Mawaziri na Manaibu waziri wapya
Jana Rais Jakaya Kikwete alitangaza baraza la mawaziri ambalo linajumuisha mawaziri 29 na naibu mawaziri 15 hivyo jumla yao kuwa 44. Katika safuhii tunakuletea wasifu wa baadhi ya mawaziri ambao wamo katika baraza hilo litakaloapishwa Jumamosi ya wiki hii, Ikulu jijini Dar es Salaam.
1. Jina: Mathias Meinrad Chikawe Malome
Nafasi: Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais – Utawala Bora
Kuzaliwa: 30 May 1951
Jimbo la Ubunge: Nachingwea - CCM (2005-2010) na amechaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa 2010
Nafasi nyingine:
Waziri wa Katiba na Sheria (2006-2008)
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria (2005-2006)Elimu:
Stashahada wa Uzamili ya Sheria za Kimataifa na Maendeleo (Uholanzi) (1981 -1982)
Stashahada wa Uzamili katika Utawala (Uingereza – 1977 – 1978)
Shahada ya Sheria - LL.B (Hons) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1972 – 1975)
2. Jina: Stephen Masato Wasira
Nafasi: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu
Kuzaliwa: 1945
Jimbo la Ubunge: Bunda – CCM (2005 – 2010) na amechaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa 2010
Nafasi nyingine
• Waziri: Kilimo na Mifugo (1989 – 1990), Maji (Januari 2006 - Octoba 2006), Kilimo, Chakula na Ushirika (Octoba 2006 - Februari 2008), Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) (Februari 2008 - Mei 2008) na Kilimo, Chakula na Ushirika (Mei 2008 – Novemba 2010).
• Mbunge: Mwibara (1970 – 1975), Bunda (1985 – 1990),(1995 -1996) na (2005 – 2010)
• Naibu Waziri: Wizara ya Kilimo (1972 – 1975), Serikali za Mitaa (1987 – 1989),
• Mkuu wa Mkoa: Mara (1975 – 1982), Pwani (1990 – 1991),
• Waziri mwambata: Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC, Marekani (1982 – 1985)
Elimu
• Shahada ya Uchumi (BA in Economics) Chuo Kikuu cha Washington, DC (Marekani)
• Shahada ya Sayansi ya Siasa (Chuo Kikuu cha Washington, DC (Marekani)
• Shahada za Uzamiri katika Utawala (Masters in Public Administration),Chuo Kikuu cha Washington, DC Marekani.
3. Jina: Hawa Abdulrahman Ghasia
Nafasi: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Manejimenti ya Utumishi wa Umma Kuzaliwa: 10 Januari 1966
Jimbo la Ubunge: Mtwara Vijijini (2005 – 2010) na amechaguliwa katika uchaguzi mkuu wa 2010.
Nafasi nyingine:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Manejimenti ya Utumishi wa Umma (2006 – 2010)
Elimu:
Shahada ya Uzamiri ya Maendeleo Vijijini (M.A. Rural Development) Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) (2001-2003)
Stashahada ya juu ya Uchumi (1992 1995) Chuo Kikuu cha Mzumbe
Historia ya Ajira
Mkurugenzi Msaidizi na nafasi mbalimbali katika – Halmashauri ya Wilaya ya Masasi (1992 – 2005).
Endelea kusoma habari hii..........................
No comments:
Post a Comment