Nato yashambulia waasi inaowasaidia
Waasi mashariki mwa Libya wanasema majeshi yao yamepigwa na majeshi ya Nato katika shambulizi la anga - kwa bahati mbaya.
Madaktari mjini Adjabiya wameiambia BBC kuwa wapignaji wasiopungua 13 wa waasi wameuawa katika shambulio hilo.
Mwandishi wa BBC Wyre Davies ameripoti kuwepo kwa mkanganyiko katika viunga vya Adjabiya, huku majeshi ya waasi yakirudi nyuma na kutoa taarifa za kushambuliwa na ndege za Nato.
Hili ni tukio la tatu kutokea katika siku za hivi karibuni, kuhusiana na majeshi ya kimataifa yaliyopelekwa kulinda raia wa Libya.
Kamanda mmoja wa waasi ameiambia BBC kuwa aliona mabomu yasiyopungua manne yakianguka katika eneo la wapiganaji wa waasi.
Watu wengi wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa, amesema kamanda huyo.
Raia wanaripotiwa kukimbia mji wa Adjabiya kwa maelfu, kwa mujibu wa taarifa vya mashirika mbalimbali ya habari, kufuatia tetesi kuwa majeshi ya Gaddafi yanajiandaa kushambulia jiji.
Waasi walikuwa wakipeleka mizinga, magari ya ijeshi na mabomu ya kudungua ndege katika na uwanja wa mapambano, katikati ya miji ya Adjabiya na Brega, kwenye msafara wa zaidi ya magari 30.
Source: BBC
Thursday, April 7, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment