Meneja wa Bolton Owen Coyle amesema alizungumza "kwa ufupi" na Fabrice
Muamba kwa mara ya kwanza tangu kiungo huyo alipopoteza fahamu kutokana
na matatizo ya moyo.
Mchezaji huyo amelazwa katika hospitali ya London Chest baada ya
kuanguka na kupoteza fahamu wakati Bolton walipokuwa wakicheza dhidi ya
Tottenham katika robo fainali ya kuwania Kombe la FA siku ya Jumamosi.
"Bado ana safari ndefu kupona kabisa lakini kusema ukweli maendeleo yake yanatia moyo," alisema Coyle.
"Kwa hali tuliyokuwa nayo siku ya Jumamosi usiku, kwa hapa tulipofikia kamwe sikutarajia hali ya kutia moyo kama hii."
Muamba alipata usingizi "mzuri" usiku wa
Jumatatu katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum,
taarifa ya pamoja ya klabu ya Bolton na hospitali ilieleza siku ya
Jumanne.
Waganga wamesema wanaendelea kumuangalia kwa karibu kujua maendeleo yake.
Siku ya Jumatatu ilielezwa bado alikuwa akiumwa
sana lakini kwa sasa hali hiyo imetengemaa baada ya mchezaji huyo wa
zamani wa kikosi cha vijana cha England chini ya umri wa miaka 21 kuanza
"kupumua bila ya msaada wa mashine".
Source: BBC
Wednesday, March 21, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment