Waziri mwingine atua Samunge
Via Mwananchi
NAIBU Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chizza na familia yake, jana walikuwa miongoni mwa watu waliopata kikombe cha tiba ya magonjwa sugu kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila katika Kijiji cha Samunge, Loliondo.
Chizza aliwasili Samunge akiwa na mkewe na wanafamilia wengine na kupokewa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali. Mbali ya kupata kikombe, alitumia fursa hiyo pia kumpa pole mchungaji huyo ambaye amefiwa na mtoto wake.
Akizungumza mara baada ya kupata kikombe cha tiba, Chizza alisema ni wajibu wa Serikali kuboresha miundombinu ya kufika Samunge kutokana na watu wengi wa ndani na nje ya nchi kwenda Samunge."Bado barabara siyo nzuri na mazingira ya Samunge ni machafu. Ni wajibu wa Serikali kuboresha miundombinu na utaratibu wa kutunza mazingira," alisema Chizza.
Waziri huyo ambaye alifika Samunge kwa gari alisema, ameamua kutumia mapumziko ya Pasaka kwenda Samunge kupata tiba baada ya kusoma habari za Mchungaji Mwasapila na kupata taarifa za watu kupona magonjwa mbalimbali.
Robo tatu ya magari Samunge yatokea Kenya
Raia wa Kenya, juzi na jana walitinga kwa wingi hapa Samunge na kufanya karibu robo tatu ya magari yaliyokuwapo hapa kutoka nchi hiyo jirani. Mengi ya magari hayo ni mabasi madogo, maarufu kama matatu (daladala).
Wakenya hao waliingia kuanzia juzi usiku na kutawala Viwanja vya Samunge, huku magari machache ya Watanzania yakianza kuingia jana asubuhi.Licha ya Wakenya, raia wa Rwanda na Uganda jana walitinga Samunge na kupata kikombe na sasa idadi ya wageni kutoka nje ya nchi waliofika Samunge, imefikia zaidi ya 13,700.
Endelea kusoma habari hii...................................
Tuesday, April 26, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment