Sitta: Bunge lijalo linatisha
Asema limesheheni watu makini kutoka upinzani
SPIKA wa Bunge lililomaliza muda wake, Samuel Sitta, amesema Bunge lijalo litakuwa tishio na anatamani kuwa spika wake.
Sitta alitoa kauli hiyo jana muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge katika Jimbo la Urambo Mashariki (CCM).
Sitta ambaye amejiita kuwa ni ‘Chuma cha Pua’ kutokana na ushindi alioupata, alisema amekuwa akisoma majina ya wabunge wateule walioshinda na kubaini kuwa limesheheni vijana wengi machachari na watu wenye uwezo na uzoefu wa siasa kutoka vyama vya upinzani.
“Bunge lijalo ninavyoliona mimi, litakuwa Bunge la kutisha, maana lina vijana na watu machachari, ukisoma majina yao utaona kabisa kwamba ni watu makini na ni tishio, hivyo natamani kuwa spika wa Bunge hilo ili nikabiliane na changamoto zitakazojitokeza,” alisema Sitta.
Kwa mujibu wa Sitta, pamoja na bunge hilo kuwa na watu machachari, anaamini kwamba atalimudu vyema hivyo amekiomba chama chake kumpa ridhaa ya kushika wadhifa huo kwani ana uzoefu wa kutosha.
Alipoulizwa jambo gani analolikumbuka katika Bunge lililopita na lililotoa changamoto kubwa kwake, Sitta, hakusita kutaja sakata la Richomnd, lililosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa huo.
Sakata hilo lilisababisha pia aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha na wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kujiuzulu.
Endelea kusoma habari hii....................
No comments:
Post a Comment