Friday, November 5, 2010

Best Blogger Tips
JK Ateuliwa Kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kuapishwa kesho

 Akitangaza rasmi matokeo ya Urais sasa hivi katika viwanja vya Karimjee,jijini Dar Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Lewis Makame,ametangaza rasmi kuwa Dk Jakaya Mrisho Kikwete kupitia chama cha CCM ameteuliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu nyingine tena ya pili.

Rais Kikwete ameibuka kwa ushindi wa kura Mil.5,276,827 ambayo ni asilimia 61% ya watu wote waliopiga kura,Huku mpinzani wake wa karibu kupitia chama cha CHADEMA,Dk.Willbroad Slaa (ambaye hakuwepo kwenye kushiriki hafla hiyo ya kutangazwa rasmi kwa kiti cha urais) ameibuka na idadi ya kura Mil.2,271,941 ambayo ni 20% ya wapiga kura.Mh Makame amesema kuwa idadi ya wapiga kura waliojiandikisha jumla yao ilikuwa ni Milioni 20,137,303,lakini waliopiga kura idadi yao ilikuwa ni Milioni 8,626,283 ambayo ni 42% ya waliopiga kura.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits