IGP Mwema apangua makamanda
Amng'oa kamishina Nzowa Dawa za kulevya
MKUU wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, amefanya mabadiliko makubwa kwa makamanda wa Polisi wa mikoa na maofisa waandamizi ndani ya jeshi hilo.
Habari za kuaminika zilizopatikana mjini Dar es Salaam jana, zinasema IGP Mwema amefanya mabadiliko hayo ikiwa ni sehemu ya uboreshaji na utendaji kazi wa kila siku wa jeshi hilo.
“Ni kweli IGP Mwema amefanya mabadiliko makubwa yakianzia makao makuu ya jeshi hadi kwa makamanda wa polisi wa mikoa, nadhani nia ni kuboresha utendaji wa chombo hiki,” kilisema chanzo chetu.
Katika mabadiliko hayo, IGP Mwema amemhamisha Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Godfrey Nzowa, kwenda ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), pia amemhamisha Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Charles Mkumbo, ambaye sasa anakwenda makao makuu.
Wengine waliokumbwa na uhamisho huo ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, ambaye anahamishiwa makao makuu, wakati nafasi yake inachukuliwa na Charles Kenyela anayetoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Pia IGP Mwema amemhamisha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye, kwenda mkoani Arusha, wakati aliyekuwa kamanda wa mkoa huo, Basilio Matei, amehamishiwa makao makuu.
Taarifa zinasema, nafasi ya Kamanda Andengenye imechukuliwa na ofisa mmoja kutoka makao makuu aliyetajwa kwa jina la Mama Charo.
Rungu hilo limemwangukia pia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi, ambaye amehamishiwa makao makuu, huku nafasi yake ikichukuliwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani.
Endelea kusoma habari hii.................
Source: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment