JK aapishwa kuwa Rais wa Tanzania
Akitoa hotuba mara baada ya kuapishwa alisema kuwa kipao mbele chake kwa hivi sasa ni kuhakikisha kuwa wanajenga umoja wa kitaifa na kurudisha amani iliyokuwepo awali kwani anaamini kuwa uchaguzi uliweza kuwagawa watanzania kwa namna moja ama nyingine.
Alisema mchakato wa jinsi serikali yake itakavyofanya kazi ataitoa hivi karibuni wakati akilihutubia Bunge jipya.
Alisema kuwa katika mchakato wa kuwania uongozi nchini ni wazi kuwa yapo majeraha yaliyotokea hivyo muda huu ni mzuri kwa baadhi ya taasisi kurejesha amani ya watanzania.
Amevipongeza vyama vya upinzani kwa kukipa changamoto Chama Cha Mapinnduzi na kudai kuwa wamewaamsha katika usingizi kwani hivi sasa watakaa chini na kujiuliza kuwa ni wapi walipo na wafanyaje katika chaguzi zingine zijazo.
Wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi waliweza kuhudhuria katika hafla hiyo ya kuapishwa rasmi kwa rais kikwete akiwemo, Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Rais wa Zammbia Rupia banda, Rais wa Jam huri ya Demokrasia ya Kongo Joseph kabila, Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma, Rais wa Kenya mwai Kibaki, Rais wa Zanzibar Ally Mohamed Shein, maraisi wastaafu wa Tanzania Ally Hassan Mwinyi, Benjamini William Mkapa na Rais mstaafu wa Zanzibar Ally Karume.
Sherehe hizo zilipambwa na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo rais Kikwete alipigiwa mizinga 2I pamoja na ndege za kivita kufanya maonyesho na baadaye alikagua gwearide likiwa katika muonekano wa alfa.
No comments:
Post a Comment