CCM yapata pigo katika ubunge Tanzania
Via VOA News
Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa Tanzania ulofanyika tarehe 31 Oktoba, yanaoynesha baadhi ya wakuu wa serikali katika nafasi za mawaziri na wakuu wa mikoa, wametupwa katika nafasi za ubunge zilizokuwa na upinzani mkali.Miongoni mwa waliopteza nafasi katika serikali kuu, ni Dk. Batilda Buriani ambaye alikua akiwania ubunge kaika jimbo la Arusha mjini ameshindwa kwa kishindo na Godbless Lema wa CHADEMA.
Philip Marmo ambaye ni kiongozi wa siku nyingi katika serikali naye ameshindwa kuitetea nafasi yake ya Mbulu. Vongozi wengine ambao wanasadikiwa wamepoteza nafasi zao ni pamoja na aliyewahi kuwa waziri katika serikali Anthony Dialo, Waziri wa sasa wa mambo ya ndani Lawrence Masha aliyeshindwa na Ezekiah Wenje wa CHADEMA pia katika jimbo la Nyamagana.
Waziri wa viwanda na biashara Mary Nagu ambae alikua anatetea kiti chake cha huko Hanang ameondolewa sawa na Getrude Mongella wa CCM aliyekua spika wa Bunge la Afrika.
Viongozi wengine wa serikali za mikoa walioshindwa ni pamoja na Monica Mbega wa Ruvuma, na Mohamed Abdulaziz wa Lindi. Vincent Nyerere ambaye ni mtoto wa kakake rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere, ameshinda jimbo la Musoma mjini.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi jaji mstahafu Lewis Makame, alitangaza Jumatatu matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais ya majimbo 10 ya Tanzania bara na visiwani.
No comments:
Post a Comment