaib alisema ni vema apate muda wa kutoa uamuzi kwa sababu ana safari na kupanga kutoa uamuzi huo Juni 16.

Lulu jana alionekana mchangamfu akiashiria kuanza kuzoea maisha hayo tofauti na siku za awali, alipokuwa mnyonge mahakamani na wakati mwingine akilia.

Lulu anadaiwa kufanya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba. Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na itatajwa tena Juni 4 mwaka huu.
Chanzo: HabariLeo

Nchimbi aonya vurugu Zanzibar

Best Blogger Tips
 WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kumkamata mtu yeyote atakayechochea fujo na vurugu visiwani hapa bila kujali wadhifa wake.

Akizungumza na viongozi mbalimbali wakiwemo wanajumuia za maimamu (Jumaza) pamoja na mwakilishi wa mabalozi katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani Kilimani, katika mkutano uliohudhuriwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Saidi Mwema, Nchimbi alisema Watanzania wanahitaji amani ambayo inatakiwa kulindwa na kila Mtanzania.

Nchimbi ambaye alidai kuridhishwa na kurejea kwa utulivu katika viunga vya mji huu, alisema serikali haiwezi kamwe kunyamaza na kuwaachia watu wachache wakivuruga amani na kuhatarisha usalama wa wengi.

Bila kutafuna maneno, waziri huyo alikiri kutofurahishwa kwake na mwenendo mzima wa kikundi cha Uamsho kinachotuhumiwa kushiriki vurugu kubwa zilizozuka kwa siku mbili zilizopita.

Alisema jumuia hiyo, ambayo kwa karibu mwaka mzima imekuwa ikiitwa na kuonywa na polisi dhidi ya matamshi mbalimbali yaliyolenga kuwagawa Watanzania, lakini mara tu inapotoka katika meza ya mazungumzo hurejea tena kuhubiri yaleyale, jambo alilosema sio la kiungwana.

“Hata katika mikutano na maandamano ya juzi walikuwa na haki ya kufanya maandamano, na walitakiwa kuomba kibali na kupatiwa ulinzi, jambo ambalo hawakulifanya,” alisema.

Aliwaomba viongozi wa serikali kushirikiana na kuona wananchi wanarudi katika hali yao ya zamani na kusisitiza jeshi kutosita kuchukua hatua kwa yeyote atakayevunja sheria.

Naye sheikh kutoka msikiti wa Amir Tajo, Omar Mohamed Ali, alimtaka waziri huyo kuangalia kanda za jumuia za Uamsho na kuona kama kuna uvunjifu wa amani, na kudai kuwa juzi walifanya matembezi ya hiyari bila kudhuru mtu, ambapo polisi walikuwa na habari ya matembezi hayo na badala yake, walimchukua sheikh wao kwa njia ya kumteka nyara hali iliyozua hisia tofauti kwa wananchi.

Katika hatua nyingine watu 30 wakiwemo viongozi watatu wa jumuiya ya Uamsho akiwemo Mussa Juma Issa wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe wakikabiliwa na tuhuma ya kukusanyika na kuandamana bila kibali na kufanya fujo.

Viongozi na watu hao hata hivyo, wameachiwa kwa dhamana ambapo upelekezi wa kesi hiyo bado unaendelea.

Vurugu kubwa zilizuka juzi mjini hapa ambapo, kundi la watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa Uamsho walifanya ghasia kubwa ikiwemo kuchoma magari, kushambulia nyumba ambapo kanisa moja la T.A.G Kariakoo lilichomwa moto na kuharibiwa vibaya ikiwa ni pamoja na magari ya watu.
Aidha katika vurugu hizo inadaiwa kwamba watu wasiofahamika walianza kusaka nyumba wanazoishi watu kutoka Tanzania Bara wakitishia kuwaua.

Marekani yahuzunika
Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, ameeleza kusikitishwa kwake na vurugu zilizozuka mjini hapa na amewataka viongozi wa makundi yote kuhakikisha kuwa wanasimamia amani na utulivu kwa nguvu zote.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, balozi huyo alisema vurugu hizo zimetia doa amani, umoja na mshikamano ambao umekuwepo tangu uchaguzi mkuu uliyopita, na kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Amesema ni vema kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kulinda amani kwa kuwa ghasia hizo zitaleta athari kwa uchumi wa nchi na kuwaogopesha watalii na wawekezaji wa kigeni kuingia nchini.

Uamsho yakana kuchoma kanisa
Katika hatua nyingine, Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), imepinga kuhusika kuhamasisha kufanya machafuko yaliyotokea mji wa Zanzibar usiku wa Mei 26 na kusababisha kuchomwa moto kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) la Kariakoo ikiwa ni pamoja na kuharibu magari, miundo mbinu na mali nyingine.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari imesema, “Kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshima zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukumu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (makanisa, mahekalu na sehemu nyingine za ibada) zisivunjwe wala zisiharibiwe.”

Jumuia hiyo ilitoa wito kwa Waislamu na Wazanzibar wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu.

Taarifa hiyo ilibainisha kwamba matukio hayo wanayachukulia kama njama za makusudi za wale wasioipendelea amani ya nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.

“Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na vyombo vyote vya dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa polisi na vikosi vingine kwani wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu,” ilisema taarifa hiyo.
Chanzo: Tanzania Daima

30 waachiliwa kwa dhamana Zanzibar

Best Blogger Tips
 Viongozi wawili wa kundi la Uamsho waliokuwa wanashikiliwa na polisi wa Zanzibar kwa zaidi ya siku mbili pamoja na baadhi ya wafuasi wao wameachiwa kwa dhamana katika mahakama ya Mwanakwerekwe huko mjini Zanzibar.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo ya kisiasa, kuachiwa kwa viongozi hao ambao walikuwa wanakabiliwa na kosa la kuandamana bila kibali kunaweza kukomesha uhasama wa takriban siku mbili baina ya wafuasi wa kundi hilo na polisi.

Mwandishi wetu Aboubakar Famau aliyekuwa Zanzibar anasema hali ilianza kuwa shwari mjini Zanzibar baada ya kuachiliwa kwa dhamana kwa wafuasi takriban thalathini wa kundi la Uamsho waliokuwa wanashikiliwa na polisi mjini humo kwa tuhuma za kuandamana bila kibali.

Miongoni mwa waliopata dhamana hiyo ni Sheikh Mbaruku Saidi Khalfan na Musa Juma Musa wote wakiwa viongozi wa kundi hilo ambao kukamatwa kwao kumeleta kizazaa mjini humo.

Mbele ya Hakimu wa mahakama ya Mwanakwerekwe majira ya saa nne asubuhi Jumatatu, baada ya kusomewa mashtaka ya kufanya mkusanyika haramu katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, watuhumiwa hao kwa pamoja walikana tuhuma hizo.

Baadaye wakili wa watuhumiwa hao aliwaombea dhamana, ombi ambalo lilikubaliwa bila pingamizi lolote.

Kukamatwa kwa viongozi hawa kumeleta sokomoto kubwa mjini Unguja hasa baada ya wafuasi wa kundihilokuamua kuandamana kwa lengo la kuishinikiza polisi kuwaachia.

Hali iliyosababisha vuta nikuvute baina ya wafuasi hao na polisi ambao wamekuwa wakitumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.

Uamsho ni kundi la kidini ambalo limejipa jukumu la kuwaelimisha wazanzibari kuhusu suala la muungano hasa wanapotoa maoniyaokatika Tume ambayo inakusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Hata hivyo, taarifa zisizothibitishwa zinasema, kundihilolimejikita zaidi katika kuwahamasisha wananchi kuupinga muungano.
Chanzo: BBC

Friday, May 25, 2012

Britney Spears Having "Incredible Time" at X Factor Auditions

Best Blogger Tips
 As we told you yesterday, new judges Britney Spears and Demi Lovato settled into their seats next to Simon Cowell and L.A. Reid without any hiccups (no, Spears didn't storm off the stage!).

"I am having the most incredible time and love being able to sit next to Simon at the judging table," Spears exclusively tells E!. "The talent has been tremendous."

So, is the second day of auditions in Austin going as smoothly as the first?
Before we get to that, we've gotta tell you what Spears' fiancé Jason Trawick gave her last night.


After yesterday's long day, the 30-year-old pop star went back to her hotel to relax for day two of auditions. Spears and Trawick enjoyed dinner before they ended the night with Trawick giving his gal—get ready for it!—a foot massage, according to a source.

What a guy!

As for today, according to a fan on Twitter, at one point during today's round of auditions a contestant teased BritBrit by announcing, "I work at Britney's favorite coffee shop!" The crowd replied, "Starbucks!" which caused the coffee-loving songstress to smile and laugh.

Spears, dressed in the same dress as yesterday for taping continuity, wasn't amused by every one of today's hopefuls, however. Another audience member tweeted, "Britney: 'i wanna know who [let] u on stage, i feel uncomfortable with you looking at me.'"
Source: Eonline



CHADEMA kuwasha moto Jangwani leo

Best Blogger Tips
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kitafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Wilbord Slaa watahutubia.

Aidha, viongozi wengine wakiwemo wabunge wake 15 ni miongoni mwa watakaoshiriki mkutano huo, akiwemo Mbunge wa Ubungo John Mnyika ambaye juzi, alitangazwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa mbunge halali baada ya kushinda kesi ya kupinga ushindi wake, iliyokuwa ikimkabili.

Joto la mkutano huo limepanda kiasi kwamba, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetangaza kuweka ulinzi mkali.

Taarifa ya CHADEMA jana imesema kuwa, ingawa Mahakama Kuu imewapatia ushindi wabunge wake, Tundu Lissu, John Mnyika, Gervas Mbasa na wengine waliopingwa, leo katika mkutano huo itaeleza umuhimu wa mabadiliko ya kimfumo katika mhimili huo, na katika utendaji kazi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), ambayo chama hicho kinataka iwe chombo huru katika kutekeleza majukumu yake nyeti mbalimbali, ikiwemo kusimamia uchaguzi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, alidai kunahitajika mabadiliko ya kimfumo kwa sababu kumekuwa na athari kubwa katika maendeleo ya wananchi, na pia kikwazo cha kuweka madaraka ya uendeshaji wa nchi mikononi mwa umma kama inavyotamkwa katika ibara ya 8 ya katiba ya sasa.

“Tunataka wananchi wajitokeze kwa wingi kusikiliza masuala mbalimbali, zikiwemo hoja juu ya umuhimu wa kufanya mabadiliko ya kimfumo kupitia uandikwaji wa katiba mpya, waje wajue namna ambavyo ubovu wa katiba ya sasa umechangia kwa kiasi kikubwa matatizo makubwa yanayotukabili kama taifa, ikiwemo umaskini, ujinga, maradhi, ufisadi na CCM yenyewe,” alisema Mnyika.

Alidai kuwa katika mkutano huo, watazindua kampeni ya ‘kuiamsha Dar es Salaam’, ikiwemo kaulimbiu ya ‘Vua Gamba, Vaa Gwanda’ inayotarajiwa kuwapokea viongozi na wanachama wengi kutoka CCM.

Aliongeza kuwa, tofauti na CCM ambayo imeanza mchakato wa katiba kwa kujifungia na kutoa misimamo ya mamlaka za chama bila hata maoni ya wanachama wake nchi nzima, CHADEMA itatumia fursa hiyo kutoa elimu ya uraia kwa umma juu ya sheria ya mabadiliko ya katiba, ili kuwezesha umma kumiliki mchakato na hivyo taifa lipate katiba bora.

Mbali na Mnyika, wabunge wengine watakaoonekana leo ni pamoja na Peter Msigwa, Ezekiah Wenje, Tundu Lissu, Grace Kiwelu, Halima Mdee, Rose Kamili, Mhonga Said, Suzan Kiwanga, Joyce Mkya, Godbless Lema na Meya wa Manispaa ya Musoma, Alex Malima Kasurula.

MVUTANO POLISI, CHADEMA
Hata hivyo, pamoja na Jeshi la Polisi kuruhusu kufanyika kwa mkutano huo, kumezuka mvutano kati ya pande hizo mbili kuhusu suala la wanachama kufanya matembezi ya hiyari kutoka kila kona ya Jiji la Dar es Salaam kuelekea Jangwani.

Wakati CHADEMA wakitangaza ramani yatakapopita matembezi hayo, polisi imeyapiga marufuku kwa madai kwamba hakuna sheria yoyote inayoruhusu chama cha siasa kufanya matembezi au maandamano.

Awali, CHADEMA ilituma maombi ya maandishi kwa Jeshi la Polisi kuruhusu matembezi hayo ya amani, kutoka sehemu mbalimbali za jiji hadi viwanja vya Jangwani panapofanyika mkutano wa hadhara leo.

Lakini jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema, wanaruhusu kufanyika kwa mkutano huo, na wamejiandaa kikamilifu katika ulinzi, lakini si kwa matembezi.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, CHADEMA iliwasilisha barua ya kuomba kibali cha kufanya mkutano, lakini kabla ya kujibiwa, kilipeleka barua nyingine yenye lengo la kupewa kibali cha matembezi ya amani.

Kova alidai kuwa, mwanachama yeyote atakayekaidi amri hiyo, atachukuliwa hatua za kisheria, na kuonya kuwa watu wasidanganyike kufanya matembezi hayo, ila kila mtu anayo haki ya kwenda katika mkutano kwa namna ya kawaida.

Hata hivyo, CHADEMA imepinga na kudai kuwa hayo si maandamano, bali matembezi maalum kutoka kwenye maeneo ya jiji kwenda viwanja vya Jangwani, ikizingatiwa kuwa hali ni ngumu na si kila mtu mwenye uwezo wa kumudu gharama za usafiri.

Chama hicho kimedai kuwa, Watanzania wanayo haki kikatiba kufanya maandamano na mikusanyiko ili mradi hawavunji sheria, na kimetangaza barabara zitakazotumiwa na watu wa majimbo ya Ilala, Ukonga na Segerea, kuwa ni Buguruni, Uhuru, Msimbazi, Morogoro hadi Jangwani.

Watakaotoka majimbo ya Kinondoni, Kawe na Ubungo, watakutanika katika bustani ya Magomeni, kupitia barabara ya Morogoro hadi Jangwani, wakati wale wa Kigamboni, wataanzia Kivukoni, kupitia Posta ya zamani, Makao Makuu ya Jiji, barabara ya Morogoro hadi Jangwani.

Wale wa Temeke, wataanzia Mwembeyanga, kupitia barabara ya Mandela, Buguruni na kukutana na wale wa majimbo ya Ilala na kuelekea Jangwani.
Chanzo: Tanzania Daima

Thursday, May 24, 2012

Mnyika Mbunge halali Ubungo

Best Blogger Tips
 CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana kilikuwa katika furaha baada ya Mbunge wake wa Ubungo, John Mnyika kuthibitishwa na Mahakama Kuu kuwa Mbunge halali wa Ubungo jijini Dar es Salaam.

Ubunge wa Mnyika ulikuwa unapingwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na aliyekuwa mgombea wa CCM, Hawa Ng’humbi.

Mahakama hiyo jana kupitia kwa Jaji Upendo Msuya, ilitamka kuwa uchaguzi katika jimbo hilo ulikuwa wa halali na kura alizopata Mnyika ni halali.

Aidha, Jaji Msuya alisema maombi ya Ng’humbi kuwa mahakama hiyo ibatilishe matokeo yaliyompa ushindi Mnyika yametupwa kwa kuwa hakuthibitisha madai yake na kutakiwa kulipa gharama za kesi hiyo aliyoifungua mwaka 2010, siku chache baada ya kubwagwa na kijana huyo.

Awali kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Mahakama hiyo jana ilijaa wanachama na wapenzi wa Chadema na CCM na kusababisha askari Polisi kufanya kazi ya ziada ya kutanda kila mahali katika mahakama hiyo na katika Barabara ya Kivukoni kuanzia Mahakama ya Rufaa wakiwa na magari ili kuimarisha ulinzi.

Hukumu hiyo ilisomwa na Jaji Msuya mahakamani hapo kwa takribani saa moja na nusu kuanzia saa 4 asubuhi ambapo pia amuru gharama za kesi hiyo kubebwa na Ng’humbi ambaye kabla ya kuwania ubunge mwaka 2010, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

Jaji Msuya alisema Ng’humbi katika madai yake yote matano hakuna hata moja alilolithibitisha kama ambavyo sheria inamtaka mdai katika kesi ya uchaguzi, kuthibitisha dai lake bila kuacha shaka yoyote na kutoa ushahidi kuonesha ni namna gani iliathiri matokeo ya uchaguzi.

Alisema Ng’humbi na mashahidi wake aliowaita mahakamani, hawakuonesha wala kuthibitisha madai yaliyowasilishwa hapo kwamba yalitendeka na namna gani madai hayo yaliathiri matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 31, mwaka juzi.

“Nilipata nafasi ya kupitia ushahidi wa kila shahidi pamoja na vielelezo vilivyotolewa mahakamani katika kesi hii, lakini nimeshangaa ni kwa nini mdai hakuleta mahakamani mashahidi ambao walikuwepo katika chumba cha majumuisho ya kura ambako ndiko madai hayo yalikotokea,” alisema Jaji Msuya.

Alisema hakuelewa ni kwa nini watu zaidi hawakuletwa kuunganisha ushahidi wao kuthibitisha madai ya mdai na kuhoji kama kweli madai hayo yalitokea, ni kwa nini wagombea wengine au watu waliokuwa katika chumba cha majumuisho hawakulalamika?

Katika madai ya Ng’humbi ya dosari ya kura zaidi ya 14,000 alizodai hazieleweki zimetoka wapi, Jaji alisema alipata nafasi ya kuhesabu kura walizopata wagombea wote wa vyama vilivyogombea jimbo hilo ambavyo ni 16 na kubaini ilikuwa ni kosa tu la kibinadamu na halina uhusiano wowote na mdaiwa wa pili, Mnyika.

Kwa mujibu wa Jaji Msuya, fomu namba 24 b ilikuwa na dosari na ndiyo ilikuwa inabishaniwa na Ng’humbi kwa kuwa ilikosewa kuandika.

Alisema Mnyika alitangazwa kuwa ni mshindi baada ya kupata kura 66,742 wakati Ng’humbi alipata kura 50,544 na wagombea wote kuwa kura 132,496.

Jaji Msuya alisema katika ushahidi wa Ng’humbi, hakuonesha ni vipi ongezeko hilo la kura liliathiri matokeo ya uchaguzi na vipi Mnyika alihusika na ongezeko hilo.

Kabla ya kuanza kuchambua hoja za Ng’humbi, Jaji Msuya aliwapongeza mawakili katika kesi hiyo ambao walijitahidi kuwasilisha mashahidi na kuhoji maswali ya msingi.

Alisema mawakili hao hawakupoteza muda kwa kuuliza maswali yasiyo na msingi wala kuwasilisha pingamizi zinazosababisha shauri kuwa na mlolongo mrefu.

Mnyika aliwakilisha na wakili Edson Mbogoro wakati wakili wa Ng’humbi alikuwa Issa Maige na Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliwakilishwa na Justus Mlokozi.

Kuhusu madai ya Ng’humbi kuwa alidhalilishwa kwa kuitwa fisadi na Mnyika katika mkutano alioufanya katika kampeni kwamba aliuza nyumba ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), na kwamba watu wasichague CCM inakumbatia mafisadi, Jaji Msuya alisema hayakuwa na ushahidi.

Alifafanua kwamba Ng’humbi alidai maneno hayo yalizungumzwa na Mnyika katika mkutano uliokuwa na watu zaidi ya 500, lakini yeye hakuwapo. Kutokana na kukosekana kwa uwepo wake, Jaji Msuya alisema Mahakama haichukui maneno ya kuambiwa, bali mtu aliyesikia mwenyewe au kushuhudia.

“Katika watu wote hao 500 waliokuwa katika mkutano huo, hakuja hata mtu mmoja kutoa ushahidi na pia haikuthibitishwa ni namna gani iliathiri uchaguzi na hivyo hoja hiyo imeondolewa,” alisema Jaji Msuya.

Kuhusu madai kwamba Mnyika aliingia na wafuasi wengine wa Chadema katika kujumlisha matokeo, Jaji Msuya alisema ushahidi pekee ni wa Ng’humbi na kwamba hadhani kuwa ni jambo linalowezekana mtu asiyehusika kuingia katika chumba cha majumuisho ya kura wakati kulikuwa na ulinzi.

Alisema mbali na ulinzi, hata wagombea wengine wangelalamikia jambo hilo, lakini Ng’humbi hakuleta mashahidi waliokuwa katika chumba hicho kutoa ushahidi kuwa kuna watu wasiohusika waliingia.

Kuhusu madai kuwa Msimamizi wa Uchaguzi alitumia kompyuta za mkononi (laptop) za Mnyika badala ya kompyuta rasmi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na pia hazikukaguliwa kiasi cha kutia shaka kuwa pengine kulikuwa na taarifa zisizo rasmi katika kompyuta hizo ikiwa ni pamoja na ongezeko lile la kura 14,000, Jaji Msuya alisema ushahidi umeonesha kuwa kompyuta hizo hazikutumika.

Alifafanua kwamba kompyuta zilizotumika zilikuwa za mawakala na kwamba katika madai hayo, Ng’humbi angeweza kuleta mashahidi zaidi kuthibitisha akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Rajab Kiravu.

“Tofauti ya kura kama nilivyosema nimepiga hesabu na nimeona kuwa ni matatizo ya kibinadam na hakuna athari yoyote katika matokeo ya uchaguzi, ni shahidi wa tatu pekee aliyekuja kutolea ushahidi hili na Ng’humbi angeweza kuleta mashahidi zaidi,” alisema Jaji Msuya ambaye alianza kuisikiliza kesi hiyo kuanzia Aprili 19, mwaka huu na majumuisho ya pande zote yalifanywa Mei 4, mwaka huu.

Baada ya hukumu hiyo, Mnyika alikumbatiana na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye alikuwapo mahakamani hapo. Pamoja walitoka nje, Mnyika akiwa amebebwa na wafuasi wa Chadema wakiimba na kushangilia kwa ushindi huo.

Hata hivyo, hakukuwa na vurugu kubwa zilizokuwa na madhara zaidi ya maandamano yaliyoondoka mahakamani hapo wakiimba.

Mbowe aliwaeleza waandishi wa habari kuwa kesi hiyo imetumia zaidi ya Sh bilioni mmoja na kutaka kabla ya kusikiliza kesi kama hiyo, uchunguzi ufanyike kwanza ili ikionekana haina hoja za msingi, itupwe mapema.

“Mahakama imetenda haki na hii inaonesha namna ambavyo inaweza kutenda haki hata katika vyama vya upinzani,” alisema Mbowe.

Naye Ng’humbi alisema amepokea uamuzi uliotolewa, lakini hawezi kusema lolote kwa sasa na kuwataka wana CCM wawe na utulivu kwa sababu anaamini ni watulivu na kama kuna jambo tofauti, atazungumza baadaye.

Hadi sasa, Mahakama imekwisha kutengua matokeo ya ubunge ya mwaka 2010 katika majimbo mawili pekee, Arusha Mjini kwa Godbless Lema wa Chadema na Sumbawanga Mjini lililokuwa la Aeshi Hilary wa CCM.

Majimbo ambayo kesi zao zilitupwa na mahakama na wabunge wake kuendelea na nafasi zao ni Segerea, Kasulu Mjini, Biharamulo, Singida Mashariki, Ilemela, Nyamagana, Kilwa Kusini, Muhambwe na Meatu.
Chanzo: HabariLeo

 

Sunday, May 20, 2012

Rage ataja kilichomliza kwa Patrick Mafisango

Best Blogger Tips
MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, ameanika kilichomliza wakati wa kusoma risala kwenye zoezi la kuaga mwili wa kiungo wa timu hiyo, Patrick Mafisango kwenye viwanja vya TCC, Chang’ombe juzi, jijini Dar es Salaam aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi.

Baada ya kufika katikati, Rage alijikuta akilemewa na simanzi hadi kuangua kilio, hivyo risala hiyo kusomwa na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu,’ hali ambayo ilizidi kuongeza huzuni kwa wengi.

Rage alisema jana kwa njia ya simu kuwa, alishindwa kuendelea na risala baada ya kuvuta hisia ya mengi mazuri, kubwa zaidi la utayari wake wa kuchezea Simba hata bure.

Alisema, Mafisango aliyekuwa akichezea Simba kwa mkopo akitokea Azam, baada ya timu kurejea kutoka Sudan, alimfuata na kumweleza kuwa, kama watamtema, yu tayari kuchezea timu hiyo bila kulipwa.

Rage alisema hayo baada ya kuona mkataba wake wa kuichezea Simba unakaribia mwisho, hivyo akaamua kueleza ya moyoni mwake kwa kusema, alikuwa tayari kubaki akicheza hata bure, ni timu aliyokuwa ameipenda.

“Ukweli ni kwamba, kilichoniliza hasa ni pale nilipokumbuka kauli yake ya mwisho ya kuniambia maadamu mkataba wake umeisha, ni bora aendelee kuichezea Simba hata bure kutokana na mapenzi yake kwa Simba,” alisema Rage na kuongeza: “Ni vigumu kumsahau mchezaji wa aina hii.

Rage, Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salam (DRFA) na Shirikisho la Soka Tanzania -TFF (wakati huo FAT), alisema kingine kilichomfanya apate uchungu zaidi, ni ushujaa wa Mafisango kukiri kosa.

Alisema, wakati Simba ikiwa kambini kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya ES Setif ya Algeria katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho, Mafisango alisimamishwa kwa utovu wa nidhamu.

Rage alisema nyota huyo alifanya kitu cha kishujaa ambacho hajapata kukiona, baada ya kwenda kambini Bamba Beach na kuwaomba msamaha wachezaji wanzake na benchi la ufundi chini ya Milovan Cirkovic.

Alisema, baada ya kufanya hivyo, Mafisango alifunga safari hadi nyumbani kwake (Rage), na kumwomba msamaha kwa kosa ambalo alilokuwa ametenda, kitu ambacho si cha kawaida kwa wachezaji walio wengi.

“Ni wachache wenye ujasiri wa kiwango chake, lakini Mafisango alifanya hivyo kiasi cha kunishangaza hata mimi, kuniafuata hadi nyumbani! “Sikusita kumsamehe, ingawa ilikuwa imesalia siku moja kabla ya kwenda Algeria,” alisema.

Alisema, kwa vile hakuwemo kwenye hesabu ya kwenda Algeria, alilazimika kufanya kazi ya ziada kupata tiketi na suti ya ziada, kabla ya kumpigia simu usiku kumjulisha alikuwa miongoni mwa wanaokwenda Algeria, hivyo kuwa ‘surprise’ kwa nyota huyo.

“Tiketi na suti kwa wachezaji zilikuwa tayari, kitendo cha Mafisango kuomba msamaha, nikampigia simu Meneja wa Egypt Air (Shirika la Ndege la Misri), kumwomba anitafutie tiketi moja, pia nikamnunulia suti kama wenzake, kisha nikampigia simu na kumpa taarifa ya ghafla,” alisema.

Aidha, Rage alisema kuelekea mechi ya mwisho ya Ligi Kuu dhidi ya Yanga, Mafisango alimwendea na kumweleza kuwa angemfurahisha kwa kucheza vizuri katika mechi hiyo, ikiwezekana kufunga mabao hadi wamtambue yeye ni nani.

“Kabla ya mechi ya Yanga, alinifuata na kunieza: “Mwenyekiti lazima nikupe raha baada ya mechi kwa kuwashindilia Yanga mabao mpaka wakome; wanitambue mimi ni Mafisango,” alisema Rage akimnukuu nyota huyo anayezikwa leo kwao DR Congo.

Rage alisema, alipotafakari utayari wa Mafisango kucheza Simba bure, kitendo cha kuomba radhi kwa staili ya kipekee na umati uliokuwa unazidi kufurika kuaga mwili wake, akajikuta ameshindwa kuendelea kusoma risala.

Alipoulizwa ni vipi ameshindwa kuondoka na mwili kama kiongozi mkuu wa klabu, Rage alisema alitamani iwe hivyo, lakini naye jana jioni alitarajiwa kuondoka kwenda Marekani kwenye msiba wa shangazi yake.
“Nilitamani sana kwenda, lakini leo jioni (jana), natarajia kwenda Marekani kwenye msiba wa shangazi yangu, ila nitawakilishwa na wengine. Mungu amlaze mahali pema peponi amen,” alisema Rage.
Chanzo: Tanzania Daima

Monday, May 7, 2012

Mkapa asimama kortini kumtetea Profesa Mahalu

Best Blogger Tips
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa jana alipanda kizimbani kumtetea Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu katika kesi ya uhujumu uchumi yanayomkabili, huku akimmwagia sifa kemkem za utumishi mwema.

Profesa Mahalu na mwenzake, Grace Martin aliyekuwa Ofisa Utawala wa Ubalozi huo, wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakidaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60, kupitia mchakato wa ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania Italia.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa Rais Mstaafu kupanda kizimbani kwa sababu yoyote ile.

Mkapa ambaye wakati wa ununuzi wa jengo hilo alikuwa Rais, aliieleza Mahakama kuwa anatambua mchakato wa ununuzi huo na kwa kuwa yeye ndiye aliyetoa idhini ya ununuzi, mchakato wote ulikwenda vizuri.

Mkapa na msafara wake ulioongozwa na maofisa wa itifaki aliwasili mahakamani hapo saa 3:45 asubuhi. Akiwa amevalia suti ya rangi ya kijivu alielekea ndani ya Mahakama hiyo akiwa amezungukwa na wapambe wake akitabasamu baada ya kuwaona wanahabari.
Aliingia katika chumba maalumu cha mapumziko hadi saa 5:32 asubuhi muda ambao aliitwa kizimbani kutoa ushahidi wake.

Kabla hajaanza kutoa ushahidi, alikula kiapo maalumu cha kutoa ushahidi wa ukweli na baadaye kuendelea hadi saa 7:31 mchana alipomaliza na kuondoka.

Mkapa alianza kutoa ushahidi katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ilvin Mugeta, akiongozwa na mmoja wa mawakili wa Profesa Mahalu, Alex Mgongolwa kwa kueleza historia ya utumishi wake katika nafasi za kidiplomasia.

Mkapa alijibu maswali kwa kujiamini na kwa umakini mkubwa huku mara kadhaa akiwavunja mbavu wasikilizaji kwa jinsi alivyokuwa akiwajibu mawakili wa Serikali wakati mwingine mwenyewe alishindwa kujizuia kucheka.

Akielezea mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo. Mkapa alidai kuwa Serikali yake ilifahamu ununuzi wake na taratibu za malipo baada ya kufahamishwa na Profesa Mahalu na kwamba lilinunuliwa kwa maagizo ya Serikali yake.

“Nilitambua muuzaji alipaswa alipwe malipo kwa kutumia akaunti mbili tofauti na Serikali ilitoa baraka. Mimi nilitaarifiwa na sikuzuia,” alidai Mkapa.

Kuhusu kuwepo kwa mikataba miwili katika ununuzi wa jengo hilo Mkapa alijibu: “Ninachoweza kukumbuka kwa hakika mimi ni kwamba niliambiwa kuwa kuna malipo katika akaunti mbili ‘separate’ (tofauti).

Alieleza kushangazwa na taarifa kwamba aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Martin Lumbanga katika ushahidi wake alidai kuwa alikuwa hajui mchakato wa ununuzi wa jengo hilo.

Wakili Mgongolwa: Shahidi, alikuja hapa Shahidi wa kwanza wa mashtaka (PW1), Martin Lumbanga akasema kuwa hakuwa na taarifa za idhini ya Serikali katika ununuzi wa jengo hilo. Je, wewe unasemaje?

Mkapa: Ninashangaa ni kwa nini alisema hivyo.

Mgongolwa: Lakini wewe ukiwa Rais ulijua na ukabariki, inawezekana yeye asingeweza kujua?

Mkapa: Ndiyo.

Mkapa alidai kuwa katika mchakato wa ununuzi wa jengo hilo, mbali na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia kwa Balozi Mahalu, wizara nyingine ambazo zilihusika ni Ujenzi na Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akidai kuwa zote zilituma wataalamu wake kufanya tathmini ya jengo hilo kabla ya ununuzi.

Akielezea maelezo yaliyoko katika kielelezo cha 6 cha ushahidi wa upande wa utetezi ambacho ni taarifa ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa bungeni wakati huo Jakaya Kikwete (sasa Rais) juu ya mchakato wa ununuzi wa jengo hilo Mkapa alisisitiza:

“Maneno hayo ni sahihi. Hayo ndiyo ninayoyajua mimi kuwa ndiyo yaliyotokea.”

Taarifa hiyo pamoja na mambo mengine, inaeleza kuwa jengo hilo lilinunuliwa kwa jumla ya Sh.2.9 bilioni na kwamba hati za umiliki wake zilishawasilishwa wizarani na kupelekwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Mkapa alieleza kuwa hajawahi kupata malalamiko yoyote kutoka Italia kuhusu ukiukwaji wa sheria katika mchakato wa ununuzi wa jengo hilo na wala kwa mmiliki wa jengo hilo kudai kuwa alilipwa pungufu ya kiasi walichokubaliana.
Wakili Mgongolwa: Kikatiba Rais hukabidhiwa ripoti ya CAG. Je, una taarifa yoyote ya CAG kuhusu malalamiko juu ya ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Sikuwahi kupata malalamiko hayo.
Wakili: Nini ufahamu wako kama Rais Mstaafu juu ya utumishi wa mshtakiwa ambaye ulimteua kuwa Balozi Italia?
Mkapa: Ninamfahamu kama ni msomi mzuri, mwadilifu na mfanyakazi mwaminifu na kiongozi wa haki.
Akizungumzia mawasiliano yake na Profesa Mahalu wakati akiwa Balozi, Mkapa alidai kuwa walikuwa wakiwasiliana ama kwa maandishi au kwa mdomo na kwamba hiyo ilitegemea usiri wa jambo husika, lakini akasisitiza kuwa wakati wa mchakato wa ununuzi wa jengo hilo waliwasiliana.
Baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake, Mkapa aliulizwa maswali mbalimbali na mawakili wa Serikali, Vicent Haule na Ponsiano Lukosi kuhusu ununuzi wa jengo hilo, sehemu ya mahojiano hayo ilikuwa kama ifuatavyo:
Wakili Haule: Mheshimiwa katika Hansard (kielelezo namba 6 cha upande wa utetezi) uliyosoma imeandikwa jumla ya pesa zilizopelekwa kununua jengo hilo ni kiasi gani?
Mkapa: Sh.2.9bilioni.
Haule: Na zilizoandikwa kwenye hii risiti ambazo ulisema ulikuwa unazifahamu ni kiasi gani?
Mkapa: Nilichosema ni Euro 3milioni, mimi sijui exchange rate (gharama za ubadilishaji wa fedha) wakati huo ilikuwa ni kiasi gani hiyo si kazi yangu.
Haule: Nani aliagiza upelelezi wa ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Mimi Sijui.
Haule: Uchunguzi wa malipo hayo ulifanyika lini ukiwa bado madarakani au baada ya kutoka madarakani?
Mkapa: Mimi sijui, nilikuja kusikia tu kuwa Balozi wako anashtakiwa.
Haule: Ulijua lini kuwa Balozi wako uliyekuwa umemteua wewe anashtakiwa?
Mkapa: Siku alipofikishwa mahakamani ndipo nilipoambiwa na kesho yake kweli nikamuona kwenye magazeti.
Haule: Ulisema ulipotaarifiwa kuhusu ununuzi huo ulibariki na hukuzuia, kwani ulipaswa kuzuia?
Mkapa: Ningeweza kuzuia na kuamuru hizo pesa zipelekwe kwingine kwa kuwa wakati huo tulikuwa na crisis (tatizo) ya fedha, lakini kwa kuwa niliona umuhimu wa ununuzi wa jengo hilo nikaagiza linunuliwe.
Haule: Umuhimu upi wa kulipa kupitia akaunti mbili?
Mkapa: Kupata Chancellery (ofisi ya ubalozi)
Haule: Baada ya kutoa maagizo hayo (kwa Profesa Mahalu) ni nani mwingine wizarani (Mambo ya Nje) uliyemwarifu kuhusu malipo hayo kwa akaunti mbili?
Mkapa: Kwani hiyo inahusiana na nini? Maagizo yangu mimi nilishatoa kwa balozi jengo linunuliwe, kama Rais nilikuwa ninaagiza tu.
Haule: Mheshimiwa, nakuuliza tena na nisingependa nawe uniulize swali. Ni kweli au si kweli kwamba hakuna mtu mwingine wizarani ambaye ulimpa taarifa hizo?
Mkapa: Sikumbuki mimi.
Lukosi: Mheshimiwa, Lumbanga akiwa Katibu Kiongozi ulikuwa ukimwamini?
Mkapa: Ndiyo.
Lukosi: Ni kwa kiasi gani ulimshirikisha katika ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Specifically katika hilo sikumbuki lakini ki-principle nilishatoa maagizo kuwa kupata chancellery nunueni na yeye alikuwa akijua. Tulifanya hivyo India, Marekani na Uingereza.

Lukosi: Sasa Lumbanga alisema hajui ununuzi wa hili. Je, wewe unaona ni kitu cha kawaida?

Mkapa: Ndiyo maana nimesema nashangaa, maana haingewezekana kwamba mimi nika-communicate (nikafanya mawasiliano) na wizara moja tu na Lumbanga asijue.

Lukosi: Ulipata kujua au kuuliza ni kwa nini muuzaji alitaka alipwe kupitia akaunti mbili tofauti?
Mkapa: Sikuuliza, mimi nilichokuwa nataka ni Chancellery.
Lukosi: Unakumbuka kuna jengo jingine la ubalozi ambalo muuzaji alitaka alipwe kwa utaratibu huu wa kupitia akaunti mbili tofauti?
Mkapa: Siwezi kusema, nakumbuka lakini siwezi kusema kwa sababu mambo mengine ukiyasema, yanaweza kuharibu uhusiano na nchi husika.
Hakimu Mugeta: Kwa hiyo hayo mazingira huwa yapo?
Mkapa: Ndiyo.
Lukosi: Unawakumbuka watu wengine uliowahi kuwateua ambao wako mahakamani na yuko mwingine alishakuja kukuomba umtetee?
Mkapa: Ni lazima nilijibu hili? Alihoji Mkapa huku akicheka na kuwafanya wasikilizaji nao wacheke.
Lukosi: Kwa hiyo hii ni kesi ya kwanza kwako kuombwa kuja kutoa ushahidi?
Mkapa: Ndiyo.
Wakili: Nikiwaambia lengo la mwenye jengo kutaka mchakato wa uuzwaji kuwepo na mikataba miwili lilikuwa ni kukwepa kodi kwa Serikali yake utasemaje?
Mkapa: Hilo ni tatizo lake na nchi yake, mimi nilikuwa nataka nyumba na nimepata nyumba, nasema Al Hamdulillah, alisema Mkapa huku akicheka tena na kuwafanya wasikilizaji nao wavunjike mbavu.
Lukosi: Nikikwambia kuwa hizo pesa kulipwa kwa instalment (awamu), Profesa Mahalu alikuwa anataka azitumie kwa maslahi yake utasemaje?
Mkapa: Mimi nitashangaa sana, hasa nitakushangaa wewe, maana Profesa mimi namuamini. Alisema Mkapa na kuwachekesha wasikilizaji.
Mahojiano kati ya Mkapa na Wakili wa Profesa Mahalu, Mabere Marando katika kusawazisha maswali aliyoulizwa na mawakili wa Serikali yalikuwa kama ifuatavyo:
Wakili Marando: Shahidi, Umewahi kupata malalamiko yoyote kutoka wizarani kuwa kuliwapo makosa katika ununuzi wa jengo la Ubalozi Italia?
Mkapa: Sijawahi.
Wakili: Ama kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Martin Lumbanga au Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje au wa Wizara ya Fedha au Hazna kwamba Balozi alifanya kosa kwenda kufanya malipo katika akaunti mbili za muuzaji?
Mkapa: Yeyote kati ya hao hakuna.
Marando: Mpaka unaalikwa kwenda kuzindua jengo hilo uliwahi kupata ushauri kutoka Ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma) au kwa AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) kwamba usiende katika uzinduzi wa jengo hilo kwa kuwa kuna uchafu?
Mkapa: Sikuwahi kushauriwa.
Awali, Profesa Mahalu akijibu maswali ya Wakili Mgongolwa, alisema kuwa Februari 19, 2006 alipigiwa simu na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na kumwarifu kuwa kesho yake anatakiwa afike Dar es Salaam kwa ajili ya mashauriano.

Alidai kuwa alimwambia kuwa kesho yake isingewezekana kwa sababu ilibidi ajiandae, ndipo akaambiwa kuwa Februari 21, awe amefika.

Alidai kuwa majira ya alasiri kama saa 10:30 ya Februari 21 alikuwa ameshafika ofisini kwa Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Patrick Mombo ambaye alimpa barua ya utenguzi wa uteuzi wake kama Balozi nchini Italia iliyokuwa imeandikwa siku hiyohiyo ya Februari 21, 2006.

Profesa Mahalu alisema kuwa alishangaa maana hakuwahi kuwa na jambo la kusababisha uteuzi wake kutenguliwa na kwamba alipomuuliza Mombo alimjibu tu kuwa ni agizo ya Rais.

“Kabla ya kutenguliwa kwa uteuzi huo sikuwahi kuwa na tuhuma yoyote juu ya jambo lolote,” alisisitiza Profesa Mahalu.
Katika kiapo chake alichokiwasilisha mahakamani mwaka jana Mkapa alisema: “Kwa kipindi chote ambacho nimefanya kazi na Balozi Mahalu katika nafasi mbalimbali za utumishi wa Serikali ameonyesha tabia thabiti na za dhati, uaminifu, utiifu, uchapakazi na ubora.”
Alisema kuwa sifa hizo zilimfanya atunukiwe na Rais wa Italia, Tuzo ya Heshima ya Juu wakati wa kuadhimisha siku ya taifa hilo, muda mrefu baada ya kuwa ameondoka nchini humo.
Mahalu na mwenzake wanadaiwa kula njama na kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti na katika maeneo tofauti huko Italia, likiwamo la kumpotosha mwajiri wao katika hati ya matumizi.
Wanadaiwa kuwa Septemba 23, 2002 jijini Rome, wakiwa waajiriwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walisaini vocha yenye namba D2/9/23/9/02 ikionyesha kuwa bei ya ununuzi wa jengo la ubalozi ni Euro 3,098,741.58, maelezo ambayo yalikuwa ni ya uongo na yenye nia ya kumdanganya mwajiri wao.
Chanzo: Mwananchi

Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits