Via BBC
Kundi la maafisa kutoka Umoja wa Mataifa limetumwa mjini Tripoli kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Libya.
Serikali ya Libya imesema itashirikiana na jopo hilo la wachunguzi ambalo pia litachunguza madai ya dhulma zilizotekelezwa na waasi na majeshi ya Nato.
Kuna taarifa kuwa tangu maandamano ya kumpinga Kanali Gaddafi yaanze watu wametoweka, wengine wameteswa na hata kuuawa.
Kamishna wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay alisema kuwa huenda uhalifu dhidi ya binadamu unafanyika nchini Libya tangu mzozo huo uanze.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema zaidi ya watu elfu moja wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika mapigano hayo.
Meli zimekuwa zikiwasafirisha watu waliojeruhiwa hadi mjini Benghazi kupata huduma za matibabu.
No comments:
Post a Comment