Sugu asiachwe yatima, asaidiwe kuleta mapinduzi
Via Mwananchi
KATIKA matokeo ya wagombea ubunge, sasa tayari wameanza kazi ya ubunge baada ya kula kiapo jana kule Dodoma, yale ya Joseph Mbilinnyi , maarufu Sugu au Mr II yalivuta hisia za wengi.Licha ya kuwa mbunge wa Mbeya Mjini lakini Sugu ambaye alishinda kwa kishindo kikubwa dhidi ya mgombea wa CCM, Benson Mwalugala Mpesya, lakini tunaweza kumweleza kuwa sasa ni mwakilishi wa wasanii wa Tanzania ndani ya chombo cha kutunga sheria.
Mwanzo ilikuwa vigumu kuamini kuwa ilikuwaje hadi Sugu akaamua kuingia katika siasa, tena kugombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hapo ikawa mwanzo wa wasanii mbalimbali nao kuibuka na kutangaza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Hata hivyo, wengi walishindwa katika nafasi ya udiwani.
Mbunge huyo mpya licha ya kuchanguliwa na wananchi wa Mbeya Mjini, lakini naamini atawahudumia watu wengi zaidi kwani kila msanii au mdau wa fani au kazi ya zanaa, anaamini kuwa kazi yake kubwa akiwa bungeni atakuwa balozi na mwakilishi wa wasanii wote nchini na si wale wa Mbeya Mjini pekee.
Katika kampeni hizo, ahadi mbalimbali zilitolewa na sasa wananchi wanasubiri utekelezaji wake licha ya kuwa wasipotekeleza wajue mwaka 2015, mwendo wao wa kurejea bungeni utakuwa mgumu.
Mwanzo wa kampeni zilizuka tarifa kuwa kuna baadhi ya wasanii walimkacha msanii huyo wakati alipokuwa katika hatua za awali akitangaza kugombea ubunge, sitaki kuamini kuwa wasanii hao wapo na kama wapo watakuwa wachache na labda walifanya hivyo kutokana na kukosa uvumilivu uliotokana na kutokuwa na kutopata mahitaji muhimu ambayo labda yangeweza kuwawezesha kuendelea kuwa bega kwa bega na Sugu kwa muda wote wa kampeni yake.
Ninachoamini ni kwamba kama kweli wapo wasanii waliomtenga balozi wao, hawakuwa na nia mbaya naye ya kutaka ashindwe, bali majukumu ndiyo yaliyowafanya wafikie hali hiyo.
Naamini walifanya hivyo wakiamini kuwa licha ya kutokuwepo kwao atafanikiwa kuwa mbunge wa Mbeya Mjini na ndiyo maana baada ya kutangazwa kuwa mshindi wamejitokeza kumpongeza.
Nimezungumzia dhana ya kuondoa chuki, imani potofu na visasi ambavyo huenda vikajitokeza kutokana na tuhuma za kutengwa kwa Sugu na baadhi ya wasanii.
Lakini, ninavyoamini mimi ni kwamba kama chuki na visasi vitachukua nafasi katika miaka hii mitano ya uwakilishi wa Sugu kule bungeni, hakika hatoweza kurudi tena bungeni na ndoto za kufanikisha kuweka au kuingiza changamoto ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria zitakuwa zimekwama.
Endelea kusoma habari hii.................
No comments:
Post a Comment