Saturday, April 16, 2011

Best Blogger Tips
Zito aibua ufisadi mpya

Via Newhabari

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (CCM), Kabwe Zitto, ameibua ufisadi mpya na wa kutisha unaoonyesha kuwa zaidi ya Sh bilioni 48 zimetafunwa na wajanja.

Zitto alimbana Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jana, ambapo alisema kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, fedha hizo zilipotea katika utaratibu wa mpango wa kuhuisha uchumi (stimulus package) ambapo Bunge lilipitisha bajeti ya dharura ya Sh trilioni 1.7.

Zitto aliuliza: “Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu, katika bajeti ya mwaka 2009/2010 Serikali ilileta Bunge mapendekezo ya kutenga zaidi ya shilingi trilioni 1.7 kwa ajili ya kuhuisha uchumi (stimulus package) na Serikali iliahidi hapa Bungeni ya kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atafanya ukaguzi maalumkwenye eneo hili.

“Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ametoa taarifa yake. Katika taarifa yake pamoja na kuonyesha kwamba kuna zaidi ya shilingi bilioni 48 ambazo ameshindwa kuzithibitisha kama zilitoka kwa taratibu zinazotakiwa. Lakini pia amesema kwamba Serikali imemnyima taarifa muhimu ikiwemo orodha ya watu na makampuni ambayo yalifaidika na mpango huu. Mheshimiwa Waziri Mkuu unatoa kauli gani kuhusu suala hili?”

Baada ya hoja hiyo ya Zitto, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema: “Mheshimiwa Spika, sijui Mheshimiwa Kabwe maana mimi ndio Waziri Mkuu, ndio ninayeshughulika na masuala ya Serikali kwa upana wake. Kwa bahati mbaya sana hiyo taarifa kwamba aliomba baadhi ya taarifa kutoka Serikali tukamnyima mimi nilikuwa sijazipata na kwa sababu taarifa hizo na mimi nimezipata juzi yaani kwa maana ya ma-book yale na so long ndio nazipitia labda nipe nafasi nikishapata nafasi ya kuipitia then tuta-take up issue seriously kwa sababu hatuna sababu ya kumnyima yeye ndio Mkaguzi wa Hesabu na kwa nini tusiseme hapana.”
Endelea kusoma habari hii...............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits