NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bw. January Makamba
amewataka wananchi wa Tarafa ya Mgwashi mkoani Tanga kutumia fursa
mbalimbali ikiwemo kufanya biashara na Halmashauri mpya ya Bumbuli
badala ya kuwaachia wageni waiuzie halmashauri hiyo hadi karatasi za
ofisini.
Chanamoto hiyo aliitoa juzi wakati anahutubia
mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Mgwashi Kata ya Mgwashi
wilayani Lushoto na kuwaeleza wananchi kuwa kwa kupata halmashauri ni
ushindi mkubwa kwani pamoja na kufanya biashara, lakini pia huduma za
jamii zitaboreka.
"Nitashangaa kama nitaona hata biashara ya
kuuza karatasi (shajala) mtawaachia watu kutoka Arusha. Sasa ni wakati
wenu kufanya biashara na Halmashauri ya Bumbuli kwa kuchukua zabuni
mbalimbali ili kuinua vipato vyenu," alisema Bw. Makamba.
Bw.
Makamba aliwatahadharisha wananchi wa tarafa hiyo kuwa uteuzi wa yeye
kuwa Naibu Waziri hauwezi kumaliza changamoto zao bali ataendelea
kupigana kama Mbunge kuona kero mbalimbali zikipatiwa ufumbuzi moja
baada ya nyingine.
"Jamani mimi nilipokuja hapa niliomba kazi ya
ubunge. lakini sio uwaziri, hivyo nafasi yangu ya unaibu Waziri hauwezi
kumaliza kero na changamoto zenu, bali kama nilivyopigana kama mbunge
wenu wa kupata umeme tangu dunia iumbwe kwenye Tarafa ya Mgwashi.
"Ndivyo
nitakavyo hakikisha barabara ya kutoka Mbelei hadi Mashewa
inatengenezwa huku ikihamishiwa kutoka halmashauri kwenda TANROADS
(Wakala wa Barabara) ambayo itawezesha kusafirisha mazao yenu, lakini
pia
tatizo la maji linakwisha," alisema Bw. Makamba.
Awali,
Ofisa Tarafa ya Mgwashi Bw. Moka Urban alimueleza Bw. Makamba ambaye pia
ni Mbunge wa Bumbuli kuwa Kituo cha Afya Mgwashi kinaletewa dawa kama
kata badala ya kituo cha afya, hivyo kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Bw.
Urban alisema pia barabara ya kutoka Soni hadi Mgwashi sio nzuri, umeme
bado haujafika kwenye vijiji vingi pamoja na kufika makao makuu ya kata
ya Mgwashi na baadhi ya vijiji havina mawasiliano ya simu.
Chanzo: Majira
Thursday, May 31, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment