Republican yashika udhibiti wa bunge
Imekuwa siku muhimu kwa chama cha Republican nchini Marekani baada ya matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula kuangazwa. Baadhi ya maeneo muhimu ambayo yalikuwa ngome ya chama cha Democratic sasa yako chini ya chama cha Republican.
Hii ina maana kwamba spika mpya atakuwa John Boehner kutoka jimbo la Ohio.
Amesema kwa kuwa sasa chama chake kina idadi kubwa ya wabunge watajiandaa kufanya mambo kwa njia tofauti. Ameongeza kuwa watazingatia kupunguza matumizi badala ya kuongeza.
Hamasa kubwa inayoonekana katika kampeni za chama cha Republican imetoka kwa vuguvugu la Tea party ambalo limeundwa na wanaharakati.
Chama cha Rais Barack Obama kimepata pigo kubwa kama ilivyotarajiwa lakini pia wamejipatia ushindi katika maeneo machache ikiwa ni pamoja na Nevada ambapo kiongozi wa Senate Harry Reid alimshinda mpinzani wa vuguvugu la Tea party.
Baada ya kutangazwa mshindi seneta Reid alikiri kuwa kilikuwa kibarua kigumu kuhimili upinzani huo.
Rais Obama sasa atakabiliwa na changamoto kubwa katika kutimiza ajenda yake.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment