Viongozi wawili wa kundi la Uamsho waliokuwa
wanashikiliwa na polisi wa Zanzibar kwa zaidi ya siku mbili pamoja na
baadhi ya wafuasi wao wameachiwa kwa dhamana katika mahakama ya
Mwanakwerekwe huko mjini Zanzibar.
Mwandishi wetu Aboubakar Famau aliyekuwa Zanzibar anasema hali ilianza kuwa shwari mjini Zanzibar baada ya kuachiliwa kwa dhamana kwa wafuasi takriban thalathini wa kundi la Uamsho waliokuwa wanashikiliwa na polisi mjini humo kwa tuhuma za kuandamana bila kibali.
Miongoni mwa waliopata dhamana hiyo ni Sheikh Mbaruku Saidi Khalfan na Musa Juma Musa wote wakiwa viongozi wa kundi hilo ambao kukamatwa kwao kumeleta kizazaa mjini humo.
Mbele ya Hakimu wa mahakama ya Mwanakwerekwe majira ya saa nne asubuhi Jumatatu, baada ya kusomewa mashtaka ya kufanya mkusanyika haramu katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, watuhumiwa hao kwa pamoja walikana tuhuma hizo.
Baadaye wakili wa watuhumiwa hao aliwaombea dhamana, ombi ambalo lilikubaliwa bila pingamizi lolote.
Kukamatwa kwa viongozi hawa kumeleta sokomoto kubwa mjini Unguja hasa baada ya wafuasi wa kundihilokuamua kuandamana kwa lengo la kuishinikiza polisi kuwaachia.
Hali iliyosababisha vuta nikuvute baina ya wafuasi hao na polisi ambao wamekuwa wakitumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.
Uamsho ni kundi la kidini ambalo limejipa jukumu la kuwaelimisha wazanzibari kuhusu suala la muungano hasa wanapotoa maoniyaokatika Tume ambayo inakusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Hata hivyo, taarifa zisizothibitishwa zinasema, kundihilolimejikita zaidi katika kuwahamasisha wananchi kuupinga muungano.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment