Tuesday, April 26, 2011

Best Blogger Tips
Waziri mwingine atua Samunge

Via Mwananchi

NAIBU Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chizza na familia yake, jana walikuwa miongoni mwa watu waliopata kikombe cha tiba ya magonjwa sugu kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila katika Kijiji cha Samunge, Loliondo.

Chizza aliwasili Samunge akiwa na mkewe na wanafamilia wengine na kupokewa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali. Mbali ya kupata kikombe, alitumia fursa hiyo pia kumpa pole mchungaji huyo ambaye amefiwa na mtoto wake.

Akizungumza mara baada ya kupata kikombe cha tiba, Chizza alisema ni wajibu wa Serikali kuboresha miundombinu ya kufika Samunge kutokana na watu wengi wa ndani na nje ya nchi kwenda Samunge."Bado barabara siyo nzuri na mazingira ya Samunge ni machafu. Ni wajibu wa Serikali kuboresha miundombinu na utaratibu wa kutunza mazingira," alisema Chizza.
Waziri huyo ambaye alifika Samunge kwa gari alisema, ameamua kutumia mapumziko ya Pasaka kwenda Samunge kupata tiba baada ya kusoma habari za Mchungaji Mwasapila na kupata taarifa za watu kupona magonjwa mbalimbali.

Robo tatu ya magari Samunge yatokea Kenya
Raia wa Kenya, juzi na jana walitinga kwa wingi hapa Samunge na kufanya karibu robo tatu ya magari yaliyokuwapo hapa kutoka nchi hiyo jirani. Mengi ya magari hayo ni mabasi madogo, maarufu kama matatu (daladala).

Wakenya hao waliingia kuanzia juzi usiku na kutawala Viwanja vya Samunge, huku magari machache ya Watanzania yakianza kuingia jana asubuhi.Licha ya Wakenya, raia wa Rwanda na Uganda jana walitinga Samunge na kupata kikombe na sasa idadi ya wageni kutoka nje ya nchi waliofika Samunge, imefikia zaidi ya 13,700.
Endelea kusoma habari hii...................................
Best Blogger Tips
Liyumba kutoka gerezani?

Via Tanzania Daima

WAKATI Rais Jakaya Kikwete akitoa msahama kwa wafungwa 3,060 katika kuadhimisha miaka 47 ya Muungano, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, anatajwa kuwa miongoni mwa walionufaika na msamaha huo.

Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata kutoka kwa watu wa karibu na Liyumba zinapasha kuwa msahama huo unaweza kumnufaisha yeye na wenzake wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano ambao hadi jana walikuwa wametumikia robo ya vifungo vyao.

Liyumba alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia katika shtaka la kutumia madaraka vibaya wakati akiwa mtumishi wa umma.

Kundi lingine litakalofaidika na msamaha huu ni la wafungwa wagonjwa wa ukimwi, kifua kikuu na saratani na ambao wanaelekea kuwa katika siku za mwisho za maisha yao.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, amesema Rais Kikwete amewasamehe wafungwa wenye ukimwi, kifua kikuu na saratani.
Endelea kusoma habari hii.....................
Best Blogger Tips
Dhulma nchini Libya kufanyiwa uchunguzi

Via BBC

Kundi la maafisa kutoka Umoja wa Mataifa limetumwa mjini Tripoli kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Libya.

Jopo hilo liliteuliwa na baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa punde tu utawala wa Libya ulipoanza kushambulia waandamanaji wanaompinga kanali Muammar Gaddafi.

Serikali ya Libya imesema itashirikiana na jopo hilo la wachunguzi ambalo pia litachunguza madai ya dhulma zilizotekelezwa na waasi na majeshi ya Nato.

Kuna taarifa kuwa tangu maandamano ya kumpinga Kanali Gaddafi yaanze watu wametoweka, wengine wameteswa na hata kuuawa.

Kamishna wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay alisema kuwa huenda uhalifu dhidi ya binadamu unafanyika nchini Libya tangu mzozo huo uanze.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema zaidi ya watu elfu moja wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika mapigano hayo.

Meli zimekuwa zikiwasafirisha watu waliojeruhiwa hadi mjini Benghazi kupata huduma za matibabu.

Monday, April 25, 2011

Best Blogger Tips
Asakwa na polisi kwa kumlawiti mwanafunzi

Via Majira

POLISI jijini Mwanza wanamsaka mwanamume mmoja akidaiwa kumwingilia kinyume cha maumbile mwanafunzi wa kike wa Shule ya Msingi Mahina katika Wilaya ya
Nyamagana Jijini Mwanza.

Tukio hilo lilitokea Aprili 20 mwaka huu majira ya saa 12:00 katika eneo la Gedeli Mahina ambapo mtu huyo alimwingilia mwanafunzi huyo na kumsababishia maumivu makali sehemu hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Bw. Nonosius Komba alisema mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 11 alilawitiwa na mtu mmoja asiyemfahamu jina bali anamtambua kwa sura ambaye ni wa kabila la Kimasai.

Alisema mara baada ya kufanya kitendo hicho, mtuhumiwa huyo alitokomea kusikojulikana ambapo jeshi la polisi linaendelea kumsaka ikiwa ni pamoja na kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
Best Blogger Tips
Babu Loliondo afiwa na mwanaye

Via Mwananchi

 MCHUNGAJI Ambilikile Mwasapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu huko Samunge, Loliondo amefiwa na mtoto wake wa kiume jana. Kutokana na msiba huo, Serikali imesitisha tena tiba anayotoa hadi Ijumaa.

Habari zilizopatikana kijijini hapo jana zimeeleza kuwa mtoto huyo, Jackson Mwasapila (43), alifariki dunia jana asubuhi, nyumbani kwake wilayani Babati, Mkoa wa Manyara.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali aliliambia gazeti hili jana kuwa kutokana na msiba huo, Mchungaji Mwasapila atasitisha tiba kuanzia leo jioni.Mkuu huyo wa Wilaya alifika Samunge jana hiyo hiyo akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, kumpa pole mchungaji huyo.

"Tunapenda kutangaza rasmi kuwa huduma zitasitishwa hadi Ijumaa na tunaomba watu walio mbali wasije hadi Ijumaa," alisema Lali.Alisema Serikali itashiriki msiba huo na inajiandaa kutoa msaada wa kumpeleka Mchungaji Mwasapila, Babati kushiriki msiba huo.

Mchungaji azungumziakilichomsibu mwanaye
 Akizungumza na gazeti hili kijijini hapo jana, Mchungaji Mwasapila alisema mtoto wake huyo alifariki jana saa 5:00 asubuhi katika Hospitali ya Wilaya ya Babati baada ya kuugua malaria ghafla.

"Taarifa ambazo nimezipata ni kuwa Jackson alikuwa anasumbuliwa na kichwa na baada ya kufikishwa hospitali, alifariki dunia," alisema Mchungaji Mwasapila.Mchungaji huyo, alisema Jackson ni mtoto wake wa tatu kati ya sita alionao.

Wagonjwa wampa pole

Baadhi ya wagonjwa waliokwenda Samunge jana kupata tiba, walitoa salamu za rambirambi kwa Mchungaji Mwasapila kutokana na msiba huo.Hata hivyo, wakati wagonjwa hao wakimpa pole, mchungaji huyo alikuwa akiendelea kuwapa dawa kama kawaida.

Mchungaji Mwasapila alisema ameamua kuendelea na kutoa tiba kwa wagonjwa hao ili kuwasaidia watu ambao tayari walikuwa wamefika Samunge na wengine watakaofika leo.

"Kesho (leo) jioni nitafunga na kuelekea Babati kwa ajili ya msiba wa mtoto wangu na kama alivyosema mkuu wa wilaya, tutaendelea na tiba Ijumaa," alisema Mchungaji Mwasapila.

Friday, April 22, 2011

Best Blogger Tips
IJUMAA KUU: Maaskofu wahofia hatima ya nchi

Via Mwananchi

MAASKOFU wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo Tanzania, jana waliitumia Ibada ya Ijumaa Kuu ambayo ni ya kukumbuka mateso ya Yesu Kristo, wakielezea wasiwasi wao juu ya hatima ya nchi kutokana na kugubikwa na vitendo vya rushwa na suala zima la utoaji wa haki kwa wananchi.
Waliwataka waumini wa Kikristo na Watanzania kwa ujumla kuitumia Sikukuu ya  Pasaka kurejea vitendo vyema ikiwa ni pamoja na kuheshimiana na kudumisha amani.

Waliozungumza jana ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Dk Valentino Mokiwa, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Yuda Thadeus Ruwa’ichi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), Askofu David Mwasota, Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Nestory Timaywa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigirwa.

Askofu Ruwa’ichi alilia na haki

Kwa upande wake, Ruwa’ichi ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, alisisitiza umuhimu wa Serikali na dola kutoa haki kwa umma akisema: “Siyo lazima kelele ya wengi inaporindima ndiyo haki inatendeka.”

Akihubiri kwenye ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania, Parokia ya Bugando, Askofu Ruwa’ichi alisema kila mmoja anawajibika kusimamia ukweli ili kuungana na Kristo katika kutenda haki.

Alisema watendaji wa Serikali wanapaswa kujihoji ni kwa kiasi gani wanatimiza mapenzi ya Mungu katika kuwatendea wenzao haki.
Endelea kusoma habari hii......................

Wednesday, April 20, 2011

Best Blogger Tips
Waasi wakataa kuweka silaha chini Libya

Via BBC

Upinzani nchini Libya, umekataa pendekezo la hivi punde kutoka kwa serikali ya Kanali Muammar Gaddafi, la kuwataka kuweka silaha chini.

Msemaji wa baraza la mpito linalodhibiti mji wa Benghazi, amesema kuwa wapiganaji wa upinzani wataendelea na vita dhidi ya vikosi vya Kanali Gaddafi.

Msemaji wa kundi hilo la upinzani, Abdul Hafeel Ghoga, amewaambia waandishi wa habari kuwa Kanali Gaddafi, amependekeza mkataba huo wa kusitisha mapigano, kwa sababu wanajeshi wake wanaendelea kuangamizwa kwenye mashambulio ya anga yanayotekelezwa na wanajeshi wa NATO.

Lakini Bwana Ghoga, amesema upinzani hauwezi kusimamisha mashambulio yake dhidi ya wanajeshi wa serikali.

Akizungumzia pendekezo la kuafikiwa kwa mkataba wa kisiasa ambao utaruhusu kiongozi wa Libya, Kanali Gaddafi na familia yake kusalia nchini humo, Ghoga amesema hilo haliwezekani.
Msemaji huyo wa upinzani amesema, kwa sasa hakuna mzozo wa kijeshi nchini humo.

Amesema kuongezwa kwa mashambulio ya anga yanayofanywa na wanajeshi wa NATO, kumeimarisha hali kwa waasi wanaopinga serikali ya Gadaffi.

Huku hayo yakijri, mtengenezaji filamu mmoja aliyeteuliwa kuwania tuzo la filamu maarufu kama Oscars, ameuawa mjini Misrata.

Tim Hetherington, ambaye ana uraia wa Uingereza na Marekani aliuawa kwenye shambulio kati kati mwa mji huo ambao umeendelea kushuhudia mapigano makali kati ya wanajeshi watiifu kwa Kanali Gaddafi na wale wa waasi.

Hetherington alikuwa mmoja wa wasimamzi wa filamu ya Resrepo iliyotengenezwa kuhusu vita vya Afghanistan.

Filamu hiyo iliteuliwa kuwania tuzo la oscar mwaka huu.
Mwandishi mwingine Chris Hondros, raia wa Marekani ambaye alikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa kwenye shambulio hilo, aliaga dunia akipokea matibabu hospitalini.
Ripoti zinasema mwandishi mwingine wa habari pia alijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Monday, April 18, 2011

Best Blogger Tips
Vita ya ufisadi yageukia vyama vya siasa

Via Mwananchi

VYAMA sita vya siasa vyenye wawakilishi bungeni, vinadaiwa kuwa vimeshindwa kuwasilisha taarifa za hesabu kuhusu matumizi ya ruzuku ya jumla ya Sh17.14bilioni kwa mujibu wa sheria.Vyama hivyo ambavyo vinapata ruzuku inayotolewa na Serikali ni pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Tanzania Labour (TLP), NCCR-Mageuzi na UDP.Tuhuma hizo zimo kwenye Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inayoishia Juni 30, 2010.

CAG ametoa ripoti hiyo baada ya sheria, kwa mara ya kwanza kumpa mamlaka ya kuvikagua vyama vya siasa ambavyo mahesabu yao, yanapaswa kuwasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania.

"Taarifa za fedha kwa malipo ya ruzuku ya Sh17,146,819,904 kwa vyama vya siasa mbalimbali hazikuwasilishwa na vyama husika katika Ofisi ya Msajili," ilisema Ripoti ya CAG katika fungu la 27 kuhusu Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na matumizi ya ruzuku.

Takwimu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa zinaonyesha kuwa CCM kinapata ruzuku ya asilimia 70, CUF asilimia 20, Chadema asilimia nane na NCCR-Mageuzi, UDP na TLP vinagawana asilimia mbili.

Katika mahesabu ya kawaida, kati ya fedha hizo Sh 17.14 bilioni, CCM itakuwa imepata mgawo wa Sh12bilioni, CUF Sh 3.43bilioni, Chadema Sh1.37bilioni na vyama hivyo vitatu kwa asilimia mbili yao vikipata Sh343milioni.

Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alipoulizwa na gazeti dada la The Citizen kwa simu alisema asingeweza kuzungumzia jambo hilo nyeti kwa mawasiliano ya simu kwani anahitaji kukaa na kulifanyia kazi kwa kina.

Hata hivyo, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovic Utouh katika ripoti hiyo alisema kitendo hicho ni kinyume cha kifungu 14 (1) na (3) cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992.


Sehemu ya kifungu hicho inasema, "Chama chochote cha siasa ambacho kina usajili wa kudumu, kinapaswa kutunza hesabu zake vizuri za ruzuku na kuwasilisha kwa Msajili."

Kifungu hicho kinaendelea: "Kwa kutumia taarifa ya mwaka ya ukaguzi wa hesabu uliofanywa na mkaguzi anayetambulika kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu, huku ikiwa na tamko la mali zote zinazomilikiwa na chama hicho."

 Utouh alisema pia kwamba Sh56.9milioni zilitumika na msajili huyo wakati hazikuhusiana na shughuli za vyama vya siasa.

"Jumla ya Sh56,180.44milioni zilitumika na Msajili wa Vyama vya Siasa wakati hazikuhusiana na shughuli za vyama vya siasa," alisema Utouh katika taarifa hiyo.

Mbali na tuhuma hizo, Utouh alisema kwamba kiasi cha Sh272.8milioni zilitumika kulipa deni la miaka ya nyuma la Bodi ya Udhamini ya chama cha UDP bila kuonyeshwa katika taarifa za fedha na kusema: "Malipo haya yanaathiri utendaji wa ofisi kwa mwaka wa sasa wa fedha."

UDP kinaongozwa na John Cheyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Alipoulizwa kuhusu fedha hizo, Cheyo alisema hajaisoma vyema ripoti hiyo na kuongeza kwamba atakuwa kwenye nafasi nzuri kuzungumzia hilo baada ya kuipitia kwa kina.

"Kwa sasa hivi itakuwa ni vigumu kuzungumzia ripoti hiyo wakati sijaisoma vizuri. Nitakuwa siko sahihi kama nitazungumza bila kuisoma. Nipe muda nisome kisha nitaweza kuizungumza," alisema.

Saturday, April 16, 2011

Best Blogger Tips
Zito aibua ufisadi mpya

Via Newhabari

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (CCM), Kabwe Zitto, ameibua ufisadi mpya na wa kutisha unaoonyesha kuwa zaidi ya Sh bilioni 48 zimetafunwa na wajanja.

Zitto alimbana Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jana, ambapo alisema kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, fedha hizo zilipotea katika utaratibu wa mpango wa kuhuisha uchumi (stimulus package) ambapo Bunge lilipitisha bajeti ya dharura ya Sh trilioni 1.7.

Zitto aliuliza: “Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu, katika bajeti ya mwaka 2009/2010 Serikali ilileta Bunge mapendekezo ya kutenga zaidi ya shilingi trilioni 1.7 kwa ajili ya kuhuisha uchumi (stimulus package) na Serikali iliahidi hapa Bungeni ya kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atafanya ukaguzi maalumkwenye eneo hili.

“Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ametoa taarifa yake. Katika taarifa yake pamoja na kuonyesha kwamba kuna zaidi ya shilingi bilioni 48 ambazo ameshindwa kuzithibitisha kama zilitoka kwa taratibu zinazotakiwa. Lakini pia amesema kwamba Serikali imemnyima taarifa muhimu ikiwemo orodha ya watu na makampuni ambayo yalifaidika na mpango huu. Mheshimiwa Waziri Mkuu unatoa kauli gani kuhusu suala hili?”

Baada ya hoja hiyo ya Zitto, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema: “Mheshimiwa Spika, sijui Mheshimiwa Kabwe maana mimi ndio Waziri Mkuu, ndio ninayeshughulika na masuala ya Serikali kwa upana wake. Kwa bahati mbaya sana hiyo taarifa kwamba aliomba baadhi ya taarifa kutoka Serikali tukamnyima mimi nilikuwa sijazipata na kwa sababu taarifa hizo na mimi nimezipata juzi yaani kwa maana ya ma-book yale na so long ndio nazipitia labda nipe nafasi nikishapata nafasi ya kuipitia then tuta-take up issue seriously kwa sababu hatuna sababu ya kumnyima yeye ndio Mkaguzi wa Hesabu na kwa nini tusiseme hapana.”
Endelea kusoma habari hii...............

Thursday, April 14, 2011

Best Blogger Tips
Colorado couple thought they were millionaires

The Spragues--a retired couple in Pueblo, Colo.--have better reason than most of us to ponder the old saw, "easy come, easy go." For an exhilarating hour or so last weekend, the Spragues opened up the Sunday paper to discover that they had won more than $4 million in the Colorado Lotto.

There was just one problem, however: The newspaper had printed the wrong numbers.

Dorothy Sprague told The Lookout she was in the kitchen when her husband, a retired teacher and plumbing shop owner, checked the numbers in the Sunday edition of the Pueblo Chieftain.
"He was checking them off and he says, 'Oh at least I got three--we got a winner this time! Oh wow, there's four, five, six.' And I said no, that can't be right. He said 'Come look,' because I was still doing things in the kitchen and then sure enough it was all six numbers.
I couldn't wrap my mind around 4 million. I just said, 'No that's unreal.' "

Sprague and her husband Jim decided they wouldn't tell anybody until they were sure, except for their daughter, who was home visiting.
"We don't do the Internet or the computer or anything and my husband says, 'I got to tell somebody,' so we told her. We were discussing it and talking and then one of us said, maybe there's more than one winner. And she said, 'Why I don't check on the Internet?' So she went on her laptop and she checked the numbers and they were wrong."
Read the full article

Wednesday, April 13, 2011

Best Blogger Tips
Namkuta Adamu Lusekelo 'Ninja'

Makala ya Fred Macha

LABDA si wasomaji wengi wa Kiswahili wanaomfahamu mwandishi wa habari wa siku nyingi aliyefariki dunia wiki iliyopita, Adam Lusekelo Mwakang’ata.

Nilimfahamu Lusekelo mwaka 1970 wakatu tunasoma wote  sekondari. Tulimkatia jina la mbabe mpiganaji, yaani Njinja Maloni. Adam “Njinja” alikuwa bondia  na baadaye kujifunza Shotokan karate ( toka Korea) wakati akisomea uandishi wa habari, Nairobi. Aliwahi pia kupanda  mlima Kilimanjaro mara kadhaa.

Bahati mbaya alipoacha mazoezi na kujisahau (kwa pombe kupindukia ) akakumbwa na kisukari. Nikiwa rafiki yake wa utotoni  nilishtuka nilipomwona alivyokonda  mara ya mwisho mwaka juzi, mjini Dar es Salaam.

Ulikuwa mfano wa tabia yake ya masihara yaliyojaa ujumbe. Usingeacha kucheka ulipokutana na  Adam Lusekelo. Alikuwa chizi kupindukia na ucheshi wake ulijionyesha katika mamia ya makala za kejeli alizoziandika   katika safu ya “With A Light Touch.”
 Miaka ya mwisho alifungua pia blogu (“Adam Lusekelo On Line”) aliyoendeleza mada zake. Adam Lusekelo hakuwa mwoga. Ingawa marehemu babake alikuwa zamani katika serikali (tulipofahamiana 1970, Mzee Aaron Mwakang’ata, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha), Adam hakuhofia kuwasakama viongozi mafisadi. Kinyume cha baadhi ya watoto wa vigogo wanaofunga macho na kufaidi matunda ya wazazi wao, alitumia nafasi hiyo kukemea ufuska.

Novemba 14, 2010 aliandika : “Jini Hatimaye Limeamka” ..akichambua  namna vijana wa Kitanzania walivyochoshwa na wanasiasa waongo.
“Hao wanaolifanya Bunge hoteli ya kupangisha yenye hewa safi ya baridi itabidi waamshwe na kupigwa mateke makalioni. ”
Adam aliandika mada za kila aina, ikiwemo kumshauri mwigizaji Steve Kanumba aliyesutwa kwamba hajui Kiingereza alipoingia Big Brother Afrika Kusini, 2009. Kinachofurahisha, makala hii  ni namna anavyochangamsha hoja akitumia Kiingereza chepesi. Kinyume cha waandishi wanaojifaragua kwa lugha ya mawe, iliyojaa maneno magumu, aliandika sentensi fupi za utani, utani...

Anamkumbusha Kanumba juu ya watu wengi kukuonea wivu hasa mtu anapofaulu katika maisha. “Ukibahatika kufahamika, wapambe watataka kuimanya hata rangi ya chupi yako,” anasema.

Hata mwanamke unayekwenda naye atachunguzwa.  “Wataanza kusema sura yake mbaya kama jini, kwamba miguu yake mirefu kama ya twiga. Ndo’ ubinadamu huo.”
Adam Lusekelo aliendeleza lugha ya uandishi Tanzania akitumia Kiingereza safi chenye utamaduni wa Afrika Mashariki. Unapokisoma Kiingereza chake ni kama kumsikiliza Mswahili akiongea lugha fasaha ya kigeni bila kujisahau atokapo. Anakumbusha enzi  Mzee John Malecela alipokuwa balozi wetu Umoja wa Mataifa akiongea Kiingereza fasaha  cha lafidhi ya Kigogo na Kiswahili. Siri ya ujuzi wake nini?
 Kila nilipoongea naye, Adam, hakuacha kunitajia kitabu fulani alichokuwa akisoma; alikuwa mwanafunzi mzuri wa fasihi na lugha, jambo linalozidi kudhoofika miongoni mwa waandishi chipukizi leo Bongo.
Endelea kusoma habari hii.................
Best Blogger Tips
Mubarak atiwa kizuizini kwa siku 15

Via BBC

Mwendesha mashtaka wa Misri ameamuru kutiwa kizuizini kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak, kabla ya kufanywa uchunguzi juu ya madai ya rushwa na unyanyasaji.

Bw Mubarak, mwenye umri wa miaka 82, yuko hospitalini baada ya kuripotiwa kuwa na matatizo ya moyo. Televisheni ya taifa ilisema amri ya kutiwa kizuizini itatekelezwa kwa muda wa siku 15.

Watoto wake wa kiume Alaa na Gamal nao pia wametiwa kizuizini wakihusishwa na madai ya kuhusika na rushwa na ghasia.

Bw Mubarak aliachia madaraka mwezi Februari baada ya maandamano kufanyika ya kupinga utawala wake.
Tangu wakati huo, maelfu ya waandamanaji wamekuwa wakifanya maandamano kila Ijumaa kwenye eneo la wazi la Tahrir mjini Cairo, wakitaka ashtakiwe.

Takriban watu 360 wanadhaniwa kuuawa wakati wa maandamano, kufuatia polisi kufyatua risasi kwa ajili ya kuwatawanya waandamanaji.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema idadi hiyo ni kubwa zaidi.

Pia kuna madai yaliyoenea kuhusu rushwa na utumiaji mbaya wa madaraka katika kipindi cha miaka 30 ya uongozi wake.

Tuesday, April 12, 2011

Best Blogger Tips
Rockets sign C Cousin; recall C Hasheem Thabeet

Via USA TODAY

HOUSTON (AP) — The Houston Rockets have signed center Marcus Cousin to a non-guaranteed contract and assigned him to Rio Grande Valley, their developmental league affiliate.

The Rockets also recalled center Hasheem Thabeet from Rio Grande Valley and waived forward DeMarre Carroll.

The 6-foot-11 Cousin played at Houston. Last month, he signed a 10-day contract with Utah and played in four games. Cousin was a D-League All-Star this season, averaging 14.7 points, 8.6 rebounds and 1.16 blocks in 38 games for the Austin Toros.

The 7-3 Thabeet was assigned to Rio Grande Valley on March 21 and averaged nine points, 7.7 rebounds and 2.4 blocks in seven games. Acquired in a deadline deal with Memphis, Thabeet has played in two games with the Rockets.

The 6-8 Carroll also joined Houston in the deadline deal and played in four games.
Best Blogger Tips
Hosni Mubarak hali mahututi hospitalini Cairo

Via BBC

Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak amelazwa hospitalini akiwa katika hali mahututi mjini Cairo. Awali MUbarak alilazwa katika hospitali moja eneo la kitalii la Sharm Sheikh.

Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kuwa alipata mshtuko wa moyo alipokuwa akihojiwa na wachunguzi juu ya mauaji yaliyofanywa dhidi ya waandamanaji nchini Misri.

Televisheni ya kitaifa ya Misri imenukuu baadhi ya madaktari wakisema kuwa Muabarak alikataa kula wala kunywa baada ya kuagizwa kufika mbele ya mwedesha mashtaka mkuu, pamoja na wanawe, yapata siku mbili sasa.

kwa sasa anatibiwa magojwa ya moyo katika hospitali ya Sharm Al sheikh, ambapo madakitari wanasema kuwa anaendelea vyema.

Usalama wa hali ya juu umewekwa katika hospitali. Bwana Mubarak aliye na umri wa miaka 82 aliripotiwa kuzorota afya yake baada ya upasuaji wa moyo aliyo fanyiwa nchini Ujerumani mwaka jana.
Hata hivyo marafiki zake wa karibu zaidi wamesisitiza kuwa hali yake iko shwari.

Mamia ya waandamanaji walisalia katika hospitali hiyo baada ya maandamano ya ijumaa, na wamesisitiza kuwa wataendelea kuketi hapo hadi pale kiongozi huyo atafunguliwa mashtaka.

Wakati huo huo jeshi pamoja na polisi wameizingira bustani ya Taharir ambapo kumekuwa na waandamanaji wanaoshinikiza kuwepo na utawala wa kiraia pamoja na kushtakiwa kwa watawala waliong'olewa madarakani.

Monday, April 11, 2011

Best Blogger Tips
Pangua pangua CCM yawasomba vigogo

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), imetangaza safu mpya ya uongozi wa juu wa chama hicho watakaoongoza Sekretarieti yake na Kamati Kuu (CC) huku vigogo wengi wakianguka na kisha kutoa siku 90 kwa watuhumiwa wa ufisadi kujiondoa wenyewe NEC ya chama hicho vinginevyo watawajibishwa.

Katika uteuzi huo, Wilson Mkama amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Yusuf Makamba. Mkama atasaidiwa na Naibu Makatibu Wakuu (Bara na Visiwani), John Chiligati na Vuai Ali Vuai. Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi ni Nape Nnauye, huku, Mwigulu Mchemba akichaguliwa kuongoza Idara ya Fedha na Uchumi. Mkuu wa Oganaizesheni ni Asha Abdallah Juma na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Januari Makamba.

Waliochaguliwa kuunda Kamati Kuu ni Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji, Dk Abdallah Kigoda, Pindi Chana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Constancia Buhiye, William Lukuvi na Steven Wassira.

Kwa upande wa Zanzibar, waliochaguliwa ni Dk Hussein Mwinyi, Dk Maua Daftari, Samia Suluhu Hassan, Shamsi Vuai Nahodha, Omar Yusuf Mzee, Profesa Mbarawa Mnyaa na Muhammed Seif Khatib.

Mwenyekiti wa CCM kwa madaraka ya kikatiba aliwateua wajumbe 10 kuingia NEC ambao ni Anna Abdallah, Peter Kisumo, Mwingulu Mchemba, Wilson Mkama, Januari Makamba, Juma Shamhuna, Dk Emmanuel Nchimbi na Haji Omar Kheri.

Miongoni mwa majina yaliyokuwa yamependekezwa ni Kingunge Ngombale-Mwiru, Beno Malisa, Mussa Azzan Zungu, Shamsa Mwangunga, Profesa Athman Kapuya, William Kusila na Anthony Diallo.

Akizungumzia kile ambacho kimekuwa kikitajwa kama kujivua gamba kwa chama hicho, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alisema mkutano huo umefikia uamuzi kwamba wote wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi wajiondoa wenyewe kwenye uongozi chama na iwapo watakaidi watawajibishwa.

Rais Kikwete alisema hatua zilizochukuliwa kujiuzulu kwa Sekretarieti na Kamati Kuu, ni za mwanzo na hakuna tena sababu ya chama kusubiri ushahidi kama ilivyokuwa mwanzo.

Akifunga kikao cha NEC-CCM, jana usiku mjini hapa, Rais Kikwete alisema hivi sasa hatua zitakuwa zinachukuliwa haraka dhidi ya watuhumiwa pindi hali inapoanza kuchafuka kwenye jamii: “Tumeanza kuchukua hatua na huu ni mwendelezo, tunaowatambua tuwabane kwa kuwataka wajiuzulu na pale wanapokataa tusichelee kuwawajibisha.”

Alisema wamekubaliana kuzingatia maadili na kwamba kumekuwapo na utovu wa maadili ambavyo ni miongoni mwa mambo yaliyopoteza haiba ya chama.

Kuhusu daftari la wanachama, Rais Kikwete aliwataka watendaji wa chama hicho kuliandaa vizuri na uchaguzi utapokaribia lifungwe kwa sababu lilitumika vibaya katika uchaguzi uliopita na limewaongezea watu walionuna.

Alisema wamekubaliana kuunda baraza la ushauri la wazee, ambalo litakuwa na ajenda zake badala ya sasa kuitwa na kufuata ajenda za NEC au CC: “Tumekubaliana ngazi yetu muhimu ni shina na tawi na wajumbe wa NEC watakuwa wanachaguliwa wilayani ambako ndiko watu waliko,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Turudi kwenye masharti na matakwa ya Katiba yetu, tumeteleza mahali wagombea wananunua kadi wanakwenda wanawagawia watu ambao wako tayari kuwapigia kura wao, tumekuwa na mkusanyiko wa watu wasio waumini.”

Alisema kazi iliyopo mbele yao hivi sasa ni kujenga chama na kwamba wamekubaliana kujibu matusi ya wapinzani badala ya kutuma ujumbe mfupi wa simu kwake.

Pia alisema wamekubaliana kuzunguka kueleza ukweli wa Muswada wa Mabadiliko ya Katiba, ili kuondoa upotoshaji unaofanywa na wapinzani.

Awali, aliyekuwa katibu mkuu Makamba akiaga alisema Sekretarieti aliyokuwa akiiongoza imejiuzulu kwa maslahi ya chama huku akibainisha kwamba alikataa kujiuzulu peke yake.

Alisema anakwenda kutayarisha makao na walioingia watambue kuna siku watamfuata, huku akitoa mifano ya Yesu alivyokuwa akiaga wanafunzi wake: “Hata nyinyi mtastaafu mtatukuta tumewatayarishia makao,” alisema.

Alimtaka Rais Kikwete kutomsahau na kwamba pale atakapoona anafaa kama ni kwenda kujibu matusi yupo tayari kufanya hivyo.

Taarifa zilizopatikana jana zilisema kwamba Rais Kikwete leo atazungumza na watumishi wote wa CCM waliopo Makao Makuu ambao morali ya watumishi hao ilikuwa umekufa.
Source: Mwananchi
Best Blogger Tips
Mkama kuvaa viatu vya Makamba

Via HabariLeo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza safu yake mpya ya uongozi wa juu akiwemo Katibu Mkuu mpya, Kamati Kuu na Sekretarieti mpya.

Katibu mpya wa CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ameitangaza safu hiyo usiku huu katika ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

Katika mabadiliko hayo makubwa ya uongozi CCM, Wilson Mkama ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM kuchukua nafasi ya Yusuf Makamba.

Mkama amekuwa kiongozi kwa muda mrefu Serikalini , na kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers (TSN).

Aliyekuwa Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM, John Chiligati sasa anakuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara kuchukua nafasi ya George Mkuchika.

Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM Zanzibar ni Vuai Ali Vuai, Januari Makamba anakuwa Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Mwigulu Mchemba anakuwa Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Aisha Abdallah Juma anakuwa Katibu wa NEC Oganaizeshi, na Nnauye anakuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.

Kwa mujibu wa Nnauye, Kamati Kuu mpya ya CCM ina wajumbe 14, wajumbe kutoka Tanzania Bara ni Abdulrahman Kinana, Zakia Megji, Abdallah Kigoda, Pindi Chana, Stephen Wassira, Costansia Bugie na William Lukuvi.

Wajumbe kutoka Zanzibar ni Dk. Hussein Mwinyi, Dk. Maua Daftari, Samia Suluh Hassan, Shamsi Vuai Nahodha, Omary Yusuf Mzee, Profesa Mnyaa Mbarara, na Mohamed Seif Khatib.

Katika kujiimarisha, Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho, amewateua wajumbe saba wa NEC ili kukamilisha idadi ya wajumbe 10 anaoruhusiwa kuwateua.

Walioteuliwa ni Anna Abdallah, Peter Kisumo, Mwigulu Mchemba, Januari Makamba, Wilson Mkama, Ali Juma Shamhuna, na Dk. Emmanuel Nchimbi.
Best Blogger Tips
Majeshi ya Ufaransa 'yamkamata Gbagbo'

Via BBC

Mshirika wa Gbagbo alisema, wanajeshi wa Ufaransa wamemkamata kiongozi wa Ivory Coast Laurent Gbagbo kutoka kwenye makazi yake na kumkabidhi kwa upinzani.

Inaripotiwa kuwa waliingia baada ya vifaru vya Ufaransa kuingia katika makazi yake kwenye mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan, kufuatia mashambulio ya helikopta ya Ufaransa na Umoja wa Mataifa.

Bw Gbagbo alikataa kukabidhi madaraka kwa Alassane Ouattara, anayetambuliwa kimataifa kuwa mshindi wa urais nchini humo.

Majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kutunza amani yanayashutumu majeshi ya Bw Gbagbo kuhatarisha maisha ya raia.

Msemaji wa Rais Toussaint Alain aliliambia shirika la habari la Reuters kutoka Paris, "Gbagbo amekamatwa na majeshi maalum ya Ufaransa nyumbani kwake na amekabidhiwa kwa wapinzani."

Sunday, April 10, 2011

Best Blogger Tips
Mukama, Kinana watajwa kubeba jahazi CCM

Via Mwananchi

SIKU moja baada ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu pamoja na sekretarieti yake, baadhi ya makada wa chama hicho tawala wanatajwa kujaza nafasi za utendaji.Taarifa kutoka ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu jana usiku mjini hapa zilidai kuwa Wilson Mkama ndiye aliyepewa jukumu la Ukatibu Mkuu wa CCM huku msaidizi wake kwa upande wa Bara akitajwa kuwa ni Abdulrahman Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa Fedha na Uchumi, Zakia Meghji na Katibu wa Oganaizesheni, Dk Rehema Nchimbi.

Kuhusu Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, inadaiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwasilisha jina la Saleh Ramadhan Feruzi, lakini lilikataliwa na wajumbe kutoka visiwani.

Sekretarieti iliyojiuzulu ilikuwa inaundwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, Naibu Makatibu Wakuu bara na visiwani; George Mkuchika na Feruzi, Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati, Katibu wa Fedha na Uchumi, Amos Makala,Katibu wa Oganaizesheni, Kidawa Saleh na Mambo ya Nje, Bernard Membe.

Mkama akishirikiana na Profesa aliyefahamika kwa jina moja la Luhanjo, ndiyo waliofanya tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kupendekeza kwamba lazima baadhi ya wanachama watoswe kuokoa chama hicho.

Inadaiwa kuwa miongoni mwa ajenda za kikao hicho ni kujivua gamba ambayo hatua ya kujiuzulu kwa sekretarieti na kamati kuu ni utekelezaji wake.

Inadaiwa kwamba kujiuzulu kwa Kamati Kuu kulitokana na mvutano wa wajumbe ambao walionyesha kugawanyika, huku kundi moja likitaka Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa CC, Rostam Aziz, Mbunge wa Bariadi Mashariki na mjumbe wa kamati hiyo, Andrew Chenge wajiuzulu na jingine likipinga.

Baada ya mvutano mkali wa wajumbe hao na kuchukua muda mrefu, inadaiwa Rais Kikwete aliilazimisha kamati nzima kujiuzulu.Awali, ilidaiwa kuwa ajenda hiyo ya kuwataka wajumbe hao wawili wajiuzulu ingewasilishwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu, huku kundi linalodaiwa kupinga ufisadi likitaka wafukuzwe uanachama.

WanaCCM Dodoma wachekelea
Katika hatua nyingine, kujiuzulu kwa Sekretarieti na Kamati Kuu ya CCM kumeonekana kuwakuna baadhi ya wananchi na wafanyakazi wa chama hicho hasa wale wa Makao Makuu, Dodoma.Baadhi ya wafanyakazi hao na wananchi wakiwa kwenye makundi, walikuwa wakijadili hatua na kupongeza uamuzi huo na kwamba, hivi sasa chama hicho kimeamua.

“Tunaomba waandishi msituzibe tunataka kuwaona viongozi wetu, maana leo siyo sura tulizozoea wamejivua gamba,” walisikika wafanyakazi hao wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete alipokuwa akiingia kufungua mkutano wa Halmashauri Kuu.Tofauti na kawaida yake ya misemo na uchekeshaji, sura ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba ilionekana ya upole wakati akimkaribisha Rais Kikwete.
Best Blogger Tips
Israel na Hamas kusitisha mashambulio

Via BBC

Israel na kikundi cha Wapalestina cha Hamas, wanasema wako tayari kusitisha mashambulio ikiwa na upande wa pili utafanya vivyo.

Msemaji wa Hamas alieleza kwamba wao hawataki mashambulio kuzidi.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Ehud Barak, alisema nchi yake iko tayari kukubali mapigano kusita endapo wapiganaji wa Gaza watamaliza mashambulio.

Ndege za Israel zimeuwa watu kama 20 katika eneo la Gaza katika majuma ya karibuni; wakati inaarifiwa kuwa wapiganaji wa Kipalestina wamerusha makombora zaidi ya mia moja eneo la kusini la Israel.

Pande zote mbili, Israel na Hamas, zimelaumiana kwa kuanza mashambulio hayo, ambayo yanasemekana kuwa makubwa zaidi tangu mashambulio ya Israeli dhidi ya Gaza, zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Friday, April 8, 2011

Best Blogger Tips
Bunge halina uwezo kutunga katiba mpya

Via Mwananchi

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Othman Masoud amesema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halina uwezo wa kutunga Katiba mpya, bali kuifanyia marekebisho iliyopo."Bunge la Jamhuri halina uwezo wa kutunga Sheria ya Katiba hili ni jambo la msingi sidhani Zanzibar na watu wake kama watakubali kuvunja Katiba," alisema.

Masoud alisema hayo jana akitoa mchango wake katika mjadala wa maoni ya Muswada wa Sheria wa Mapitio ya Katiba unaoendeshwa na Kamati ya Bunge, Sheria na Katiba ya Bunge la Muungano
uliofanyika katika Hoteli ya Bwawani mjini hapa.

Alisema msingi wa hoja yake unatokana na Kifungu cha 98(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano kinachoeleza. Kifungu hicho kinasema: "Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii au masharti yoyote ya Sheria yoyote yanayohusika na jambo lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika Orodha ya Pili kwenye Nyongeza ya Pili iliyoko mwishoni wa Katiba hii, utapitishwa tu iwapo utaungwa mkono kwa kura za Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Zanzibar."

Orodha hiyo ya pili kwenye nyongeza ya pili iliyoko mwishoni wa Katiba inaeleza mambo ambayo mabadiliko yake yanahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Tanzania bara na theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Tanzania visiwani moja likiwa mambo ya muungano ambalo suala la Katiba ni mojawapo.

Alisema Bunge lililopo sasa haliwezi kutunga Katiba mpya, bali kazi yake ni kurekebisha hivyo linatakiwa liwepo Bunge jingine ambalo litakuwa maalumu kwa ajili ya kutunga Katiba.

Akiwasilisha madhumuni na sababu za muswada huo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta alisema umependekeza kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya nchi ya mwaka 2011 na unakusudia kuanzishwa kuweka masharti ya uanzishaji wa tume pamoja na sekretari kwa madhumuni ya kuendesha na kusimamia mchakato wa mabadiliko ya hayo.

Mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na mambo mengine, utaangalia chimbuko na uhusiano wa katiba iliyopo kwa kuzingatia uhuru wa wananchi na mfumo wa siasa.

Alisema pindi muswada huo utakapopitishwa na kuwa sheria, utakuwa na utaratibu wa kisheria utakaomwezesha Rais kuunda tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba na kuunda Bunge la Katiba kwa madhumuni ya kutunga Katiba mpya.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan Juma amesema muswada wa marekebisho ya Katiba ya Muungano una upungufu mwingi ukiwemo kutoshirikishwa kwa Serikali ya Zanzibar ambayo alisema haikushirikishwa kikamilifu ili kutoa maoni yake na wala haukupelekwa katika Baraza la Wawakilishi kupata maoni ya Baraza, hivyo haukustahiki kupelekwa Bungeni kujadiliwa kwani umekosa ridhaa za pande mbili.

“Muswada huo ni vyema kurudi serikalini na ukafanyiwe marekebisho na badala yake upelekwe katika Baraza la Wawakilshi ili upate ridhaa ya nchi mbili zilizoungana,” alisema Hamza.
Endelea kusoma habari hii.........................

Thursday, April 7, 2011

Best Blogger Tips
Nato yashambulia waasi inaowasaidia


Waasi mashariki mwa Libya wanasema majeshi yao yamepigwa na majeshi ya Nato katika shambulizi la anga - kwa bahati mbaya.

Madaktari mjini Adjabiya wameiambia BBC kuwa wapignaji wasiopungua 13 wa waasi wameuawa katika shambulio hilo.

Mwandishi wa BBC Wyre Davies ameripoti kuwepo kwa mkanganyiko katika viunga vya Adjabiya, huku majeshi ya waasi yakirudi nyuma na kutoa taarifa za kushambuliwa na ndege za Nato.

Hili ni tukio la tatu kutokea katika siku za hivi karibuni, kuhusiana na majeshi ya kimataifa yaliyopelekwa kulinda raia wa Libya.

Kamanda mmoja wa waasi ameiambia BBC kuwa aliona mabomu yasiyopungua manne yakianguka katika eneo la wapiganaji wa waasi.

Watu wengi wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa, amesema kamanda huyo.

Raia wanaripotiwa kukimbia mji wa Adjabiya kwa maelfu, kwa mujibu wa taarifa vya mashirika mbalimbali ya habari, kufuatia tetesi kuwa majeshi ya Gaddafi yanajiandaa kushambulia jiji.

Waasi walikuwa wakipeleka mizinga, magari ya ijeshi na mabomu ya kudungua ndege katika na uwanja wa mapambano, katikati ya miji ya Adjabiya na Brega, kwenye msafara wa zaidi ya magari 30.
Source: BBC

Wednesday, April 6, 2011

Best Blogger Tips
Bunge lawaka moto

Via Tanzania Daima
 
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa inayoongozwa na Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu na ile ya Mashirika ya Umma, zimeibua ufisadi wa kutisha ulioligeuza taifa kuwa shamba la bibi.

Kamati hizo ambazo zinaongozwa na Augustine Mrema (TLP), John Cheyo (UDP) na Zitto Kabwe (CHADEMA), ziliwasilisha taarifa zake za mwaka wa fedha wa 2008/2009 jana bungeni.

Katika halmashauri za wilaya nchini, ufisadi mkubwa umebainika kuwepo katika ununuzi wa spea za magari kwa kuongeza bei isiyo halisi, bei ya kughushi katika ununuzi wa mafuta, matumizi makubwa kwa ajili ya posho kuliko utekelezaji halisi wa miradi kama ya (TASAF), Mazingira na miradi mingine ya maendeleo.

Akiwasilisha taarifa ya kamati yake, Mrema alisema kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha 2008/2009, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga ilitumia sh milioni 2.9 kwa ajili ya kutengeneza pikipiki ya Kichina, iliyonunuliwa kwa bei ya chini kuliko ile iliyotumika kuitengenezea.

Alisema katika Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, kamati yake ilibaini kuwa halmashauri ilitumia sh milioni 15 kwa ajili ya kununua spea ya gari (Injector Pump ya Land cruiser had top).
“Lakini tulipofuatilia kwa kupiga simu kwenye duka lililouza spea hiyo, tuliambiwa bei yake ni sh milioni tatu,” alisema Mrema na kuwaacha wabunge wakibaki na mshangao.
Endelea kusoma habari hii..........................
Best Blogger Tips
Crowds Come Over Roads and by Helicopters for Tanzanian's Cure-All Potion

Via The New York Times

He’s a sensation in two countries. He’s snarled traffic for miles. He’s so popular that people have literally died waiting in line to see him.

Ambilikile Mwasapile, a 76-year-old retired pastor in rural Tanzania, has been offering a herbal concoction that he bills as a miracle potion that can cure just about any illness. In the past few weeks, tens of thousands of sick people have scrambled for a sip of his homebrewed drink. Some, apparently, have even flown in by helicopter.

On Monday, Tanzanian officials said that several dozen elderly and sick people had recently paid the price for joining the throngs.

“They died from the long queues,” said Isidore Shirima, a local official in Arusha, a town popular with tourists about six hours’ drive from the pastor’s village. “We’re not going to stop this, but we want to organize it better.”

Mr. Mwasapile, a former Lutheran preacher, lives in Samunge, a village in the middle of the savannah near the Kenya-Tanzania border. He began administering his miracle potion several months ago, and charges about 30 cents a cup. He says it can cure AIDS, cancer, diabetes, high blood pressure — you name it.

According to The Daily Nation, Kenya’s largest newspaper, Tanzanian officials have tested the herbs in the concoction and have verified that it is safe to drink. Mr. Mwasapile even has a Facebook page, listed under “Doctor, Arusha, Tanzania.”

Traditional healers are not considered fringe elements here. Sometimes, their teachings take macabre directions. In Tanzania, so many people believe, for example, that the body parts of albinos carry good luck, that dozens of albino people have been killed by thugs, who then sell their bones, hair and skin for thousands of dollars.

Mr. Mwasapile’s village is remote, with no good roads, and is hard to reach from any sizable town. It can take people from either side of the border days to reach him, with the elderly and sick camping out under trees on the way.

He issued a statement over the weekend saying that he planned to halt new arrivals to his village for a week, until he could serve everyone who was already camped out there.

Esther Lally, a recent college graduate living in Arusha, said she saw helicopters landing in the bush ferrying Tanzanian politicians to the village. She said that the potion worked.

“It’s all about faith,” said Mrs. Lally, who drank it herself two weeks ago. “If you believe that this works, it works. I saw many people there who had gotten better.”

Mrs. Lally wanted the potion to cure her ulcers, and she said she was already feeling better.
She said the drink “tastes like tea, without the sugar.”

Tuesday, April 5, 2011

Best Blogger Tips
Mama wa Rais Kabila apata kikombe

Via mwananchi

SASA ni dhahiri kwamba tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapila, imesambaa na kuvuka mipaka ya nchi na kuanza kuzigusa familia za vigogo.Juzi, mama mzazi wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Joseph Kabila alifika katika Kijiji cha Samunge, Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro na kupata kikombe cha dawa.

Mama huyo, Sifa Maanya Kabila aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Wasso, Loliondo majira ya mchana kwa siri na kwenda moja kwa moja katika Kijiji cha Samunge ambako alipata dawa pamoja na ujumbe wake wa watu wasiozidi saba, wengi wakiwa ni kina mama.

Mwananchi lilishuhudia Mama Sifa akipanda ndege katika Uwanja za Wasso juzi jioni pamoja na ujumbe wake wakiondoka huku wakisindikizwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali na maofisa wa usalama.
 Hata hivyo, Lali alipohojiwa na Mwananchi kuhusu ujio wa Mama yake Rais Kabila alisema, hakuwa akiwafahamu waliokuwamo kwenye ndege hiyo na kudai kwamba alifika kumwombea msaada wa usafiri ndugu yakealiyekuwa akienda mjini Arusha.

Lakini, chanzo chetu cha habari kilithibitisha pasi na shaka kwamba ndege hiyo ilikuwa na ujumbe wa mama mzazi wa Rais Kabila. "Ni watu kutoka Kongo (DRC) na wameambatana na mama mzito kidogo ambaye ni mama mzazi wa Rais Kabila, wengine nadhani ni watu waliomsindikiza tu," kilisema chanzo chetu cha habari kilichokuwa katika msafara huo.Ujumbe wa Mama Sifa Kabila ulipanda ndege hiyo ya kukodi kuelekea mjini Arusha ambako ulitarajiwa kupanda ndege nyingine kuendelea na safari.

Waandishi wa habari walipofika katika Uwanja wa Ndege wa Wasso hawakuruhusiwa kuusogelea ujumbe huo kutokana na kile kilichodaiwa kuwa, watu hao walikuwa katika "safari binafsi".Sifa Maanya Kabila ambaye ni mmoja wa wake watatu wa aliyekuwa Rais wa DRC, Hayati Laurent Kabila amekuwa nadra kuonekana hadharani tangu mumewe alipofariki dunia na mtoto wake kuchukua madaraka hayo, hajawahi kuzungumza hadharani wala mbele ya vyombo vya habari.Taarifa za maofisa wa Uhamiaji waliopo Samunge zinabainisha kuwa zaidi ya wageni 500, wengi wao wakiwa raia wa Kenya, wameshafika kijijini hapo kunywa dawa.
Endelea kusoma habari hii.................
Best Blogger Tips
Maajabu mapya Loliondo

*Mwizi wa fedha, simu apambana na muujiza
*Apigwa ganzi ya macho, atoa mali alizoiba

MAAJABU yanaendelea kutokea kwa Mchungaji Mstaafu Ambilikile Masapila, katika Kijiji cha Samunge, Loliondo; na safari hii ni kwa kijana anayetuhumiwa kuiba fedha na simu.

Kijana huyo aliyejulikana kwa jina moja la Joseph (28), alituhumiwa kuiba Sh 20,000 za Kenya, Sh 80,000 za Tanzania, simu na vitu kadha wa kadha kutoka katika gari walimokuwa raia wa Kenya.

Raia hao wa Kenya walifika kijijini Samunge kunywa dawa.

Wizi huo ulifanyika Aprili 2, mwaka huu, usiku baada ya watu wasiojulikana kuwapekua raia hao wa Kenya.

Taarifa zilimfikia Mchungaji Masapila na akatoa karipio akitaka vitu vilivyoibwa virejeshwe kwa wenyewe haraka.

Baada ya Ibada ya Jumapili Mchungaji Masapila alielekea hadi kwenye eneo ambalo amekuwa akitolea dawa na kuutangazia umma kuhusu taarifa za kuwapo wezi.

“Ndugu zangu wagonjwa, Kijiji cha Samunge tumevamiwa na majambazi, wezi ambao wamewaibia watu nawaomba waliofanya kitendo hicho kurejesha haraka vitu hivyo kabla Mungu hajaanza kuwaadhibu kwa mkono wake,” alinukuliwa akisema.

Alisema endapo aliyeiba angesita kurejesha mali alizoiba, basi umma ungemshangaa na kumtambua kwa matendo yake.

Ilielezwa kuwa ndani ya dakika 15 hivi, mama aliyekuwa na kijana mmoja (Joseph) alisikika akiomba msaada kwa kijana wake kwamba alikuwa akilalamika kupigwa na watu asiowaona.

Baada ya Mchungaji kumuona kijana huyo alimwamuru asalimishe vitu alivyokuwa ameiba ili ampatie dawa.

Kijana huyo aliendelea kulalamika kuwa amepoteza nuru, na wakati huo huo alianza kutoa vitu alivyokuwa ameiba.

Alitoa simu aina ya Blackberry, Sh 20,000 za Kenya, hati ya kusafiria na Sh 80,000 za Tanzania.
Umati ulipigwa butwaa, na kisha Mchungaji Masapila alimwangia dawa mwilini na kumwamuru aondoke eneo hilo haraka. Kijana huyo alianza kuondoka huku akiomba msamaha.

Kijana alitambuliwa kuwa ni mkazi wa Mkoa wa Singida. Hata hivyo, alipandishwa kwenye basi lililokuwa likienda Shinyanga.
Source: Newhabari
Best Blogger Tips
Gabo ajadili namna ya kujisalimisha


Umoja wa Mataifa umesema majenerali watatu wanaomtii Rais Laurent Gbagbo aliyezingirwa nchini Ivory Coast wanajadiliana masharti ya kujisalimisha na huku wakitaka wahakikishiwe usalama wao pamoja na wa Bw Gbagbo.

Ufaransa umesema wapatanishi hao wanakaribia kukubaliana kuhusu kuondoka kwake.
Bw Gbagbo amejihifadhi na familia yake kwenye handaki lililopo ndani ya nyumba yake kwenye mji mkuu, Abidjan.

Majeshi yanayomtii mpinzani wa Bw Gbagbo, anayetambuliwa na umoja wa mataifa Alassane Ouattara, yamesema yamezunguka nyumba yake hiyo.

Umoja huo umesema jeshi la Bw Gbagbo na washauri wake wanamkimbia.

Umoja wa Mataifa ulimweleza mwandishi wa BBC Andrew Harding, ambaye yuko nje ya mji wa Abidjan kuwa majenerali watatu wa Bw Gbagbo- mkuu wa majeshi, mkuu wa polisi na mkuu wa walinzi wa Jamhuri-wameanzisha mazungumzo.
Source: BBC

Monday, April 4, 2011

Best Blogger Tips
UConn wins National Championship

On a night when the massive arena felt like a dusty old gym, UConn made Butler look like the underdog it really was, winning the national championship Monday night with an old-fashioned, grinding 53-41 beatdown of the Bulldogs.

Walker finished with 16 points for the Huskies (32-9), who won their 11th consecutive game since closing the regular season with a 9-9 Big East record that foreshadowed none of this.

They closed it out with a defensive showing for the ages, holding Butler to a 12-for-64 shooting. That's 18.8 percent, the worst ever in a title game.

It was one of the ugliest games anyone can remember on the sport's biggest stage. But definitely the kind of game a grizzled old coach like Jim Calhoun could love.

At age 68, he became the oldest coach to win the NCAA championship and joined John Wooden, Adolph Rupp, Mike Krzyzewski and Bob Knight as only the fifth coach to win three NCAA titles.

"It may be the happiest moment of my life," Calhoun said.

Calhoun coaxed this win out of his team by accepting the reality that the rim looked about as wide as a pancake on a cold-shooting, defensive-minded night in Houston. He did it by making his players pound the ball inside and insisting on the kind of defense that UConn played during this remarkable run, but which often got overshadowed by Walker's theatrics.

UConn trailed 22-19 after a first half that came straight out of the '40s.

"The halftime speech was rather interesting," Calhoun said. "The adjustment was, we were going to out-will them and outwork them."
Access the full story......................

Sunday, April 3, 2011

Best Blogger Tips
Wabunge 'mabubu' wanyooshewa kidole

Via Majira

UTAFITI uliofanywa juu ya utendaji kazi wa wabunge, katika bunge la tisa, umetoa tahadhari kwa wabunge wa bunge la 10 wasiochangia kukaa
mkao wa kutorudi bungeni, huku vyama vyao vikihadharishwa kuwa vitaadhibiwa kwa kuzidi kupoteza wawakilishi.

Tahadhari hiyo imetokana na utafiti huo kubaini kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, moja ya vigezo ambavyo wapiga kura walivitumia ilikuwa ni kuzingatia kiwango cha ushiriki wa wabunge katika bunge la tisa.

Kutokana na kuzingatia kiwango hicho cha kushiriki katika kuchangia mijadala, chama kilichokuwa na ushiriki mdogo bungeni, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeonekana kuadhibiwa kwa kupoteza viti vingi, ambapo chama kilichokuwa na ushiriki mkubwa bungeni (CHADEMA) kimefanikiwa kuongeza viti.

"Kidokezo kinachojitokeza katika matokeo haya kwa bunge la 10 ni kwamba vyama vya siasa vyenye nia ya kukua katika siku zijazo vitahitaji kuwahimiza wabunge wao kuwa washiriki wazuri katika shughuli za bunge," imesema sehemu ya utafiti huo uliofanywa na asasi binafsi maarufu ya Uwazi, iliyoko chini ya Twaweza.

Asasi hiyo ambayo imeshafanya tafiti mbalimbali, zilizoibua mijadala mikubwa nchini, ikiwa ni changamoto kwa wahusika, kama ule wa wahitimu wa darasa la saba kutoweza kumudu masomo ya darasa la pili, imetumia tovuti ya bunge katika kukusanya takwimu za taarifa yake hiyo.
Endelea kusoma habari hii.......................
Best Blogger Tips

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma Salamu za Rambirambi kufuatia kifo cha Mwandishi wa Habari maarufu, Adam Lusekelo kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili siku ya Ijumaa tarehe 1 Aprili, 2011 kutokana na ugonjwa wa kisukari.

Katika salamu zake hizo, Rais Kikwete amesema alimfahamu vema Marehemu Adam Lusekelo kwa jitihada zake kubwa za kuendeleza Taaluma ya Uandishi wa Habari kwa kuandikia magazeti mbalimbali hapa nchini yakiwemo magazeti maarufu ya Serikali ya Daily News na Habari Leo.

“Ninamkumbuka zaidi Marehemu Lusekelo kwa safu yake maafuru ya “The Light Touch” iliyokuwa na mafundisho muhimu kwa jamii yetu”, amesema Rais Kikwete na kuongeza, “Kifo cha Marehemu Adam Lusekelo ni pigo kubwa kwa Taaluma ya Uandishi wa Habari na Wanahabari wenyewe hapa nchini, na kimeacha pengo kubwa katika Taaluma hiyo ambalo si rahisi kuzibika”.

Katika salamu zake hizo, Rais Kikwete ametoa pole kwa familia ya marehemu Lusekelo kutokana na kuondokewa na mpendwa wao ambaye amesema alikuwa mhimili madhubuti na tegemeo kubwa kwa ustawi wa familia.

Aidha, amesema yeye binafsi yuko pamoja na familia ya marehemu Lusekelo katika maombolezo ya msiba huo mkubwa, na amewaomba wawe na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya Marehemu Adam Lusekelo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
03 Aprili, 2011

Friday, April 1, 2011

Best Blogger Tips
Adam Lusekelo afariki dunia

 

MWANDISHI mahiri nchini, Adam Lusekelo (54), amefariki dunia usiku wa kuamkia jana wakati alipokuwa anakimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu, mke wa marehemu Scolastica Lusekelo amebainisha jana.

Alisema afya ya marehemu ilidhoofu usiku wa juzi na waliamua kumpeleka hospitali ya Aga Khan, lakini nao walikata shauri na kumhamishia Muhimbili na mauti ilimfika akiwa njiani kupelekwa hospitali hiyo ya rufaa.

“Oh, no! Tumempoteza kipenzi cha wasomaji wa gazeti la ‘Sunday News’,” alisema kwa masikitiko Mhariri Ichikaeli Maro mara baada ya kupokea taarifa za kifo cha Lusekelo.

Lusekelo atakumbukwa na wasomaji wa magazeti ya serikali ya Sunday News alikokuwa akichangia kwenye safu ya A Light Touch na HabariLeo kwenye safu ya Chombezo la Lusekelo.

Safu zake zilikuwa na utofauti kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuandika masuala muhimu ya kitaifa kwa lugha laini, jambo ambalo liligusa mioyo na nafsi za wapenzi wake.

“Mume wangu atapungukiwa na kitu kwa sababu alikuwa mpenzi sana wa safu ya Lusekelo,” alisema Joyce Sabuni, mfanyakazi wa Tanzania Standard Newspapers (TSN) inayochapisha magazeti ya DAILY NEWS, SUNDAY NEWS, HABARILEO na HABARILEO Jumapili, katika kitengo cha usambazaji.

Kaimu Mhariri Mtendaji wa TNS, Mkumbwa Ally ni miongoni mwa watu walioguswa na msiba wa kifo cha mwandishi huyo mkongwe aliyekuwa na kipaji cha hali ya juu katika fani ya uandishi wa habari.

Kaka wa marehemu, Ben Mwakang’ata alisema mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake Ubungo na kuwa upo uwezekano mwili wa marehemu ukasafirishwa kesho kuelekea Rungwe, mkoani Mbeya.

Marehemu Lusekelo ameacha mke na watoto watatu, wakiwemo wawili wa kike.

Katika uhai wake alifanya kazi TSN kwa muda mfupi katika miaka ya 1980 kabla ya kujiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kama mwandishi wa habari akiandikia akiwa Dar es Salaam.

Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits