Tuesday, April 12, 2011

Best Blogger Tips
Hosni Mubarak hali mahututi hospitalini Cairo

Via BBC

Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak amelazwa hospitalini akiwa katika hali mahututi mjini Cairo. Awali MUbarak alilazwa katika hospitali moja eneo la kitalii la Sharm Sheikh.

Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kuwa alipata mshtuko wa moyo alipokuwa akihojiwa na wachunguzi juu ya mauaji yaliyofanywa dhidi ya waandamanaji nchini Misri.

Televisheni ya kitaifa ya Misri imenukuu baadhi ya madaktari wakisema kuwa Muabarak alikataa kula wala kunywa baada ya kuagizwa kufika mbele ya mwedesha mashtaka mkuu, pamoja na wanawe, yapata siku mbili sasa.

kwa sasa anatibiwa magojwa ya moyo katika hospitali ya Sharm Al sheikh, ambapo madakitari wanasema kuwa anaendelea vyema.

Usalama wa hali ya juu umewekwa katika hospitali. Bwana Mubarak aliye na umri wa miaka 82 aliripotiwa kuzorota afya yake baada ya upasuaji wa moyo aliyo fanyiwa nchini Ujerumani mwaka jana.
Hata hivyo marafiki zake wa karibu zaidi wamesisitiza kuwa hali yake iko shwari.

Mamia ya waandamanaji walisalia katika hospitali hiyo baada ya maandamano ya ijumaa, na wamesisitiza kuwa wataendelea kuketi hapo hadi pale kiongozi huyo atafunguliwa mashtaka.

Wakati huo huo jeshi pamoja na polisi wameizingira bustani ya Taharir ambapo kumekuwa na waandamanaji wanaoshinikiza kuwepo na utawala wa kiraia pamoja na kushtakiwa kwa watawala waliong'olewa madarakani.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits